Wife kanizidi kipato lakini kila wiki lazima aniombe elfu 20 ya kusukia

Taratibu Basi..hasira za Nini??!!
 
Huyu kyanyangwe hajui kuishi nao. Unampa 20,000 na jioni unaomba mkopo wa laki moja ili mkaende out maana amependeza sana. Mkifika huko mnatumia 20,000 unabakiza 80,000. Hapo nani mshindi? CC Espy
😀😀..waume wa sikuhizi🤔
Heshima kwa Baba zetu.
 
Kumhudumia vizuri familia yako Ni Pamoja na kuhakikisha Mkeo anapendeza kwa kwenda saloon kila wiki.
 
Bora ungemwambia kwa sasa sina mke wangu kipenzi subiri ntapambana ntakupa siku mbili hizi..
Hamna jambo linamkera mwanamke kama kumwambia "unakosaje" kiasi fulani kufanya kitu fulani? Inakera,inamfanya aone unakimbia wajibu wako /Pia inakufanya uonekane Hopeless

Maana mwanamke hupenda mtu anaempambania, kwahiyo kitendo cha wewe kuuliza unakosaje ef20 ni sawa na kumfanya ajisikie ule ni wajibu wake vile umemuona kama ni mwanaume mwenzie [emoji2] maana anajipambania kweri kwerii mpaka hela ya kusuka ajipe!
 
Yuko sahihi sana. Kwenye hiyo pesa yako toa elfu 20 akasuke tena hizo nywele za gharama ndogo. Angekuwa hana ajira bado ungetoa, kwa hiyo hapa hutoi kwa vile anakuzidi hela sio kwa vile huna hela kwa sasa. Ndio maana unautaja mshahara wake kama sababu ya kutompa.

Fedha zake mshirikiane kuendesha familia ili kuipatia familia yenu maendeleo.

wakati mwingine huwa mnajipa stress bure,mmeambiwa ishini na wake zenu kwa akili,Mimi mke wangu ananizidi kiwango cha mshahara lakini hajawahi nunua nguo kwa pesa yake ,ni lazima nimnunulie hii kwangu huwa naona kama heshima kwangu,hakuna kitu Mke wangu amewahi kukifanya kwa mwili wake bila kuniambia,na huwa naona fahari,kwangu Mimi mke wangu nikimkuta kanunua nguo za mwilini mwake bila kunilijulisha naweza lianzisha,haya ndo mapenzi

Kuna wakati wake zetu huwa wanataka watambue umhumi wa uwepo wetu ,sasa wee 20K povu limekutoka,?

Sasa kama ndivyo wewe wa kazi gani kwa mkeo ikiwa kila kitu anajitimizia si bora akuache akaishi peke yake maana hakuna umuhimu wa kuwa na mwenz.

Mimi hata nikimuoa mama Samia(vice president) kwa mshahara wangu wa laki nne lazima nimpe pesa ya kununulia nguo pia ya kwenda kusuka,na nikumkuta kaenda.kusuka bila ya kuniomba pesa lazima pachimbike.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Naomba kuuliza,vipi kuhusu mpango wa matumizi ya fedha yake,je,mnazichanga pamoja au cha kwangu ni changu na chake ni changu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…