Ben Saanane: Kama watu wameficha fedha majumbani, TRA wanapata wapi makusanyo mnayodai yameongezeka?
Ombi: Rais Magufuli tumia zile Push-Ups ulizotuaminisha kuwa ndio kipimo cha Uongozi Shupavu badala ya kusingizia kwa vilio vya Lawama kuwa kuna watu wanaficha fedha ndio maana hali mbaya ya uchumi ili Uonewe huruma. Kama ulivyoonesha ushujaa kwenye Sakata la Sukari ,basi onesha Uhodari tena kwa hili la Walioficha fedha. Waagize wakuu wa mikoa na Wilaya kama akina Makonda waanze msako wa nyumba kwa nyumba kutafuta Maburungutu ya fedha zilizofichwa kama walivyofanya kwenye Sukari.Onesha Uimara na Ushupavu wako kama ulivyoonesha kwenye Kampeni Mzee Wetu. Vinginevyo isijekuwa Zile Pushups za kipindi kile zililenga kuwapumbaza watu wasiokuwa waelewa kama wale Raia walioishukuru kwa dhati kabisa serikali yako ya awamu ya Tano jana kwa kupeleka Tukio (Wao walisema Tamasha) la kupatwa na Jua Kule Mbarali jana.Wao waliamini ni wewe ulifanikisha kupatwa kwa Jua jana.Ona ulivyowajengea watu imani kwa Zile Push-ups Vilevile niandike kidogo tu kuhusu hili suala la kuficha fedha.Nimeshatahadharisha mara nyingi tu juu ya hatari ya kutoa matamshi ambayo sio taaluma au fani uliyobobea. Kwa mfano kwa mwanauchumi yeyote aliyesoma vizuri hawezi kuamini kuwa kuna fedha nyingi kiasi hicho ambazo zimefichwa hadi utoe uamuzi kuwa utachapisha noti mpya ili zilizofichwa ziwe karatasi tu Huku ni kutafuta kisingizio na kutafuta kuonewa huruma tu kwa ugumu wa maisha Niliwahi kusema kwa uchumi kama wa Tanzania ambako sekta binafsi bado haijatengamaa basi serikali ndio inapaswa kusisimua(Stimulate) uchumi kwa matumizi(Government expenditure). Serikali ndio iliyokua Consumer(Mlaji) wa huduma na bidhaa .Mfano mahotelini vikao vilikua vikifanyika.Kukawa na mzunguko wa fedha. Pia kwa sasa wawekezaji wanasita kuwekeza kwa sababu serikali ya awamu ya Tano haitabiriki na wawekezaji wengi hasa wenye asili ya kiasia(Wahindi) mara nyingi wapo makini kuwekeza.Niliwahi kuonya kwenye makala niliyomjibu Mwanahabari na Mchambuzi maahiri Godfrey Dilunga kuwa "Hatuhitaji Udikteta Kufikia Estada Novo(Taifa Jipya) " kwani serikali zinazofanya maamuzi ya kiimla hazitabiriki na hivyo wawekezaji husita kuwekeza Serikali inapotia pua yake kwenye kila biashara na kodi zisizotabirika inawafanya wawekezaji wa aina hii kuondoa fedha zao benki.Utawala wa awamu ya Tano unajua kukamua badala ya kutengeneza mazingira ya ukamuaji endelevu.Wao wanasimamia tax quantity badala ya Quality in terms of Efficiency Kauli ya Rais kuna walioficha fedha ni njia ya kutangaza hali ya uchumi ni ngumu lakini akataka kujinasua hapohapo kwa kusingizia watu. Anakwepa wajibu wake. Tuseme kuna watu walificha fedha tangu Novemba alipoingia madarakani ,hadi sasa karibia mwaka mzima si watakua wamezibadili ? Na wakizibadili zikawa kwa Dola ambayo ni stable currency and Internationally accepted si bado hizo shilingi zitakua kwenye mzunguko? Kwenye Uchumi kuna kitu kinaitwa Money Supply(MS) yaani Ugavi wa Fedha na kuna vizio M1, M2,M3 M1 ina kanuni zake yaani M1 Unazungumzia CC+DD CC ni Currency In Circulation(Fedha zilizopo kwenye Mzunguko + Demand Deposit(Amana) Sasa Rais Alizungumzia fedha imepungua kwenye Mzunguko na hivyo inahitajika ili mabenki yashushe Riba kisha Uwekezaji Uongezeke Kazi ya Benki ni kusisimua uchumi na inaitwa Financial Intermediary(Yaani Taasisi ya Kati kifedha) ambapo hupokea pesa za watu wanaoweka akiba/amana na benki wao hukopesha kwa watu Huwa benki wanawekewa kiwango na Benki Kuu.Benki kuu hutumia hizi benki za biashara kisheria na kikanuni katika kupunguza fedha mikononi mwa watu au kuongeza na hivyohivyo kudhibiti mfumuko wa bei Kukiwa na fedha nyingi mitaani Benki kuu hupandisha Riba inayowalazimu benki ya Biashara kupandisha riba na masharti magumu zaidi unapoenda kukopa na kinyume chake Sasa Rais anajua Gavana ndie alipaswa kuliongelea hili kitaalamu zaidi Hili la kuchapisha Noti mpya lingekuja ikiwa kuna noti bandia nyingi.Tena inakuja kama last resort. Rais angejihangaisha na washauri wake kuangalia kuwa Tanzania ni mojawapo wa vinara wa Mobile Banking Hapa Afrika kwa mzunguko mwingi kupitia Simu za Mikononi kama M-Pesa na Tigo Pesa Pia Rais alipaswa ku-address kwanza tatizo kubwa tulilo nalo hasa udhibiti wa Uwekezaji kwenye ardhi na Majengo(Real Estates Regulation) Watakatishaji fedha (Money Launders)wote hodari hutakatisha fedha kwa kutumia Real Estates Badala ya Kuweka fedha nyumbani hununua majengo .Angejiuliza ni kwanini bei za majumba zimepanda kwa kasi ya kutisha? Lakini hata kama walinunua bado fedha zingekua kwenye mzunguko Kuchapa fedha ni gharama. Mbinu hizi za kuchapa fedha mpya ziliwahi kwenda out of control mwaka 1920 kule Ujerumani na kusababisha Mfumuko wa Kutisha Dikteta Idd Amini alipoona uchumi mbaya aliamuru fedha zichapishwe.Yaani it was crazy Mugabe nae hapo Zimbabwe hivi majuzi Mbinu ya Rais kutishia kuchapisha fedha ni kutaka kutumia mwanya huo kuchapisha fedha kuongeza kwenye mzunguko badala ya anachotaka kuaminisha kuwa anafanya replacement ya fedha zilizofichwa Uchapishaji huo ni hatari zaidi kwa uchumi Inaweza kupelekea kukawa na fedha nyingi kwenye mzunguko hivyo kusababisha uhaba wa bidhaa na huduma kulingana na idadi kubwa ya fedha zilizopo mitaani(Too much money chasing few products) na pia ununuzi wa bond za Serikali kusababisha kupanda bei katika masoko ya fedha kimataifa na hivyo kushusha thamani ya sarafu yetu zaidi na nchi yetu hii "Tanzania Ya Magufuli ya Viwanda" ikazidi kuwa hatari Rais amuagize Gavana,Washauri wake wa Uchumi na wadau wengine waangalie mfumo wetu wa Kodi,Real Estates na Banking System katika kuleta harmonization katika ujenzi wa Uchumi na piakupambana na ufisadi Uchumi wa nchi huendeshwa kwa principles za kiuchumi na sio presidential decrees kama zile za akina Idd Amin,Mugabe hivi majuzi na Weimer kule Ujerumani ya 1920 Hatutaki kununua mchicha sokoni tukajikuta tunafunga safari na viroba vya Fedha kama Ujerumani na zimbabwe Vinginevyo ule ufanisi wa Pushups kwenye sukari unaweza kuzaa matunda hapa labda Sijui leo Huko Pemba atatoa lipi jipya tena maana kila aongeapo huzua mtafaruku.Usishangae akajisahu na kujisifu TRA wamevuka malengo ya kukusanya kodi.Ina maana hela zinatoka wapi? Sitarajii Waziri au Gavana aibuke na kudai Rais alikua anatania kuwa atachapa fedha mpya ndani ya Siku mbili wakati anajua kuna process ndefu . Ni Mwendo wa Kufyatua Watoto,Kufyatua Maneno na kisha kufyatua fedha na kisha .... Asisahau kuwakumbusha Wazanzibari kuwa yeye kaenda tuu huko kwao ambako hana mamlaka nako maana kuna tume yake na Rais Wake... Aluta Continua,Victory Ascerta.... Ben Saanane
https://www.jamiiforums.com/index.php?posts/17450347/