Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Wanawake Wana mbinu nyingi sana za kukutesa. Akiwa na mimba tumelala vizuri kabisa bila changamoto yoyote Ile.
Nashituka kutoka usingizini nashangaa kuona mwenzangu analia bila sababu.
Nauliza unaumwa kimya!! Uchungu umefika? Na hapo mimba Bado sana muda wa kujifungua wife yupo kimya.
Nikaanza kupapasa huku,kule na humo lkn wapi....
Kama dk 9 Hivi ndo ananiambia nahitaji embe la kutafuta Mimi.
Wakuu hapa Sasa niliishiwa ujanja nikasema ama amepata kifafa Cha ujauzito huyu embe saa7 hii natoa wapi!?
Nikajua huenda ana test mitambo. Basi nikaanza kujieleza kuwa napata wapi Sasahivi mke wangu watu wamelala na hapa ni mjini maembe Hadi kule mashambani?
Jibu sipewi analia tu. Nikaendelea kusema ukizingatia kipindi hiki sio msimu wa maembe kabisa natoa wapi Hilo embe vumilia tulale kesho nitafanya juu chini tupate.
Wakuu Kila nikimaliza kuongea naambiwa anataka embe bichi la kutafuna!!.
Aisee akili ikanijia hapa niende tu huko mashambani iwapo nitakoswa nikalale Kwa jirani hapana kwakweli sitaweza kukesha naliliwa usiku kucha Mimi.
Nikawasha pikipiki muda huo ni mishale ya saa7:37 Hivi usiku. Nikaenda Hadi shamba Moja Hivi la mzee wa kanisa flani.
Muda huo nilikumbuka sana umhimu wa tochi wakuu. Smart yangu sawa ilikuwa inawaka ila mwanga umesambaa hata haufiki mbali.
Nilizunguka miti kama 4 hakuna kitu. Ujue ni usiku na kumetulia kabisa. Nikajisemea Sasa naenda mti wa mwisho nikikoswa naenda kulala Kwa jirani yangu kwakweli.
Nimeenda huku namuomba Mungu nipate asee. Bahati nzuri nikaona kaembe kadogo na kachanga ni aibu hata kukachukua ila nikajisemea acha tu niende Nako haka haka kama ushahidi kuwa nimekoswa embe mke wangu.
Kipindi najaribu kuwasha pikipiki Ili nirudi haiwaki fanya Hivi na vile wapi nikaanza kusukuma nilitumia kama lisaa kufika nyumbani ukijumuisha na muda wa kuzunguka kwenye miembe almost masaa2 yanafika!!
Nikawa nimefika kaembe nimekaweka kwenye mfuko wa suruali nikafunga na zipi kabisa kasidondoke.
Nafika nyumbani namkuta kanisubiria Nje mlangoni kulia halii amekaa tu. Nilikuwa na hasira sana lakini nilijikaza tu.
Nikamwambia aisee embe nimekoswa kabisa nimezunguka nikaona haka tu kachanga.
Kalikwapuliwa chap kama mwewe anapita na kifaranga na kakatafunwa Hadi kale ka mbegu ka embe vinakuwaga vyeupe.
Nilishangaa Sana. Hapo hapo tukaanza na story na vicheko ila moyoni ukinifunua nime mind vibaya mno.
Akauliza kwanini pikipiki umekuja unaisukuma mafuta yameisha. Nikamwambia hata sijui imegoma tu pindi naanza kurudi.
Kesho yake nikagundua kumbe nilizima kwenye Ile batani ya stop engine asee nilijidharau sana.
Nilikaa nae nikamwambia kama mimba Yako inakupelekesha Hivi. Ukija kuniambia Tena nitaenda mazima sitarudi nitalala nitakapo lala asee siwezi kwenda kwenye miembe inayo ogopeka vile halafu usiku wa manane je niking'atwa na nyoka utapata faida Gani?
Nikamwambia msimamo wangu ndo huu. Sitakaa nifate Tena Kwa sababu nilkuwa sijakumbia nimekuambia Sasa Jana umeniuzi mno.