- Kiswahili kilibuniwa kwa usaidizi wa mwarabu kwenye pwani za Tanzania na Kenya kabla ya mwalimu Nyerere
- Lakini yeye ndiye aliwasisitizia mkitumie
- WaTz wanachukia Kingereza kwa ajili ya kushindwa kukiongea, bwana nimefanya shughuli nyingi na Wabongo kwenye corporates zenu, naongea kitu ninachokifahamu.
- Ukosefu wa kuongea Kingereza unawatatiza kiuchumi maana Kiswahili kina mapungufu sana kwenye corporate world, halafu unakuta Bongo stakabadhi nyingi zipo kwa Kingereza, mambo mengi yameandikwa kwa Kingereza maana mmeshindwa kuyatafsiri hadi Kiswahili. Unapata ni wachache wenu wanaongea Kingereza vizuri, yaani watoto wa matajiri na elites na wanasiasa ndio wanapelekwa kwenye international schools, wengine wenu mmebaki saint Kayumba siku zote. halafu hao viongozi wanafiki sana, wanawasisitizia eti mpende Kiswahili wakati wanawapeleka watoto wao hizo shule ama Kenya.
Kuna mmoja alinishangaza sana, akiwa nje na watoto wake anaongea nao Kiswahili, lakini wakiwa ndani nyumbani inakua Kingereza kwenda mbele, yaani anaficha msimuone eti sio mzalendo.