Why is Marcelo Bielsa so underrated?

Emmahu

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2014
Posts
977
Reaction score
1,713
Wajuzi wa mambo, kuna huyu kocha mkongwe muargentina ninaemkubali sana anafahamika kama Marcelo Bielsa ambae kwasasa anafundisha pale Leeds Utd.

Navutiwa sana na style yake ya soka la pasi nyingi na kushambulia kwa kasi, nasikia hata Pep aliiba maufundi kwa huyu mwamba. Sasa ninachojiuliza kwanini timu kubwa hazihangaiki na huyu kocha?

Ukiangalia historia yake kafundisha vitimu vidogo kama Lille and the likes. Timu kama Man Utd inamng'ang'ania mmasai Ole Gunnar wakat Bielsa yupo, Barca mfumo wao unafanana na Bielsa lakin wapo na kocha alieshindwa timu mapema, Madrid nao ni kama hawamuoni wameangukia kwa Ancelotti, hata Arsenal nayo jamani ni kubwa kwa Bielsa!!? Sitaki kuamini labda kuna kitu nyuma ya pazia kuhusiana na huyu gwiji.

Kuna madhaifu gani kiufundi kwa huyu kocha? nakukumbuka lile pira lake lililowatoa jasho Spain kwenye world cup ya 2010 wakat huo akiwa kocha wa Chile, na Bilbao yake iliomsumbua mzee Fergie pale OT.

Kwa anaemfaham kiundani atudadavulie kuhusu huyu mwamba.

 
Kama club kubwa zote hawamuoni , inabidi aje aichue yanga sasa.
Ili nao wao wacheze mpira sambusa
 
Huyu jamaa ndiye mwalimu original kabisa wa Pep Guardiola pamoja na diego simeone aliwafundisha wote wawili ..guardiola anasema wakati anastafu soka alikwenda moja kwa moja mpaka argentina wakati huo bielsa hana timu kufika na kufika alimkuta tayari ana mifumo yote ya mpira wanayotumia timu za premier league mpaka championship waliidadavua na kuichambua kwa mapana huyu jamaa ni smart sana.

Kutokuepo timu kubwa wala sio swala hizi timu kubwa kama Man united na Arsenal zinaamini katika mipango ya muda mrefu kuyumba kwa Man united sasa hakumfanyi OGS kuwa mbaya la hasha bali anaandaliwa kuwa katika mpango wa muda mrefu kwa sababu ni zao lao ndio sababu hata Sir Alex miaka yake ya mwanzo alifanya vibaya sana kwa OGS ni swala la muda tu ni vitu vidogovidogo tu akifanyia kazi atakua bora ni swala la muda yeye na Arteta
 

Timu ya Taifa kwanini wasimchukue?
 
Nahisi sikui nyota pia hana.. Mzee ni bonge la kocha, mie ili kocha awe mzuri kwangu ni lazima awe mkali wa mbinu.. Tajiri wa mifumo, kubadilika muda wowote kutegemea game ilivyo.
 
Alisha fundisha argentina nadhani ya 2002

Wangemuita tena aiweke sawa. Timu kubwa kama ile inakosaje makocha wazuri bwana...Simeon(Cholo) , Bielsa or Pocchetino hawa makocha walikuwa wanafaa sana kuifundisha timu ya taifa.
 
Wangemuita tena aiweke sawa. Timu kubwa kama ile inakosaje makocha wazuri bwana...Simeon(Cholo) , Bielsa or Pocchetino hawa makocha walikuwa wanafaa sana kuifundisha timu ya taifa.
Mie nadhani tatizo kubwa ni kukosa team coordination angalia 2018 world cup team ulikuwa na potential players but lack of coordination
Mfano team selection was poor
 
Shida ya Bielsa ana ubishi fulani ..hivi
Timu kubwa zina siasa Sana
Mfano Madrid anaesajili ni Perez na sio kocha
Chelsea Abrohomovic ndie final say..

Bielsa anataka awe na Uhuru wa kusajili na kupanga timu ...

Kingine Bielsa hataki kabisa mpira wa Ku defend ...falsafa yake ni kufunguka mpira uchezwe ...hii ndo maana sometimes Leeds wanapigwa nyingi

Halafu Bielsa hawawezi wachezaji ma star wa kizaz cha sasa cha kina Pogba ..

Yeye anataka wachezaji wakimbie dakika zote 90....hawa ma star watamgomea atafukuzwa

Ndo maana akienda timu kama Madrid hamalizi miezi mitatu
 
Nahisi sikui nyota pia hana.. Mzee ni bonge la kocha, mie ili kocha awe mzuri kwangu ni lazima awe mkali wa mbinu.. Tajiri wa mifumo, kubadilika muda wowote kutegemea game ilivyo.
Bielsa anabadilika? Ni 4 1 4 1 haina kuremba. Kila timu anaipelekea moto mwanzo mwisho hamna kubadilika kutokana na mpinzani. Ni kama Klopp.

Kocha ambaye ni skilled kwa mbinu na anabadilisha mifumo game ikiendelea kwa kipindi hichi nimeona Carlo akifanya hivyo sana alipokua Everton.
 
Hii yenyewe imetoka kwa formation yake nguli ya 3-3-1-3
 
Bielsa nafikiri ataenjoy mpira wa Spain kuliko England. Spain kila timu inacheza mpira wa kasi na kushambulia wakati Uingereza kuna timu zinajulikana kabisa kwamba ukikutana nazo wao mpango ni kupaki basi na zingine zinategemea counter tu.

So mfano anaipata timu kama Sevilla au Sociedad lazima ataenjoy kwakua ni timu ambazo hazina presha na media hivyo atakua huru. Nafikiri ameonekana mzuri Leeds kwavile haina presha pia, I mean Arsenal ina makando kando kibao lakini lawama anagewa Arteta unlike na timu kama Leeds ambayo mashabiki wanatarajia timu isishuke daraja na iperform hapa na pale not consistently.
 
Nilikua sifahama kama Simeoni "el cholo' nae kafundishwa na Bielsa, sasa lile pira lake sijui tuliiteje maana ni zaidi ya gwaride tofauti kabisa na falsafa za babu.
 
Mwishoni mwa ligi alibadili mfumo baada ya kuona anaruhusu bao nyingi, niliona anatumia sana 3-3-3-1 na ililipa sana.
 
Nilikua sifahama kama Simeoni "el cholo' nae kafundishwa na Bielsa, sasa lile pira lake sijui tuliiteje maana ni zaidi ya gwaride tofauti kabisa na falsafa za babu.
Na ndio maana babu hamzimii saana el cholo..

Ila ukilitizama pira la atletico kuna kipindi anaweka pira chini, zinagongwa pasi burudani. Kuna wakati anapiga pasi na wanakwenda kushambulia kwa speed kinoma.
 
Na ndio maana babu hamzimii saana el cholo..

Ila ukilitizama pira la atletico kuna kipindi anaweka pira chini, zinagongwa pasi burudani. Kuna wakati anapiga pasi na wanakwenda kushambulia kwa speed kinoma.
Atm ya msimu huu iliyochukua kombe ni ambayo hata haikutarajiwa. Ushindi ulikua unapatikana kwa nguvu kubwa na ikafikia kipindi Felix akakaa kando na Carasco akawaoutshine aliowakuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…