Course Coordinator1
JF-Expert Member
- Mar 20, 2025
- 857
- 2,341
Ni vigumu sana kuua maelfu ya watu pasipo na sababu, hususan kwenye zama hizi, halafu utegemee dunia ikae kimya.
Sasa hivi dunia imeingiliana sana. Litokealo sehemu moja basi jua kuwa litawagusa tu na wengine waliopo sehemu zingine.
Ukweli ni kwamba Tanzania kwa sasa haina vyombo vya habari.
Vilivyopo ni vyombo vya uchawa tu.
Taarifa nyingi kuhusu mauaji ya Watanzania yaliyofanywa na askari wa Samuya, kwa sasa zinapatikana kutoka vyombo vya habari vya nje.
Ambavyo vilipaswa kuwa ndo vyombo vyetu vya habari, vimeufyata na kuamua kuweka mikia yake katikati ya miguu ya nyuma na kuzikimbia kabisa habari za mauaji ya Samuya.
Jana shirika la habari la DW kutoka nchini Ujerumani kupitia chaneli yake yake ya YouTube, lilirusha makala kuhusu idadi ya watu waliouliwa na Samuya.
View: https://youtu.be/FMquYIzOK6E?si=rjEHMeSHyVigsGC2
Hata wao wanashangaa vile ambavyo utawala haramu wa Samuya unavyopingana na ukweli kuhusu hayo mauaji, licha ya kuwepo ushahidi mwingi sana.
Ni ajabu sana kwani hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM aliyezungumzia mauaji hayo.
Ukimya wao huo ndo kukiri kwao kuwa wanahusika moja kwa moja 💯% na mauaji hayo.
Vile vile. Siku hizi watu hawategemei tena kupata habari toka kwa vyombo vya habari vilivyozoeleka.
Siku hizi kuna waandishi habari raia [citizen journalists] ambao mara nyingi sana wanakuwa huru katika kufanya hizo shughuli zao.
Mojawapo ya vyombo binafsi vilivyopo huko YouTube ni chaneli ya African Diaspora News Channel.
Hawa wameendelea kuripoti habari za uchaguzi bila uoga.
Mfano, jana wamezungumzia uchafuzi wa Samuya na vile alivyojitangaza mshindi huku maelfu ya watu wakiuwawa.
View: https://www.youtube.com/live/DtY6XzXJyvg?si=8RUiI-P871pVNMY5
Pia, wakarusha habari ya kukamatwa kwa Niffer na kosa lake ambalo adhabu yake ni kifo.
Kusema ukweli wanashangaa tu jinsi Tanzania ilivyo nyuma, kwamba kucheza challenges za TikTok kunaweza kupelekea mtu kunyongwa!
View: https://www.youtube.com/live/nF0_MWXq9Wc?si=m8YR-AYid5txGeBZ
Kama walivyosema, this is pure madness.
Kama hao wauaji wanadhani kuwa kwa kukaa kimya kutalifanya jambo lote lipotee, basi watakuwa wamepiga mahesabu yao vibaya.
Damu ya maelfu ya watu wasio na hatia yoyote ile haiwezi kufagiliwa chini ya busati na wakasahaulika.
Samuya na wenzake wataenda wapi ambako hawataulizwa maswali kuhusu hayo mauaji?
Acha waendelee kujidanganya.
Mfano ni kule Mwanza Kisesa watoto 8 wa shule ya msingi na sekondari waliuliwa wakiwa Saluni baada ya kukimbia maandamano, Polisi wakawafuwata na kuwambia watoke nje watoto wa watu wakajuwa polisi wanawasaidia kwenda nyumbani Salama, wakawambia waangalie nyuma wakawapiga risasi.
Kesi za uhaini pale Mwanza kuna watoto wa kidato cha pili walikamatwa wakiwa na Uniform tarehe 30 nao wakaunganishwa kuwa wanaandamana kwa hiyo wana kesi ya uhaini, wakati wenzao wanafanya mitihani watoto wapo jela.