ISLETS
JF-Expert Member
- Dec 29, 2012
- 8,120
- 5,352
Naongelea hali niliyopitia, nilianza kupata maumivu makali nikiwa na ujauzito wa miezi 5, wakati huo nilikua nafanya kazi karatu, baada ya vipimo hospital niliambiwa mtoto kakaa vibaya, natakiwa kupumzika na nisifanye kazi Ngumu. Na Kama hali ikiendelea hivyo nitatolewa mtoto kabla ya muda. Baada ya kupewa ruhusa kazini nilirudi nyumbani mwanza, nilikwenda bugando hospital clinic majibu na ushauri ukawa huohuo.
Mfanyakazi mwenzangu alikuja kunisalimia baada ya mwezi na nusu kupita, hali alionikuta nayo Mungu ndo anaejua, nilikua na maumivu makali sana lakini pia sikutaka kumpoteza mtoto wangu. Baada ya kumuelezea tatizo,
Yeye ndie Aliyeniunganisha na mama wakimasai wa karatu, na huyu wa karatu akaniunganisha na wa mwanza, Alikua anakuja kunifanyia masaji ya tumbo asubuhi na jioni, alikua anatumia Mafuta ya ng'ombe sina hakika Kama yalichanganywa na dawa, baada ya wiki sikuhisi tena maumivu.
Ilipofika tarehe yangu ya clinic mimba ikiwa na miezi 8 niliambiwa mtoto kageuka na yuko sawa.
Na muda ulipofika nilijifungua salama,
Mwanangu sasa ana miaka 4.
Tusidharau Tiba zetu za asili.
Kwa sasa sina mawasiliano na huyo mama, nilipoteza namba zake ila nina imani kwa Kabila la wamasai wengi wana ujuzi huo. Watafute watakusaidia.
Mkuu shukuru tu Mungu mambo yalienda vizuri, si kwamba ni jambo geni mtoto kugeuzwa tumboni, hapana, hapa mahospitali kuna wakatu huwa inalazimu kabisa mtoto ageuzwe linafanyika tena ndani ya muda mfupi tu, ila ni baada ya daktari kujiridhisha kuwa ugeuzwaji unawezekana bila kuleta madhara.
Mkuu narudia kwa faida ya wengi, mimba sio kitu cha kuchezea, tuna wataalamu mahospitali tuwatumie hao. Ninaandika haya nikiwa na experience kabisa, wapo kina mama wengi wamepoteza maisha au watoto kwa kuamini hayo mambo ya kiasili. Mtu analazimisha kugeuza mtoto kumbe kondo limezunguka shingo ya mtoto kinachofuata hapo anashangaa mtoto hachezi tena na ndio mtu anakimbilia hospitali baada ya kuona hali imekuwa mbaya.