Uchaguzi 2020 Wiki ya kuamua mitano tena ya kuendelea na matatizo yetu au mitano kwanza ya matumaini mapya

Uchaguzi 2020 Wiki ya kuamua mitano tena ya kuendelea na matatizo yetu au mitano kwanza ya matumaini mapya

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Wiki hii ni muhimu sana kwako.

Ni wiki ya wananchi kuamua kuendelea kuhangaika na matibabu kwa kukosa pesa au kupata bima ya afya kwa wote.

Ni wiki ya Mwanafunzi kuamua kuendelea kulipa riba ya 15% au 3%.

Ni wiki ya Wajasiliamali kuamua kuendelea kilipia vitambulisho elfu 20 au mfanye biashara zenu bure.

Ni wiki ya Wakulima wa pamba na korosho kuamua kuendelea kukopwa mazao yao au kulipwa keshi.

Ni wiki ya kuamua tuendelee kununua ndege 11 zilizobaki kwa keshi au pesa hizo zinunue madawa na vifaa vya matibabu.

Ewe mfanyakazi wa umma hii ni wiki yako ya kuamua uendelee na mshahara wako bila nyongeza kwa miaka mingine mitano.

Ewe mama hii wiki ni muhimu sana kwako ya kuamua kuendelea kununua ndoo ya maji kwa elfu 1 kwa miaka mitano mingine.

Hii wiki ni ya wafanyabiashara kuamua kuendelea na hasara zinazosababishwa na kodi nyingi za TRA au muanzishe mfumo mpya wa kodi.

Ni wiki ya Wastaafu watarajiwa kuamua kuendelea na kikokotoo kipya au cha zamani, kumbuka cha zamani mwisho wake ni 2022.

Ni wiki ya vyombo vya habari na waandishi kuendelea kupangiwa cha kuripoti au kuwa huru kutumia taaluma yenu.

Ni wiki ya wananchi wote kuendelea na utawala unaonyanyasa, unaoteka watu, unaobambikia watu kesi au kuachana nao.

Uchaguzi ni Wetu.
 
Kura tutampigia Lisu kwa wingi lakini hatotangazwa mshindi. Wapenda mabadiliko plan B yetu ni ipi?
Plan B ni kutoka barabarani nchi nzima pale tutakapotakiwa kufanya hivyo. Hakuna kinachoweza kuzuia nguvu ya umma.

Itakuwa haina maana yoyote ikiwa tumechagua Rais wetu alafu tukubali kirahisi tu kwamba hakutangazwa mshindi ikiwa ameshinda.
 
CCM wanapima kimo cha maji kama hilo litatokea kweli. Wamealianza kwa kuondoa wagombea wa upinzani, hakuna lililotokea. Wakawafungia wapinzani wa kweli kufanya kampeni, hakuna lililotokea. Leo kiongozi mkuu kule Zanzibar ametekwa na kupelekwa sehemu isiyojulikana, hakuna kitu mpaka sasa. Hao wananchi watakwenda barabarani lini?
Plan B ni kutoka barabarani nchi nzima pale tutakapotakiwa kufanya hivyo. Hakuna kinachoweza kuzuia nguvu ya umma.
Itakuwa haina maana yoyote ikiwa tumechagua Rais wetu alafu tukubali kirahisi tu kwamba hakutangazwa mshindi ikiwa ameshinda.
 
We shall vote for His Excellency President Magufuli. Hope he win the election for more than 98%
 
Sisi Watanzania tuliowengi tutamchagua Rais Magufuli kipenzi

Rais Magufuli ameonyesha uzalendo wa hali ya juu, hakuna wa kumfikia
Mtanzania mimi na wengine tulio wengi tutaamua kulingana na vigezo alivyoainisha mleta mada

Hatutochagua kwa mapenzi ya uzalendo wa kutofikiwa labda utupe vigezo kwa uzalendo upi ambao haku wa kumfikia kivipi

# NI YEYE TU 2020
# THE BULLET PROOVE
# THE IRON PRESIDENT
# THE REAL KINJEKETILE BULLET CONDENCER
 
Bila wasi wasi mitano tena

Magufuli 5 tena 1st 💯

Hapa kijijini napoishi.. tumekuweka mahema.. ng'ombe na mbuzi wakuchinja.. vinywaji vinafika leo.. yaani tunajipa furaha Jumatano.. hakuna kulima.. na usafiri wa luxury mabasi.. upendo kijijini hapa... tutakula pati haswa, furaha sana.. chinja tule nyama.. MITANO TENA sisi tulimsikia Magufuli akisema....... na asile.. kijijini kama town moja kule nje ya downtauni kubwa.
Umeme wa REA na maji bombani muda wote.. eeeh

Karibuni mjumuike nasi.. 💚💛💚💛💚
Magufuli oyeeeeeeee
 
Kutandikwa risasi sio kwa Lissu
Kama kutandikiwa risasi hata Majambazi yanatabdikwa risasi

Watanzania hawawezi kupigia kura msaliti wa Nchi, kura tutapigia Mzalendo Magufuli Rais
Kwasababu ni
Mzalendo,
mpole,
Mchapakazi
Mvumilivu
,Mnyenyekevu
Mpenda watu
Jasiri
Nk

Kura zote kwa Rais Magufuli
Mtanzania mimi na wengine tulio wengi tutaamua kulingana na vigezo alivyoainisha mleta mada

Hatutochagua kwa mapenzi ya uzalendo wa kutofikiwa labda utupe vigezo kwa uzalendo upi ambao haku wa kumfikia kivipi

# NI YEYE TU 2020
# THE BULLET PROOVE
# THE IRON PRESIDENT
# THE REAL KINJEKETILE BULLET CONDENCER
 
Nemepeleka kitambaa cha suti ya kusherehekea ushindi wa JPM kwa fundi, mpaka sasa ajamaliza kushona suti yangu. na ishapita wiki sasa. Huyu fundi atakuwa sio Chadema kweli?
 
Bila wasi wasi mitano tena

Magufuli 5 tena 1st 💯

Hapa kijijini napoishi.. tumekuweka mahema.. ng'ombe na mbuzi wakuchinja.. vinywaji vinafika leo.. yaani tunajipa furaha Jumatano.. hakuna kulima.. na usafiri wa luxury mabasi.. upendo kijijini hapa... tutakula pati haswa... furaha sana.. chinja tule nyama.. MITANO TENA sisi tulimsikia Magufuli akisema....... na asile.. kijijini kama town moja kule nje ya downtauni kubwa..
Umeme wa REA na maji bombani muda wote.. eeeh

Karibuni mjumuike nasi.. 💚💛💚💛💚
Magufuli oyeeeeeeee
Endelea kuota.
 
Back
Top Bottom