Wiki ya 31 ya ujauzito mtoto bado hajageuka .

Ms mol

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2017
Posts
1,960
Reaction score
2,345
Habari zenu madaktari

Nilipàta maumivu kiasi ya tumbo chini ya kitovu nikaenda hospital binafsi hapa mjini mbeya.
Nilifanyiwa kipimo cha ultrasound kikaonyesha kuwa kila kitu kipo vizuri ila mtoto bado hajageuka,ujauzito ni wiki ya 31 sasa, EDD ni 1/1/2019 wakuu hapa MNA maoni! Ushauri gani?
Nikipata mitazamo tofauti tofauti nitashukuru sana kwakweli.
 
Kama EDD ni 1/1/2019 bado mda upo sana mkuu hadi siku 4 kabla mtoto anaweza akageuka.
 
Nenda kwa wamama wa kimasai watakusaidia kumgeuza kwa njia za asili bila madhara.
 
Usiwe na hofu mleta mada, wewe cha endelea na taratibu za kawaida kama mjamzito, kugeuka mtoto sio hoja sana.
Na sikushauri kwenda kwa watu eti wamgeuze saizi.
Kumbuka tu kuwa ile wiki ya mwisho kuingia EDD ujipange vizuri, na uwahi kabla uchungu haujaanza ili upime tena kama kageuka au vipi.
Hata uchungu ukianza na bado hajageuka hilo litajulikana tu na hatua zitachukuliwa kuhakikisha unapata mtoto as long as hali mendeleo yake ni mazuri.
Ni kawaida sana hiyo hali kutokea
 
cheza na vitu vingine sio mimba

Naongelea hali niliyopitia, nilianza kupata maumivu makali nikiwa na ujauzito wa miezi 5, wakati huo nilikua nafanya kazi karatu, baada ya vipimo hospital niliambiwa mtoto kakaa vibaya, natakiwa kupumzika na nisifanye kazi Ngumu. Na Kama hali ikiendelea hivyo nitatolewa mtoto kabla ya muda. Baada ya kupewa ruhusa kazini nilirudi nyumbani mwanza, nilikwenda bugando hospital clinic majibu na ushauri ukawa huohuo.
Mfanyakazi mwenzangu alikuja kunisalimia baada ya mwezi na nusu kupita, hali alionikuta nayo Mungu ndo anaejua, nilikua na maumivu makali sana lakini pia sikutaka kumpoteza mtoto wangu. Baada ya kumuelezea tatizo,
Yeye ndie Aliyeniunganisha na mama wakimasai wa karatu, na huyu wa karatu akaniunganisha na wa mwanza, Alikua anakuja kunifanyia masaji ya tumbo asubuhi na jioni, alikua anatumia Mafuta ya ng'ombe sina hakika Kama yalichanganywa na dawa, baada ya wiki sikuhisi tena maumivu.
Ilipofika tarehe yangu ya clinic mimba ikiwa na miezi 8 niliambiwa mtoto kageuka na yuko sawa.
Na muda ulipofika nilijifungua salama,
Mwanangu sasa ana miaka 4.
Tusidharau Tiba zetu za asili.
Kwa sasa sina mawasiliano na huyo mama, nilipoteza namba zake ila nina imani kwa Kabila la wamasai wengi wana ujuzi huo. Watafute watakusaidia.
 
sawa mkuu, nashukuru sana, niliingiwa na waswas kidogo! Je nizidishe mazoezi?? Labdabyatasaidia
 
Pole na hongera sana mkuu!
 
Nashu
Kama EDD ni 1/1/2019 bado mda upo sana mkuu hadi siku 4 kabla mtoto anaweza akageuka.
Nashukuru kwa kunitoa hofu mkuu!

Je nikizidisha mazoezi ya kutembeatembea naweza kusaidika? Walau kumfanya mtoto awe active na ageuke?
 
ukitaka ulete ujuaji kwenye mambo ya Mungu ...utasumbuka sana. habari za kugeuka mtoto achana nazo, endelea kusubiri wakati ukifika utafurahi. Hii ya kupangia mtoto kugeuka si njema sana
 
Asante dada,
Mara nyingi ni kuwa kama mama hayuko active mtoto nae anakuwa mvivu tumboni. Kule kijijini wanawake wajawazito bado wanatafuta kuni , wanachota maji and everything else.

Mjini unashauriwa utembee hata nusu saa asubuhi na jioni au gym.
Sasa mama ameshachelewa au anaweza kuwa active na mtoto akageuka?
 
Nashu
Nashukuru kwa kunitoa hofu mkuu!

Je nikizidisha mazoezi ya kutembeatembea naweza kusaidika? Walau kumfanya mtoto awe active na ageuke?
Usifanye mazoezi mazito wakati wa ujauzito ila mazoezi ya kutembea ni muhimu sana kama alivyokushauri Dr wetu Sky Eclat
 
😀😀😀😀😀😀😀😀 Tumekupa Heshima ya UDokta humu JF kwa kutupa elimu mbali mbali kuhusu afya.
sawa mkuu, tayari nimeshachanganyikiwa! Nina hofu sana! Naendelea na taratibu za kawaida na Dr aliniambia baada ya mwezi mmoja niende tena! Hapo tutaona km mtoto ameshageuka au bado!
 
Wale wakunga wa jadi sijui kama wapo sikiliza. Ushauri wao. Ulitakiwa uwe na midwife atakaekuzalisha sasa hivi mnapanga birth plans.
 
Back
Top Bottom