Ukweli ni kuwa udukuzi upo mi nilisoma program moja hivi ya internet, wakaeleza kuwa ukiunganishwa na internet tu hauko salama kabisaa.
Wakaenda, mbali zaidi kuwa microwave, friji, na vifaa vyote vya electronic ni majanga.
Maana , wanaeleeza kuwa hata kama ukizima hivyo vifaa bado kuna chembechembe Fulani hazizimi zinadukua kimyakimya .
Pia, pana mwingine ameuliza kuwa watu tuko wengi au billions tunaotumia internet na simu kwa kifupi ni kuwa CIA na intelligence system nyingi zimetengeneza xinaitwa intelligence software sytem ambayo imewekewa language code detectors , ambazo wakati ukiongea hiyo software inachambua automatically hizo coded languages/ words ili Simu uliyopiga ichunguzwe zaidi kwa hiyo wote billion tukiongea wanachukua zile Simu ambazo software itakuwa imetoa ishara kuwa Simu mbili au nne haziko salama.
Sasa hapo, utaona vitengo vile 5 vya CAI hapo chini vinachukua nafasi yake hadi utadakwa tu.
Zaidi, aliyesema tutumie barua, mfano makao mkuu ya CIA, wana vitengo kama 5
1. Mathematicians
2. Information system technicians ( computer experts and internet - ,ICT unity )
3. Linguistics mfano, USA wana hiki kikundi cha peace corps wale wanajifunza hadi lugha mama kisha wanaenda kutengeneza language codes za hizo lugha kwa hiyo hata ukiongea kimasai wataelewa tu ( MF. Kimasai, haajifunzi mambo yote wana mbinu za kujifunza maneno wanayoyataka na ndiyo maana basi hao peace corps wa kutoka USA huwa wanafanyiwa mafunzo kabla ya kuja huku Africa hata Tz mfano, mwaka huu wana kuja 50 hapo Tanzania)
4. Biologist hasa wale wa maabara
5. Na Intelligence analysits
Sasa hapo kila watu, wanafanya kazi zao.
Mfano, ukisema utumie barua , barua ikiwa na utata wanaipeleka maabara kitengo na 4, wanafanya kazi ya kutafuta aina ya wino ulioandikia, umetoka nchi/ umetengenezwa nchi ipi? Na kisha linguistics wanatoa maana ya maneno uliyoandika kisha intelligence analyst wanafanya kazi zao.
Kwa kifupi, ni kuwa hauko salama na pia uko salama.
Mfano, gaidi atajulikana hayupo salama.
Asiye gaidi itamsaidia kuwa salama.maana kila mahala alipo ataonekana na kusaidia hata kama uko katika matatizo.
Kwa hiyo usiri na maisha ya pekee ( privacy ) ni hakuna tena.
Maoni zaidi wadau .