Whydad amecheza mechi ya kiufundi licha ya ubovu wake na Simba kacheza mechi ya kukamia bila mipango ya kupata goli

Whydad amecheza mechi ya kiufundi licha ya ubovu wake na Simba kacheza mechi ya kukamia bila mipango ya kupata goli

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Simba hii kwa sasa naona wamebaki kukamia mechi dhidi ya waarabu na sio kuzicheza mechi hizi kiufundi, kilichoonekana Jana kinathibitisha ilo!

Kadri muda ulivyokuwa unaenda nilikuwa sioni Simba itapataje goli na kwa njia ipi, wakati wenzao waliokuwa wanayo presha kubwa ya kupata matokeo kutokana na kupoteza mechi zao 2 nyumbani na ugenini walionekana kucheza kimbinu zaidi na kwa mipango kwamba wapate goli lakini apo apo wasiruhusu goli!
Whydad kwa sasa Wana kazi kubwa sana ya kuurudisha ubora wao ambao kusema ukweli umepotea, na kitendo Cha kufungwa na jwaneng na Asec mimosas akikuwa Cha bahati mbaya vilikuwa ni vipigo halali kabisa kwa aina ya timu yao inavyocheza kwa sasa!

Na Simba Kama ingekuwa angalau inajitambua na kucheza kiufundi na kimbinu pia wasingekosa point ata moja dhidi ya whydad hii!

Lakini wao walichokifanya ni kukamia mechi tu basi mpira uje upigwe kurudishwa kwa adui!
Ni jinsi gani wangepata goli ni kitu ambacho kilikuwa akionekani kwao kocha anamtoa mchezaji mwenye energy uwanjani kibu Denis ya kuweza kuwafosi waarabu wafanye makosa kwenye eneo lao anamuingiza chama Mzee wa mwendo wa Kono Kono!

Licha ya udhaifu wa whydad but kavuna point 3 mbele ya Simba, ilikuwa ivyo ivyo pia kwa jwaneng licha ya udhaifu wao walivuna point 1 mbele ya Simba!

Na kitendo Cha whydad kupata point 3 dhidi ya Simba inaweza ikawa ndio starting point yao ya kurudisha morali yao iliyokuwa imepotea na Hali ya kujiamini ikarejea kwao kwa maana mechi inayofata aitakuwa nyepesi kwa Simba watabadilika pakubwa!

Ni kawaida kwa wachezaji wanapoona kocha mpya kaingia uwa wengi wanacheza kutafuta namba kwenye kikosi ata ambae ajiwezi lazima ajitutumue ndicho kilichoonekana kwenye mechi na whydad lakini ukiangalia energy yao na uwezo wao ni MBINGU na ARDHI ndio maana kadri muda ulivyokuwa unakwenda walikuwa wanakata pumzi na kukaribisha mashambulizi ya hatari golini kwao!

N:B MKIA UMEVUTWA RASMI NA NDIO IMEENDA IYOOO!!!!
 
WHYDAD? Oneni huyu mchambuzi ambaye hata kuandika jina la timu hawezi
 
Back
Top Bottom