HURUMA KWA VIUMBE WENGINE
Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi (Kumbukumbu la Torati 22:6–7)
Haki, huruma, na wema, na upendo ambao Neno la Mungu linatufundisha unaonekana kuwa ni kitu cha pekee sana. Maana vitu hivi vinatakiwa kuvuka mipaka na uelewa wetu kibinadamu. Ukichukua kwa mfano ile sheria ya kumpenda adui na kumwombea, ni kama haiji vile. Yaani nimwache adui yangu ili aendelee kunitesa! Lakini ukiongozwa na Roho wa Bwana, ndivyo utakavyofanya!
Mambo haya hayapaswi kuwa kwa binadamu tu! Ni kwa viumbe wote! Hata unapotaka kumchinja mnyama yeyote ili upate nyama, hutakiwi kumfanyia ukatili, hata kama kuua ni kuua.
Jambo hili linatuambia kuwa huruma na wema wa Mungu kwa viumbe wake ni wapekee. Hii ndio maana katika Biblia kuna mwongozo wa namna ya kupanda mazao pia. Sisi tunapofurahia kilimo cha mseto, Biblia inasema, usifanye hivyo, maana mazao mengine yataonewa. Hata kwa habari ya nguo za rangi mchanganyiko.
Hata hivyo hoja ya leo ipo kwenye kumchukua ndege pamoja na vitoto vyake. Ni jambo la aina yake na unaweza usione sababu ya kwa nini iwe hivi. Lakini ukweli ni kwamba Mungu anawalinda viumbe wote na kwa namna hii anaweka utaratibu wa kuwa kuhusiana nao na hata kupata huduma kutoka kwao. Tukiishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu, inaonekana mambo ni rahisi kabisa! Hata mvua zitanyesha kwa wakati! Mwaka huu inaonekana kuna jambo la pekee, maana projection ya mvua kwa mikoa mingi ya kusini huwa ni kuanza tarehe 15.11.2020, na ninaona imeanza sasa. Tuendelee kuishi kwa kufuata neema na utaratibu Mungu aliotupatia. MUNGU AKUBARIKI [emoji2399] Gerson Mgaya.
Sent from my SM-A715F using
JamiiForums mobile app