Wiki ya 31 ya ujauzito mtoto bado hajageuka .

Naongelea hali niliyopitia, nilianza kupata maumivu makali nikiwa na ujauzito wa miezi 5, wakati huo nilikua nafanya kazi karatu, baada ya vipimo hospital niliambiwa mtoto kakaa vibaya, natakiwa kupumzika na nisifanye kazi Ngumu. Na Kama hali ikiendelea hivyo nitatolewa mtoto kabla ya muda. Baada ya kupewa ruhusa kazini nilirudi nyumbani mwanza, nilikwenda bugando hospital clinic majibu na ushauri ukawa huohuo.
Mfanyakazi mwenzangu alikuja kunisalimia baada ya mwezi na nusu kupita, hali alionikuta nayo Mungu ndo anaejua, nilikua na maumivu makali sana lakini pia sikutaka kumpoteza mtoto wangu. Baada ya kumuelezea tatizo,
Yeye ndie Aliyeniunganisha na mama wakimasai wa karatu, na huyu wa karatu akaniunganisha na wa mwanza, Alikua anakuja kunifanyia masaji ya tumbo asubuhi na jioni, alikua anatumia Mafuta ya ng'ombe sina hakika Kama yalichanganywa na dawa, baada ya wiki sikuhisi tena maumivu.
Ilipofika tarehe yangu ya clinic mimba ikiwa na miezi 8 niliambiwa mtoto kageuka na yuko sawa.
Na muda ulipofika nilijifungua salama,
Mwanangu sasa ana miaka 4.
Tusidharau Tiba zetu za asili.
Kwa sasa sina mawasiliano na huyo mama, nilipoteza namba zake ila nina imani kwa Kabila la wamasai wengi wana ujuzi huo. Watafute watakusaidia.

Mkuu shukuru tu Mungu mambo yalienda vizuri, si kwamba ni jambo geni mtoto kugeuzwa tumboni, hapana, hapa mahospitali kuna wakatu huwa inalazimu kabisa mtoto ageuzwe linafanyika tena ndani ya muda mfupi tu, ila ni baada ya daktari kujiridhisha kuwa ugeuzwaji unawezekana bila kuleta madhara.
Mkuu narudia kwa faida ya wengi, mimba sio kitu cha kuchezea, tuna wataalamu mahospitali tuwatumie hao. Ninaandika haya nikiwa na experience kabisa, wapo kina mama wengi wamepoteza maisha au watoto kwa kuamini hayo mambo ya kiasili. Mtu analazimisha kugeuza mtoto kumbe kondo limezunguka shingo ya mtoto kinachofuata hapo anashangaa mtoto hachezi tena na ndio mtu anakimbilia hospitali baada ya kuona hali imekuwa mbaya.
 
sawa mkuu, nashukuru sana, niliingiwa na waswas kidogo! Je nizidishe mazoezi?? Labdabyatasaidia
Mama kijacho hii ni mimba yako ya kwanza sio 😀😀
Kawaida mazoezi yanakusa mengi mimba inapokuwa changa na unapunguza kadri mimba inavyokuwa kubwa.
Hivyo basi kwa sasa fanya mazoezi ya kawaida sana mfano kazi za kawaida za nyumbani na kutembea tembea, ula sio kazi nzito nzito mfano kubebelea mandoo ya maji nk.
 
H
Wale wakunga wa jadi sijui kama wapo sikiliza. Ushauri wao. Ulitakiwa uwe na midwife atakaekuzalisha sasa hivi mnapanga birth plans.
Hivi huyu mtoto atazaliwa kwa njia ya asili kweli? Au ndo operation itahusika?

Wakunga wa jadi siku hizi wamepotea sana!
 
Mama kijacho hii ni mimba yako ya kwanza sio 😀😀
Kawaida mazoezi yanakusa mengi mimba inapokuwa changa na unapunguza kadri mimba inavyokuwa kubwa.
Hivyo basi kwa sasa fanya mazoezi ya kawaida sana mfano kazi za kawaida za nyumbani na kutembea tembea, ula sio kazi nzito nzito mfano kubebelea mandoo ya maji nk.
Mkuu islets mwanzoni niliambiwa kupumzika zaidi maana sukari na presha vilikuwa chini na ilisababishwa na kutapika sana.
Muda wote nafanya shuhuli ndogondogo za nyumbani, ila nilipopata maumivu makali ndio nikaenda hospital nikafanya ultrasound Dr kwa mshangao mkubwa sana, aliniambia kuwa mtoto hajageuka.

Hofu yangu ni je? Nilipofikia hapa mtoto atafanikiwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida au ndio basi operation inahusika!?
 
Hizi tabu ziko mijini tu huko maporini tunalima mpaka siku ya kujifungua na ukimaliza unajipikia supu au uji fresh hamna ultra sound wala madikodiko

Badilisheni mtindo wa kula, mazoezi ni muhimu pia punguzeni madeko deko

Pole
 
Mkuu wakati mwingine shida ikija inakuja tu, huyu ni mtoto wa 3 ndio ameleta hili tatizo wengine fresh tu jamani!
 
Wanakuandaa kisaikolojia ili wakuambie utajifungua kwa mkasi na watakupa siku ya kufanyiwa operation.
Ukiwa mjamzito usipende sana hospital za private, kwani wakati mwingine huforce ufanyiwe operation ili wapate fedha.
Private hospital za kibongo usicheze nazo, kuwa making unaweza kuandikiwa dawa ya ugonjwa hata usiokuwa nao maadam tu wakiona hazitakudhuru
 
Nashukuru mkuu, japo sidhani km anaweza kumifanyia hivyo.. Nasema hapana!
 
Mkuu islets mwanzoni niliambiwa kupumzika zaidi maana sukari na presha vilikuwa chini na ilisababishwa na kutapika sana.
Muda wote nafanya shuhuli ndogondogo za nyumbani, ila nilipopata maumivu makali ndio nikaenda hospital nikafanya ultrasound Dr kwa mshangao mkubwa sana, aliniambia kuwa mtoto hajageuka.

Hofu yangu ni je? Nilipofikia hapa mtoto atafanikiwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida au ndio basi operation inahusika!?
oooo kumbe ulikuwa hivyo. Pole, bado uwezekano muda wa mtoto kugeuka upo sana na ukajifungua kawaida na hata kwa bahati mbaya hajageuka bado kuna options nyingi za kufanya kulingana na alivyokaa, mfano kugeuzwa kwa mikono, au kujifungua kawaida hivyovyo kama itaonekana ataweza kupita, au operation kama itaonekana hakuna namna nyingine.
Cha msingi ni kupata muda wa kupima tena ultrasound muda mchache kabla ya EDD.
Na kama hizo hali za sukari zimekaa sawa, anza tu mazoezi mkuu taratibu
 
Asante mkuu! Dr alishauri nirudi kwa ajili ya vipimo vya ultra sound baada ya wiki 4 hivi, nadhani Kwa uwezo wa Mungu km watoto huwa wanageuka hata km wamekuwa wakubwa itatokea tu ageuke, azaliwe salama!
 
Ni ombi langu pia iwe hivyo. Kila la kheri
 
Fuata ushauri waliokupa hospital. Kikubwa hapo ni mazoezi hasa ya kutembea daily, then pata muda wa kupumzika. Usihofu, utajifungua salama!
 
Mkuu shukuru tu Mungu mambo yalienda vizuri, si kwamba ni jambo geni mtoto kugeuzwa tumboni, hapana, hapa mahospitali kuna wakatu huwa inalazimu kabisa mtoto ageuzwe linafanyika tena ndani ya muda mfupi tu, ila ni baada ya daktari kujiridhisha kuwa ugeuzwaji unawezekana bila kuleta madhara.
Mkuu narudia kwa faida ya wengi, mimba sio kitu cha kuchezea, tuna wataalamu mahospitali tuwatumie hao. Ninaandika haya nikiwa na experience kabisa, wapo kina mama wengi wamepoteza maisha au watoto kwa kuamini hayo mambo ya kiasili. Mtu analazimisha kugeuza mtoto kumbe kondo limezunguka shingo ya mtoto kinachofuata hapo anashangaa mtoto hachezi tena na ndio mtu anakimbilia hospitali baada ya kuona hali imekuwa mbaya.

Soma andiko langu vizuri utaelewa, tatizo la mtoto kukaa vibaya na kujifunga shingoni ni vitu viwili tofauti.
Sikulazimishi uamini nilichoandika.
Pia usinilazimishe niamini kua hakuna njia mbadala za asili hasa kwa matatizo ya uzazi . Kwani huko hospitali tunapona kwa uwezo madaktari bila kudra za Mungu?
Mungu ni wetu sote, kikubwa ni kufanya jitihada.
 
Back
Top Bottom