WikiLeaks: Tanzania official fears for his life!

WikiLeaks: Tanzania official fears for his life!

Kwa asilimia kubwa inaonekana Hosea aliyasema kweli, kukanusha kwake kunaweza kuwa kunatokana na mojawapo kati ya yafuatayo:

1.Anahofia kitumbua chake
2.Alimsingizia Rais

Na 1 hapo juu inatokana na kushindwa kwake kazi aliyokabidhiwa,kama kweli Rais alimwambia,yeye angelikuwa ni mzalendo halisi wala asingesubiri kulalamika kwa balozi wa Marekani. Angeitisha vyombo vya habari akawaeleza wtz na akajiuzulu. Ingekuwa ni heshima sana kwake na nchi hii ingemkumbuka daima.

Na 2 yawzekana alimsingizia Rais kwa balozi ili kujastify kushindwa kwake kazi. Kama alimsingizia Rais lazima sasa akane kwa sababu ingembidi atoe ushahid wa kuthibitisha kwamba kweli Rais alimwambia hivyo.
Mimi sina imani na Hosea tangia ile sakata ya Richmond
 
Hosea akumbuke kilichompata General Patreous,aliyekuwa Commander wa majeshi ya Marekani kule Afganistan. Alipoteza kazi baada ya wikileaks kutoa taarifa za yeye kuhojiwa na gazeti moja na kumkashifu Obama na Joe Baiden.

Pamoja na kuwa Dr Hosea ni msomi, si ajabu lugha ya kiingereza bado inampiga chenga, na labda alimaanisha kitu hiki kumbe Balozi huyo wa US akaelewa tofauti. Hosea, ushauri wa bure tu, huwezi kumsema Commander in Chief hivyo, hutaweza tena kufanya naye kazi, kama huna imani naye achia ngazi.

Simply fuata mfano wa General Patreous, na jamii itakuheshimu. But uwe makini usije kukutwa na yaliyomkuta Marehemu Kombe, wakakushindilia risasi hadi ufe wakikudhania kuwa wewe ni jambazi sugu, loh Tanzania haina shukurani.
 
wee umetumwa eehh?? amuwajibishe kwa kusema ukweli?? ndo tabia zenu ccm huwa hampendi mtu aseme ukweli..eti amuwajibishe nani asiyejua kuwa jk ndo kikwazo cha kesi kubwa kubwa hapa bongo na sababu ikiwa ni ushkaji na watuhumiwa?? wee k naona hapa hapakufai, peleka pumba zako kale na mkeo na nduguzo home sio ku2letea u2mbo hapa..
nadhani mzee ukinielewa, hapo tunachotaka ni rais achukue hatua, kama atakanusha (siyo kikwazo) then amuwajibishe Hosea, na kama akikaa kimya basi ni kweli yeye ni kikwazo, na hatumtaki atuongoze. umenipata hapo, mkuu?
 
mzee we ndo umepotea kimtazamo.Hosea amejitahidi kuonesha rais ni mchafu anazuia haki isitendeke halafu wewe unataka ang'oke tena!!?daah!ama kweli ukombozi bado uko mbali.jk anawapa mafisadi nguvu kubwa sana kiasi kwamba ikulu imekua kama sebleni kwao na hili jambo ndio linafanya kazi ya takukuru kua ngumu (ingawa takukuru yenyewe sio pure asilimia 100)
Mzee naona wewe hukunielewa....., what we want is JK kujitetea kwamba yeye si Kikwazo, kwa kufanya yafuatayo
1) Kumwajibisha Hosea, na kutoa ushahidi bayana kwamba yeye ni safi
2) kukubali uchafu/ ukikwazo wake na kuachia ngazi...
 
Hosea anatapatapa tu hana lolote yaliyosemwa na wikileaks ni kweli tupu hata mazingira ya PCCB kushughulikia mafisadi papa yanadhihirisha ukweli huu. Bado tunasubiri kutoka wikileaks kuhusu mikataba ya madini, mafuta na gas nao wataanza kutafutana kama Hosea.

Wikileaks juu juuuuuuuuuuu zaidiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
"sometime the only solution is execution for some" huyu mtu hata haoni aibu kukanusha na kujidanganyanganya? ningekuwa kikwete ningemsimamisha kazi mpaka atoe maelezo kamili. ile ni kashfa kubwa sana kwa kiongozi wa nchi, kusema Rais anazuia upelezi.... hata kwenye hayo maelezo bado hajakanusha hilo,
sasa utajuaje ushahidi ni dhahifu kama ujauchunguza vya kutosha...... nitamshangaa sana kikwete asipomdiscipline huyu mtu.

Mkuu usingekuwa na ubavu huo maana alichosema jamaa ndicho chenyewe..................au umesahau ule msemo wa JK waacheni wazee wapumzike kwa amani?
 
Wikileaks noma!

Na bado watashikana uchawi kwa sana tu!!!
 
Wikileaks wamechelewa sana kuyatoa haya,

Fikiria kama habari hizi zingetolewa miezi miwili kabla ya uchaguzi joto lake lingekuwaje? na watu wangapi wangebadilishwa misimamo yao juu ya JK na CCM yake? Maana wengi walikuwa wanaona ayasemayo Slaa na chama chake ni uzushi na wivu tuu. Jee balozi wa Marekani ana wivu na JK na serikali yake?

Jibu ni hapana, Ukweli ulikuwa unawekwa hadharani
 
"sometime the only solution is execution for some" huyu mtu hata haoni aibu kukanusha na kujidanganyanganya? ningekuwa kikwete ningemsimamisha kazi mpaka atoe maelezo kamili. ile ni kashfa kubwa sana kwa kiongozi wa nchi, kusema Rais anazuia upelezi.... hata kwenye hayo maelezo bado hajakanusha hilo,
sasa utajuaje ushahidi ni dhahifu kama ujauchunguza vya kutosha...... nitamshangaa sana kikwete asipomdiscipline huyu mtu.
Kikwete hana ubavu huo.... kama angekua nao basi angeshamsimamisha zamani sana kwa kuvuruga ccm primaries ambazo zilitawaliwa na rushwa iliyokithiri
 
Ninachokijua ni kimoja tu, kwamba TZ haina Raisi since 2005 bali ni genge la mafisadi ndilo lipo ikulu likiongoza nchi
 
Wikileaks wamechelewa sana kuyatoa haya, fikiria kama habari hizi zingetolewa miezi miwili kabla ya uchaguzi joto lake lingekuwaje? na watu wangapi wangebadilishwa misimamo yao juu ya JK na CCM yake? Maana wengi walikuwa wanaona ayasemayo Slaa na chama chake ni uzushi na wivu tuu. Jee balozi wa Marekani ana wivu na JK na serikali yake? jibu ni hapana, Ukweli ulikuwa unawekwa hadharani
chakaza

wikileaks care less whether we have election or erection, all they did is expose global denial of information in the name of intelligence, which in facts its just ass covering for leaders

to me i think this has come at the best time so that we can confirm competency ya mkuu wa nchi.... kama kweli anayo!!!

Kwangu mimi hili ni swali la section A na jibu ni yes or no... the ball is in Mr. President's court
 
Hoseah is just trying to cover his ass. Angekiri alichosema kuwa Kikwete ni Kikwazo kwenye vita dhidi ya ufisadi na amezuia kesi ya Kiwira dhidi ya Mkapa na ya Richmond dhidi ya Lowassa anajua kuwa angefukuzwa kazi mara moja. Ukweli unabaki pale pale, Kikwete hana dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi kwa kuwa hata yeye aliwekwa madarakani na sehemu ya pesa za Kagoda zilizoibiwa BoT.

Pia anaogopa akiruhusu Mkapa achunguzwe atakuwa ameweka precedent, hivyo Rais ajaye naye ataruhusu Kikwete achunguzwe kwa ufisadi.

The bottom line is that kesi zote kubwa za kifisadi ambazo zinahusu vigogo na wafanyabiashara wakubwa walio karibu na Kikwete na Mkapa, eg rada, Kiwira, Richmond, Kagoda, Meremeta/Tangold, Gulfstream presidential jet, military helicopters, military vehicles, kamwe hazitafikishwa mahakamani chini ya utawala wa Kikwete.

Hoseah ana hulka ya uoga, si mtu bold kama Githongo ya Kenya, hivyo kwa kuwa hana support ya Kikwete kwenye vita dhidi ya ufisadi, tujue kuwa kilichobaki ni usanii tu wa kuridhisha wafadhili wasikate misaada. Wataendelea kuwa na selective prosecution of corruption cases by targeting relatively weaker suspects kama kina Mramba na wengineo.

Hawa US diplomats wako makini sana kwenye kazi yao. Nina hakika 100% kilichotoka WikiLeaks ndicho Hoseah alichosema. Pia kuna uwezekano mkubwa kuwa walimrekodi Hoseah bila ya yeye mwenyewe kujijua. Tusubiri kuna confidential audio and video files zitatolewa WikiLeaks siku zijazo.
 
KAMa KUNA MTU ANA CV YA DK HOSEAH AIPOST HAPA MAANA NAFIKIRI TATIZO NI LUGHA HAPPA INAWEZEKANA DK HAJUI KIMOMBO VIZURI SASA MMAREKANI KAELEWA VINGINE WAKATI DK ALIKUWA ANAELEZA VINGINE

CV PLS TUJUE ALIUNGA UNGA WAPI KUPATA UDAKTARI
 
Anachosema Dr. Hoseah ni kwamba for some reason, ofisa wa ubalozi wa Marekani anamsingizia. Huyo ofisa atakuwa na interest gani ya kuwadanganya viongozi wake kule Washington na kwenye issue kama hiyo. Kama alivyosema Nyambala hapo juu hawa wakuu wetu hawatakiri hata siku moja.

Sasa hivi tunamwona huyu Mkuu akijitahidi kulinda maslahi yake badala angekuwa mjasiri akasema yes ndiyo hivyo nilivyohisi wakati ule. Sidhani kama kuna mtu ambaye angemlaumu kama angesema hivyo lakini tunavyojua, hawa viongozi wetu wanaona ni lazima wajikombe kwa viongozi wao.

Ni lini wazungu wakawa na nia njema kwa waafrika? Nafanya nao kazi nawaelewa. They normally play around things! Nagombana nao kweli na wananichukia kwa kuwa sipendi umbeaumbea. Hasa hasa Waingereza na Wamarekani.
 
Dk Hoseah adaiwa kufichua siri za JK Monday, 20 December 2010 23:53 0diggsdigg

Waandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, anadaiwa kufichua siri za Rais Jakaya Kikwete kwamba kiongozi huyo wa nchi asingependa vigogo serikalini kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa.
hoseah.jpg
Dk Hoseah

Kadhalika, mkuu huyo wa Takukuru anadaiwa kushindwa kuwafikisha mahakamani vigogo waliohusika na kashfa ya rada kwa sababu anahofia usalama wake, gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti juzi.

Mbali na hofu hiyo, gazeti hilo pia lilieleza juzi kuwa Dk Hoseah alipewa maelekezo maalumu na Rais Kikwete kutoshughulikia kesi za rushwa zinazowahusu vigogo katika serikali yake na hasa marais waliomtangulia. The Guardian lilitoa taarifa hiyo likiunukuu mtandao wa habari wa WikiLeaks uliojizolea umaarufu duniani kwa kutoa habari za kiuchunguzi hasa baada ya mwasisi wake, Julian Paul Assange, kutiwa matatani.

Kwa mujibu wa habari hiyo, Dk Hoseah, alisema hayo Julai 14 mwaka 2007, alipokuwa akizungumza na mwanadiplomasia wa Marekani, Purnell Delly jijini Dar es Salaam. Alisema uchunguzi wa kashfa ya rada ni hatari kwake kwa kuwa vigogo nchini, hawaguswi kwa tuhuma na kwamba “tayari alikuwa ameanza kupata vitisho”.

Akizungumza kwa huzuni na kusononeka, Dk Hoseah alidai kuwa kwa ari na utashi alionao katika vita dhidi ya ufisadi, angeweza kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa ufisadi, lakini ameshindwa kwa kuwa kesi hiyo inawagusa vigogo kadhaa, wakiwamo marais na waziri mkuu mstaafu na ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). "Biashara hiyo chafu iliwahusisha maafisa kuanzia ngazi ya Wizara ya Ulinzi na afisa mmoja au wawili wa ngazi za juu ndani ya jeshi, The Guardian lilieleza likinukuu vinasa sauti vya ubalozi huo.

Dk Hoseah alitumia mkutano huo kueleza mafanikio ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na kueleza kuwa matumaini yake ya awali kusimamia mkakati huo, yamevunjwa moyo. "Alituambia waziwazi (rais) kwamba tuhakikishe kesi inayomhusu rais au waziri mkuu na viongozi waliomtangulia, tusiziguse na ziwekwe chini ya meza," lilieleza gazeti hilo katika taarifa yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria zake ndogondogo, mtu yeyote aliyewahi kuwa rais wa nchi hawezi kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zozote zinazomkabili.

Lakini, wadau kadhaa wa masuala ya siasa, sheria, haki za binadamu na utawala bora wamekuwa wakiendesha harakati za kudai katiba mpya ambayo pamoja na mambo mingine, wametaka iondoe kinga ya rais ya kutoshitakiwa mahakamani hata mara baada ya kustaafu kwenye nafasi hiyo.
“Kuna taarifa za ufisadi ndani ya Beki Kuu ya Tanzania (BoT). Pia Visiwani Zanzibar kuna mambo mengi yanayohusiana na rushwa na ufisadi,"alinukuliwa Dk Hoseah ambaye alieleza kuwa anaamini “maisha yake yatakuwa hatarini” iwapo atathubutu kuendesha uchunguzi huo.

Taarifa hizo kutoka kumbukumbu za vinasa sauti vya ubalozi wa Marekani nchini, zimeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Dk Hoseah alikuwa anarudia na kusisitiza kuhusu usalama wake, akisema anaamini maisha yake yapo hatarini kwa sababu alishapokea ujumbe wa vitisho kupitia simu yake ya mkononi na barua. "Amesema (Dk Hoseah) amekuwa akikumbushwa mara kwa mara kwamba katika vita hiyo ya ufisadi, anapigana na matajiri na wenye nguvu katika vita dhidi ya ufisadi,”gazeti The Guardian lilimnukuu Delly, afisa huyo wa Marekani aliyekuwa akizungumza na Dk Hoseah.
Imeelezwa katika taarifa hiyo kuwa sababu kubwa ya Dk Hoseah kujaribu kutia mguu kwenye sakata la rada ni taarifa ya uchunguzi wa Taasisi ya Kuchunguza Ufisadi ya Uingereza (SFO), ambayo ilieleza kinagaubaga kuhusu kesi hiyo. Delly alisema, Hoseah amekuwa akionywa katika vitisho hivyo kwamba anaweza akaiona chungu nchi yake ikiwa ataendelea na mapambano hayo.

"Alisema (Dk Hoseah), ukihudhuria mikutano ya ndani na vigogo wa serikali, wanataka wakuone ukijihisi kwamba wao ndio wamekuweka katika cheo chako, lakini ukiwa mbishi wa kushikilia misimamo yako tu, basi uko katika hatari,” gazeti hili lilimnukuu Delly. Awali akizungumza na gazeti hili, Dk Hoseah alikiri kupata vitisho vinavyohatarisha maisha yake kutokana na mapambano yake dhidi ya rushwa, lakini akasema hajaiona habari hiyo iliyonukuu mazungumzo yake na mwanadiplomasia huyo wa Marekani.

Hata hivyo, mtendaji huyo wa Takukuru alisema ni kawaida yake kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kila mwaka na kujadiliana nao mambo mengi kuhusu Tanzania. Alisema mabalozi ni wadau wakubwa katika bajeti ya Tanzania na hivyo huwa wanakutana kila mwaka kujadili mambo mbalimbali ya kuhusu kusaidia bajeti ya serikali. “Mimi huwa nakutana na mabalozi wa nchi mbalimbali kwa sababu wao ni wadau katika mradi wa ‘government budget support’ (Mpango wa kusaidia bajeti ya serikali), hivyo hilo sio tatizo,” alisema Dk Hoseah.

“Msimamo wangu ni kwamba mapambao dhidi ya ufisadi ni endelevu hadi hapo tutakapofanikiwa kumaliza tatizo hili,” alisema Dk Hosea na kukiri: “Vitisho vipo vingi tu, kutoka kwa watu wanaotuhumiwa, lakini si hata ninyi waandishi mnamwagiwa ‘tindikali’ katika mapambano yenu, hivyohivyo hata mimi napata vitisho.” Alisisitiza kuwa pamoja na vitisho hivyo, hawezi kurudi nyuma katika mapambano ya rushwa na ufisadi.
“I’m Tanzanian I will die in Tanzania, it is my country’ (mimi ni Mtanzania, nitakufa Tanzania, ni nchi yangu), siwezi kuhama nchi kwa vitisho vya watu wachache wanaotuhumiwa kwa ufisadi na rushwa,” alisisitiza Dk Hoseah. “Hilo la kwamba nafikiria kuhama nchi wametia chumvi si unajua magazeti? Sijafikiria kuhama nchi licha ya vitisho, mimi naona ni changamoto na jambo la kawaida katika mapambano,” aliongeza Dk Hoseah.

Kuhusu Rais Kikwete kukwamisha mapambano ya ufisadi kama alivyonukuliwa na gazeti hilo la The Guardian, Dk Hoseah alipiga chenga kulijibu badala yake akaeleza: “Ili umpeleke mtu mahakamani si lazima umtuhumu na kumfanyia uchunguzi? Lakini pia lazima tujenge utamaduni wa kuwaheshimu viongozi wetu.” Lakini baadaye saa 9:30 alasiri jana,Takukuru ilituma taarifa iliyoeleza kuwa Dk Hoseah ameshangazwa na Ofisa wa Ubalozi wa Marekani kumnukuu vibaya huku akisema hajui ana lengo gani.

Katika taarifa hiyo, Dk Hoseah alikiri kukutana na ofisa huyo wa Ubalozi wa Marekani ofisini kwake Julai mwaka 2007, lakini, akasema ripoti ya mazungumzo yao aliyoipeleka nchini kwake imechakachuliwa. “Kwa mfano haikutokea katika mazungumzo yetu kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete hakutaka kuruhusu sheria kuchukua mkondo wake, kuwashitaki vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kama ilivyodaiwa na Ubalozi wa Marekani,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na idara ya mahusiano ya Takukuru.
“Nilichosema ni kwamba Rais hayuko tayari kuruhusu kushitakiwa kwa vigogo wa serikali au mtu mwengine yeyote kwa tuhuma za uvumi au kwa ushahidi dhaifu, kwa sababu kufanya hivyo, serikali itakuwa hatarini kwa kulipa gharama kubwa ya fidia ikiwa mtuhumiwa huyo atashinda kesi mahakamani,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza.

Kuhusu hofu ya maisha yangu, nakumbuka niliulizwa na Ubalozi wa Marekani kwamba je, naogopea maisha yangu au la, nikiwa Mkuu wa Takukuru? Na jibu langu lilikuwa rahisi kwamba ‘bila ya shaka’ unapopambana na wakubwa na matajiri kama hao wanaotuhumiwa unapaswa kuwa makini na maisha yako. Lakini hata siku moja sikusema kwamba napanga kuhama nchi kwa sababu maisha yangu yapo hatarini.

Ni mshangao kuona kwa mara nyengine ofisa wa Ubalozi wa Marekani ananinukuu mimi vibaya au nje ya mada na sielewi kabisa lengo lao lilikuwa nini.” Alsema rekodi yake, akiwa Mkuu wa Takukuru iko wazi kabisa wakati wowote anapokuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya mtuhumiwa yeyote wa ufisadi hawaogopi lolote isipokuwa ni kumburuza mahakamani bila ya kujali cheo chake.

Naye Mkurugezi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu, hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa muda wote. Kwa upande wa msaidizi wake, Premi Kibanga aligoma kuzungumzia suala hilo kwa kile alichoeleza kuwa hajaisoma habari hiyo iliyochapishwa na gazeti la The Guardian la Uingereza.
“Mimi sijaiona wala kuisoma habari hiyo, hivyo siwezi kuzungumzia kitu ambacho sijakiona. Sina uhakika kwamba Dk Hoseah amesema hayo, pengine umemuelewa vibaya,” alisema Kibanga. Juhudi za kumpata Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alphonso Lenhardt, kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa baada ya simu yake ya mkononi kutokuwa hewani kila ilipopigwa.


HALAFU MAASKOFU WANATUAMBIA KUWA JK NI CHAGUO LA MUNGU. MUNGU YUPI? WATANZANIA TUKO NDANI YA KABURI.
 
Back
Top Bottom