Why should I confess?

Why should I confess?

Uongo ulikunywa we kenge ulivyo mroho uligeuza hadi chupa nje ndani ukailamba.
Dah au sio 😃,
FB_IMG_17289131352517594.jpg
 
Natumai wote mu wazima wa afya,.

But why am writting this?,. Why should i do this?.. Sina majibu mpaka sasa wakati huu ninavyoandika.....

Wacha niandike tu bhana huwenda nikapunguza mzigo moyoni,. Mtanisamehe kwasabu ni ndefu kidogo😑😑

Ni kwamba najuta kuwa na cycle ya watu ambao niko nao sasa,. Nisipokuwa makini naweza kuangukia kwenye midomo ya mamba..

Tuanze sasa,. Ilikuwa ni 2022 mwishoni kama sikosei alikuja mdada ofisini kwetu,. Naweza kusema ni aina ya hii midada ya mjini wale ambao maisha wanayoishi na vibiashara wanavyofanya ni vitu viwili tofauti yaani type ya wale wadada naweza kusema ni wadangaji wa mjini waliokubuhu/shindikanaa kabisa ( wale wenye matatoo mara mableach, wengine wamejitoboa hadi kwenye vitovu wameweka vipini )...

Nilimhudumia vizuri sana ukizingatia na nlivyo charming sikuwa hata nimemchukulia tofauti kama wenzangu walivyomchukulia,. Basi wakati anatoka akaniomba namba nikampatia alivyofika kwenye gari yake nje akanitumia text nimfate mara moja nikatoka akaniambia nilitaka nikupatie pesa ya soda maana umenihudumia vizuri lakini isingekuwa vizuri kukupa mbele ya wenzio baasi nikachekacheka pale nikapokea nikarudi kuendelea na kazi..

Baada ya kama mwezi hivi akawa ameniletea na marafiki zake,. Na hao marafiki zake ndio walewale tu,. Ila tu kila mmoja alikuwa anakuja kwa nafasi yake na walichokua wanasisitiza ni kwamba nisije nikaropoka flani naye alikuja maana yule wa kwanza alinitambulisha tu kama nendeni sehemu flani kuna mdogo wangu yupo basii. Si unajua midada ya mjini kuvimbiana hakuna anayetaka aonekane kaishiwa mbele ya wenzie..

Kiukweli ni watu ambao sijui ndio walikua wananipenda au walikuwa wanapenda ninavyowahudumia,. Maana ilikuwa kama desturi tu wakija lazima waniachie hela za maji yaani mtu kukupa 50k kwakwe sio shida zake,. Ukiachana na hivyo utakuta hata kama mtu anapita maeneo ya ofsini atakupigia akuulize kama ulikula kama bado atakwambia njoo sehemu flani basi tule ukienda utarudi na mazaga kibao,. Atakutambulisha kwa wenzie na wenzake nao ndio walewale wananimwagia upendo kama wote baasi nikawa najiona ndugu si ndio hawa nimepata kumbee😓😓....

Waliendelea hivyo hivyo mpaka ikafika kipindi wote wakawa wananitreat kama mdogo wao yaani,. Kuna zile nyakati labda wamepost status wako China sijui Dubai wanasema wamefata mizigo ya biashara zao,. Mie nikireply tu naulizwa nikirudi nikuletee nini najibu chochote lakini wakirudi wanarudi na hiyo mipackage mpaka nasema hivi huu upendo mbona kama umepitiliza lakini nikawa najionea tu raha nasema kweli nimepata nduguu...

Ngoja kwanza ninywe chai nakuja🙌
Jihadhari na mishangingi ya mjini (gold diggers), watakakuua mkuu. Usithubutu kuzoeana nao kamwe! Waogope kama ukoma.
 
Dunia ya sasa mtu msiejuana kukupakupa vitu ni lazima uwe na tahadhari aisee.

Ila kwa nature ya wadada sio rahisi kuahtukia mchezo maana wameshazoezwa kupokea, ila kwa sisi Me kupewapewa vizawadi namna hiyo lazima mwenye akioi timamu angeshawasha double hazard.
Mimi ningeweka four wheel kabisa🤣
 
Natumai wote mu wazima wa afya,.

But why am writting this?,. Why should i do this?.. Sina majibu mpaka sasa wakati huu ninavyoandika.....

Wacha niandike tu bhana huwenda nikapunguza mzigo moyoni,. Mtanisamehe kwasabu ni ndefu kidogo😑😑

Ni kwamba najuta kuwa na cycle ya watu ambao niko nao sasa,. Nisipokuwa makini naweza kuangukia kwenye midomo ya mamba..

Tuanze sasa,. Ilikuwa ni 2022 mwishoni kama sikosei alikuja mdada ofisini kwetu,. Naweza kusema ni aina ya hii midada ya mjini wale ambao maisha wanayoishi na vibiashara wanavyofanya ni vitu viwili tofauti yaani type ya wale wadada naweza kusema ni wadangaji wa mjini waliokubuhu/shindikanaa kabisa ( wale wenye matatoo mara mableach, wengine wamejitoboa hadi kwenye vitovu wameweka vipini )...

Nilimhudumia vizuri sana ukizingatia na nlivyo charming sikuwa hata nimemchukulia tofauti kama wenzangu walivyomchukulia,. Basi wakati anatoka akaniomba namba nikampatia alivyofika kwenye gari yake nje akanitumia text nimfate mara moja nikatoka akaniambia nilitaka nikupatie pesa ya soda maana umenihudumia vizuri lakini isingekuwa vizuri kukupa mbele ya wenzio baasi nikachekacheka pale nikapokea nikarudi kuendelea na kazi..

Baada ya kama mwezi hivi akawa ameniletea na marafiki zake,. Na hao marafiki zake ndio walewale tu,. Ila tu kila mmoja alikuwa anakuja kwa nafasi yake na walichokua wanasisitiza ni kwamba nisije nikaropoka flani naye alikuja maana yule wa kwanza alinitambulisha tu kama nendeni sehemu flani kuna mdogo wangu yupo basii. Si unajua midada ya mjini kuvimbiana hakuna anayetaka aonekane kaishiwa mbele ya wenzie..

Kiukweli ni watu ambao sijui ndio walikua wananipenda au walikuwa wanapenda ninavyowahudumia,. Maana ilikuwa kama desturi tu wakija lazima waniachie hela za maji yaani mtu kukupa 50k kwakwe sio shida zake,. Ukiachana na hivyo utakuta hata kama mtu anapita maeneo ya ofsini atakupigia akuulize kama ulikula kama bado atakwambia njoo sehemu flani basi tule ukienda utarudi na mazaga kibao,. Atakutambulisha kwa wenzie na wenzake nao ndio walewale wananimwagia upendo kama wote baasi nikawa najiona ndugu si ndio hawa nimepata kumbee😓😓....

Waliendelea hivyo hivyo mpaka ikafika kipindi wote wakawa wananitreat kama mdogo wao yaani,. Kuna zile nyakati labda wamepost status wako China sijui Dubai wanasema wamefata mizigo ya biashara zao,. Mie nikireply tu naulizwa nikirudi nikuletee nini najibu chochote lakini wakirudi wanarudi na hiyo mipackage mpaka nasema hivi huu upendo mbona kama umepitiliza lakini nikawa najionea tu raha nasema kweli nimepata nduguu...

Ngoja kwanza ninywe chai nakuja🙌
Jilaumu kwa kutokuwa ethical na kujirahisisha
 
Wameshakurekodi Picha Zako Za Utupu Na Kukusaga Na Kama Ulivyosema Ukinywa Tungi Hujitambui Siku Ukijifanya Mjanja Kuwakataa Wanafanya Yao,,Kazi Kwako Sasa Kuwa Mtumwa Wao Pale Watakapo Amua Kukutuma Lolote Lile
 
Back
Top Bottom