Hili la Waislam wa Sunni na Shia kugombea nyama ya ngamia mpaka wanapigana inatokea sana.
Tuache hilo, umejibu kihekima sana leo, ila Nina swali kwako na kwa members wengine
Kuna Workmate mwenzetu mmoja amekuja majuzi, tukazoeana kidogo ikaja mada ya kutambuana kidini akasema yeye si Muislam na si Mkristo ni MBAHA'I
Nikampeleleza zaidi na kugundua mambo kadha wa kadha ambayo sikuwa nayafahamu kabla.
Mwanzilishi wa dini hii ni BAHA 'U LLAH aliyekuwa Mpersia
Kitabu kitakatifu kwao ni ''KITAB - i - AQDAS''
Wanaabudu kila baada ya siku 19 ya kupokea mwezi.
Hawafanyi Injili wala kuhubiria watu ili wajoin katika dini yao
Wanakula vyakula vyote
Wanatumia lugha ya kiarabu kufanyia ibada.
Kutoa sadaka si lazima na wala haipo katika taratibu za ibada yao, na wanajali sana vitu viwili tu
1) Familia hasa katika suala la chakula
2) Elimu
Na viongozi wao wa kidini wana influence kubwa sana na hata kuingilia familia ya muumini wao na kujua bajeti ya kila area kwenye familia.
Hawa watu wapo ndani ndani mwa nchi yetu na wanatambuana sana lakini sijui kwanini wanajificha sana, ingawa wanawaelewa sana Waislam.
Nani anawafahamu zaidi hawa Wabahai?
Che mittoga safuher Mokaze
mgen