Unamaanisha nini ukisema hamjafika hali ya watu kukata tamaa? Unajua ni watanzania wangapi tumeshika huku Kenya wakijaribu kuingia Somalia??
Hali ngumu ya maisha ni moja wepo ya sababu tu.... E.g aliongoza mashambulizi ya garisaa alikua amesoma hadi 4th year University...
Hawa alashabaab waliouliwa na KDF kwa hii picha Kuna raia was Tz, uarabuni....UK, US, huyo ambae ameonyeshwa na hio arrow anaitwa Thomas Evans kutoka UK, alipolelewa hakukua na waislamu, inasemekana aliangalia video mtandaoni na kuvutiwa na propaganda za jihad, alipofika miaka 16 akasafiri Egypt kusoma kiarabu alipomaliza akapitia Sudan, Ethiopia alafu ndo akaingia Somalia alipopewa mafunzo...
The only reason hawajaanzisha jihad Tz ni kwasababu Tz haionekani kuwaonea waislamu... Hata sisi tulikua hivyo kabla tutume wanajeshi Somalia, miaka hio yote tulikua hatushambuliwi .... Kwahivyo wale waislamu wenye itikadi Kali huko Tz wanaona no heri wakasaidie ndugu zao huko Somalia..etc... Lakini jaribuni kufanya Jambo ambalo litaonekana kama mnalenga waislamu, jaribuni kutuma majeshi Somalia au kusaidia jeshi la Somalia na silaha za kivita au mafunzo ya kijeshi alafu uone vile hali itageuka....
Unafaa ujiulize kama dhahabu yenu inaweza kuibwa na msiishike huko kwenu (imajin kama hizo kilo 35 za dhahabu ingekua no kilo 35 za vilipuzi/grenade), tuje tuishike huku Kenya, kama mwizi wa benki anaweza kukimbia Tz na tumshike huku Kenya.... Kama dawa za kulevya kama cocaine,heroin..etc zinaingia Tz bila kushikwa, kama ndovu,kifaru wanauliwa na pembe zao kuuzwa nje ya nchi bila kushikwa..... Inakuaje unafikiri mko na uwezo wa kuzulia magaidi wakiamua kuwapiga vita vya jihad????? Ni watanzania wangapi hua wanafungwa baada ya polisi kufanya upelelezi wa aina ya juu ambapo muizi au muuaji alikua ni mtu amejipanga na kujificha kabisa Hadi ikabidi polisi wakabidi watumie mbinu za kisayansi ili kumshika mshukiwa Tena wanampeleka kotini na ushahidi unasababishwa wafungwe jela ..