Kwa hiyo Mkuu hapo ndio kusema kuwa Waafrika hatuwezi kutoka kwenye tope tulilozama auu kuna njia gani tufanye ili tutoke tulipo ??
Kutoka naona tunaweza mkuu, japo mimi sio mtaalam wa mambo yenyewe
Wazungu wako mbele Kwasababu wametuzidi maarifa au teknolojia. Kwa kutumia mauchawi hayo wanatengeneza vitu na kutuuzia kwa bei watakapo wao. Unaweza kuta maligafi wanaiba kwetu. Kwa hili laiti bei za maligafi na final product zingewiana wasinge tuacha mbali kihivyo. Lakini, mfano wanaiba coltan Kongo na kutengeneza simu halafu bei wanatupangia na sisi tunahitaji simu. Inakula zaidi kwetu
Uarabuni wako mbele sababu ya mafuta. Naona kwa kiasi kikubwa wamedhibiti mali asili yao. Inawanufaisha. Nasisi tungekuwa na utajiri wa madini kama Kongo halafu tukahakikisha tunafaidika nayo tungekuwa mbali.
So, naona ni teknolojia na maliasili ambayo kwingineko inahitajika sana
Kwa Teknolojia ni ngumu. Kufanya kama wachina wanaosifika kwa kuibia wazungu teknolojia zao ni ngumu kujipanga, mfano tu. Lakini linawezekana
Tangia kipindi cha mkapa kama tungejipanga vizuri katika ubinafsishaji na uchimbaji wa madini uliokuwa unafanywa na wageni naona hali zetu zingekuwa bora zaidi. Na hili ni pamoja na kuwa na mipango bora na kuwa na vipaumbele vizuri
Kutoka tunaweza. Lakini ni vita kali. Kenya wasingependa tuwe na viwanda vya blueband ili tuendelee kuwa mateja wao, mfano tu. Kuna watu wangependa waje wamhonge rais na wasaidizi wake ili wachimbe bure dhahabu na nk. Sasa hela za kujengea barabara na kununulia vifaa vya shule zitatoka wapi?