Wikileaks wadai Afrika inachunguzwa na CIA kwa kutumia vifaa kama simu za mkononi na runinga

Wikileaks wadai Afrika inachunguzwa na CIA kwa kutumia vifaa kama simu za mkononi na runinga

Mkuu usijaribu, hawatojua kuwa unajaribu. Itakupa shida sana.
Ngoja nikupe senario:
Kuna jamaa alishawai kuniambia kuwa nchi ya Israel inefanya tafiti za lugha nyingi na kuzihifadhi ktk softwere hivyo mazungumzo yyote hatarishi ktk devices ina detect hii aliniambia inafanyika sana ni ndani ya Israel. So,CIA can go beyond that.

Kumbuka alichokisema Snowden kuhusu usiri wa watu ktk nazungumzo ya simu.

Senario ya mwisho.
Jirani yangu ni dereva US embassy DSM. Kuna siku mfanyakazi wa gari la maji alipitisha gari nyumbani kwake kutokana na shida ya maji, mkewe na majirani kama wanne wakawa wanachota kutoka ktk ile gari. Kumbe camera ya ile gari inatuma image Pentagoni then ndo inarudishwa ubalozini. Pentagon wakapiga simu kuwa hiyo gari isirudi ubalozini ba jamaa ikawa mwisho wa kazi.

Don't try what you are suggesting itakukost....

Mkuu kuna Watu huwa hawakai na kujiuliza maana ya binadamu kuumbwa kwa sura na Mfano wa Mungu.Sisi binadamu ni sehemu ya waumbaji.Watu Wengi wangejua maajabu ya tekinolojia yote iliyokwisha vumbuliwa duniani toka kuwepo kwake wangestaajabu sana.Ngoja dunia iendelee kuwa "kiganja" kutoka kuwa "Kijiji" tutastaajabu zaidi.Juzi nimeona Ndege moja YouTube iki-takeoff na kufanya Landing majini.Maana yake Watu wanaanza kutafuta solution ya Ndege kutua majini panapokuwa na dharura Na nimeona Ndege ikitua kwenye mlima.Maana yake hiyo ni hatua kuelekea kutatua tatizo la Ndege kushindwa kutua mahali pasipo Na uwanja.Tatizo ni sisi Waafrika kuyapa kipaumbele majungu, matukio ya maisha ya Watu wengine Na kusahau kukabiliana Na changamoto zilizo mbele yetu.Watu wanaendelea kuaminishwa Na akina Lusekelo Na Gwajima kuwa tatizo la maendeleo yetu ni uchawi, laana Na mapepo.Tatizo letu ni kupata vyeti halafu tunavifanyia Lamination Na kwenda kuviweka kwenye briefcase Na mabegi Na kisha kusubiria kutangaza sifa za vyeti hivyo kwenye harusi, misiba Na makungamano mbalimbali kwa majina Dr, Prof Na Vinginevyo.
 
Shirika la Ujasusi la kitanzania (Shilawadu) halihitaji software...... 😀
 
Acheni utani huku ninako ishi mimi ni mbali sana hawawezi nichunguza hata kidogo japo natumia kilakitu
 
mbona rahisi tu...wewe mpigie mtu simu,akipokea anzisha mazungumzo halafu chomekea maneno haya

"I'm planning to attack america tomorrow".

"my jihad brothers are on the way to USA to attack the white house".

" the suicide vest is complite".

pia unaweza ukayabadili kwa kiluga chenu almradi tu uwe unayatamka hewani ktk simu.

halafu sikilizia.
hahahaha
 
Ukweli ni kuwa udukuzi upo mi nilisoma program moja hivi ya internet, wakaeleza kuwa ukiunganishwa na internet tu hauko salama kabisaa.

Wakaenda, mbali zaidi kuwa microwave, friji, na vifaa vyote vya electronic ni majanga.

Maana , wanaeleeza kuwa hata kama ukizima hivyo vifaa bado kuna chembechembe Fulani hazizimi zinadukua kimyakimya .

Pia, pana mwingine ameuliza kuwa watu tuko wengi au billions tunaotumia internet na simu kwa kifupi ni kuwa CIA na intelligence system nyingi zimetengeneza xinaitwa intelligence software sytem ambayo imewekewa language code detectors , ambazo wakati ukiongea hiyo software inachambua automatically hizo coded languages/ words ili Simu uliyopiga ichunguzwe zaidi kwa hiyo wote billion tukiongea wanachukua zile Simu ambazo software itakuwa imetoa ishara kuwa Simu mbili au nne haziko salama.

Sasa hapo, utaona vitengo vile 5 vya CAI hapo chini vinachukua nafasi yake hadi utadakwa tu.


Zaidi, aliyesema tutumie barua, mfano makao mkuu ya CIA, wana vitengo kama 5
1. Mathematicians
2. Information system technicians ( computer experts and internet - ,ICT unity )
3. Linguistics mfano, USA wana hiki kikundi cha peace corps wale wanajifunza hadi lugha mama kisha wanaenda kutengeneza language codes za hizo lugha kwa hiyo hata ukiongea kimasai wataelewa tu ( MF. Kimasai, haajifunzi mambo yote wana mbinu za kujifunza maneno wanayoyataka na ndiyo maana basi hao peace corps wa kutoka USA huwa wanafanyiwa mafunzo kabla ya kuja huku Africa hata Tz mfano, mwaka huu wana kuja 50 hapo Tanzania)
4. Biologist hasa wale wa maabara
5. Na Intelligence analysits

Sasa hapo kila watu, wanafanya kazi zao.

Mfano, ukisema utumie barua , barua ikiwa na utata wanaipeleka maabara kitengo na 4, wanafanya kazi ya kutafuta aina ya wino ulioandikia, umetoka nchi/ umetengenezwa nchi ipi? Na kisha linguistics wanatoa maana ya maneno uliyoandika kisha intelligence analyst wanafanya kazi zao.

Kwa kifupi, ni kuwa hauko salama na pia uko salama.

Mfano, gaidi atajulikana hayupo salama.
Asiye gaidi itamsaidia kuwa salama.maana kila mahala alipo ataonekana na kusaidia hata kama uko katika matatizo.

Kwa hiyo usiri na maisha ya pekee ( privacy ) ni hakuna tena.

Maoni zaidi wadau .
Mkuu unaonaje ukatutolea mifano ya matukio yenye uhalisia ambayo hayo mambo yalitumika kugundua uhalifu.
 
Kama ni hivyo Osama asingelipua marekani vitisho amabvyo avina msingi
 
CIA wanahangaika kutupeleleza sisi maskini lakini sidhani kama kuna cha maana watakipata toka kwetu,hizi simu mara nyingi watu wanazitumia kwenye kuwasiliana na michepuko yao,kuweka appointment ya kukutana.Hatuna interest na mambo ya US
 
hahaha umetisha mkuu
ndo hivyo kiongozi maana wadaku wakisikia tu faragha yetu haipiti hata dakika 5 utaipata audio whats app tabu yote yanini kujijazia mamsongo na kupasuana bandama bureee!
 
Haya yaliyosemwa na wikileaks siyaamini hata asilimia 50%
Walishindwa nini kuzui mashambulizi yale yaliyowapata
Na vipi kuhusu wale vijana walio kuwa wana tengeneza passport fake mpaka sasa hawajawapata ni vitisho tu kama walivyozoea kucheza drama zao,

Msiwe wajinga kufikiri na kuchanganua mambo
Kuna baadhi ya mambo ni sawa kama kuhack
Lakini msemavyo friji inawatumia taarifa hasa hivi vitu vya kielectonic si kweli maana si kazi rahisi kwenda kila nchi kuingia na makampuni mkataba na kuchomeka hizo chip sa sijui wameweka WI-FI kwenye jokofu...!

Basi nikitaka kutambua kama kuna utumaji wa taarifa nitatumia njia ya chini kabisa kutambia nawasha kiredio kidogo kisha naanza kukinzungusha ili mawimbi yaingiliane nisikie kikiunguru.
 
Kama ni hivyo Osama asingelipua marekani vitisho amabvyo avina msingi
SHIDA HULETA MAARIFA.BAADA YA HAPO WAKATULIZA VICHWA NA KUPATA HILI WAZO HATA TUKIWA SEBULENI,MSALANI,BAA,KWENYE BAO,KAHAWA NAKADHALIKA BASI WATUONE AU WATUSIKIE KWA KILA TUNACHOFANYA
 
Back
Top Bottom