Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena unaweza kuta naye ana discuss na huyo huyo h/girl na majirani pia. Maana anaonekana yuko aware na data walizo nazo majirani...amejuaje kama nae akai kwenye majungu na umbea?
Haya mambo ya uwifi haya. Mi nashukuru mume wangu kwao wote ni wanaume.
Biashara matangazo ati. Wewe toa terms mbona wateja tupo.
Nilikuta comment moja Michuzi Blog. Jamaa analalamika eti kuna kampuni iko PPF Tower inauza software za kutrack mazungumzo ya simu.
Mimi mwenzenu nikaona mbona hii ni good news. yeye kaona ni kikwazo...kumbe ameitangaza kiaina. Anasema serikali iifute. Mwe! Nikija huko lazima niitafute aisee.
Sasa wewe umeleta huu uzi ili iweje? Tumnange wifi yako au? Unataka ushauri wakati wewe pia ni third third party?
Ngoja nikwambie kitu...huyo wifi yako ni wa kumsaidia kimawazo na si kumtundika na kumcheka.
Wanawake wengi wako so insecure na inapofikia situation kama hiyo si wote wana busara za yupi wa ku share nao yaliyopo moyoni. Wewe una mume?
Ni kweli kuwa haipaswi kumuonyesha house girl kuwa huna imani na mumeo...ila fact kuwa yuko mbali ameona atapata clue kupitia kwa h/girl which is wrong. Lakini jua yuko confused na anataka comfort si kuchekwa.
Ukizingatia Tanzania private investigators hawapatikani...unakuta anaamua kutumia any means at her disposal kukusanya data za mumewe.
Muite umwambie kama unampenda wifi yako...mwambie huyu H/girl si wa kumpa siri zako...hata mimi najuua mnayoongea., hata majirani wanajua. Tafuta mwingine wa ku m-confide si h/girl...maana it seems like she needs someone to talk to.
Kwanza nina wasiwasi na nyie mnamteta wifi yenu kwa h/girl...ni mule mule tu.
Wote mna feed data zisizomuhusu kila mtu kwa muda wake.
Yaani hata hili nalo umekuja kuuliza humu??
Wewe unashindwa kumwambia wifi yako kuhusu umbea wa bek3?..are you serious??
Hawa mabeki3 mbona mnawapa sana nguvu??
Hamna kitu kibaya kama hiki aisee! Usithubutu kuingilia hgeli wa mtu unless ni madhara kwa watoto wao. Kila mtu anamjua maid wake yukoje, na ana udhaifu gani na kuna anachompendea. Anaweza kuwa mdaku ila anaangalia watoto vizuri na ni msafi. Ukimsema hapo tayari ugomvi na wifi.