Wilaya Kaliua na sakata la Mwalimu Johari kupigwa ofisini

Wilaya Kaliua na sakata la Mwalimu Johari kupigwa ofisini

Wilaya ya Kaliua inakumbwa na majanga mengi kwa watumishi wake changamoto inayoikabili wilaya ni Rushwa ya ngono kwa watendaji wake hasa wakuu wa vitengo kuwakata watumishi wa kada za chini.

Tukianzia sakata la mwalimu johari kupigwa na mkuu wake wa shule. Ni kweli mkuu wa shule alimpiga mwalimu na kumdhalilisha vibaya. Haswa.Unajua waalimu wengi huwa ni waoga sana wakiambiwa waseme watoe ushahidi wengi wao huishia kukimbia. Uzuri mwalimu Johari namfahamu na nimefanya nae kazi ni mchapa kazi kweli sio madam wa kulia lia. Aliipaisha shule ya msingi Ufukutwa na ikawa inafanya vizuri. Alikuwa promoted to halmashauri.

Changamoto alialiyoipata mwalimu Johari kutakwa kimapenzi na mkuu wake wakitengo Kwani mwalimu mkuu anatumika na afisa elimu kumbana mwalimu johari. Yaani huyo afisa elimu naona karibia waalimu wa kike wote ni mademu zake. mfano kuna mwalimu mmoja anaitwa madam Siwa wa mwangaza primary kila ikotokea kazi maalum lazima apate na mara nyingi huwa madam anapewa special duty mfano kuwa reseved party. Kufanya kazi wilaya ya Kaliua kwa wanawake ni shida bora hata kipindi cha pima.

Ukija sekondari ndio balaa kuna mkuu mmoja Kaliua high school bado ni kijana sana na dhani wangesubiri kidogo nafasi aliopewa nadhani anakula sana wanafunzi ni ushari tu, alikuwepo mkuu mmoja anaitwa Beni physics yeye ilikuwa kazi yake ni kuuza vyakula vya wanafunzi, sasa huyu wa sasa kazi yake ni kula wanafunzi sasa hofu yangu nikale ka ugonjwa ketu pia headmaster wa Kaliua ni rafiki yake na afisa elimu sekondari. Kazi ni kupasiana watoto zetu.

Mkurugenzi wa Kaliua (mandevu) yeye yuko busy na simu muda wote. Yeye mwenyewe ndio anaongoza kula wafanyakazi, kiufupi Kaliua hatuna mkurugenzi yule anafaaa kuwa kiongozi katika magroup ya watsap,insta,facebook, telegram na n.k.Maaanake kila ukiongea nae yuko busy kuna malalalamiko mengi sana katika waliya hii lakini yeye yuko,

Mfano kuna kijana mmoja anaitwa mpaji ni kiongozi wa uvccmm kazi yake ni kuwaibia vijana pesa kwa kuwaambia vijana kuna ajira mwisho wa siku mtu anaambukia vumbi kali. Kesi zimepelekwa viongizi wa chama chake lakini wameishia kulindana, mfano kuna jammaa kapigwa 1.5m kesi iko kwa mkurugenzi mpaka sasa. Mkurugenzi mpaka sasa anazungusha na kijana yuko mtaani anadunda.
Ukiaangalia kwaundani Kaliua mpaka sasa haina viongozi wala nini, hasa huyu DED na DAS (man from UDOM) wake ndio hovyo kabisa, mkuu wa wilaya anapiga kazi vizuri
Acha kumtetea mkuu wa wilaya , kifupi mkuu wa wilaya naye hafai kuwepo hapo kwa sababu naye ni sehemu ya tatizo

Haiwezekani wilaya iwe na tuhuma nyingi kiasi hicho nayeye yupo na hayo yote yapo ndani ya mamlaka yake halafu uniambie eti mkuu wa wilaya anachapa kazi !?

Hapana mkuu wa wilaya naye ni tatizo hapo kaliua.
 
Adui ya mwalimu ni mwalimu.

Poleni jamani, maisha gani hayo kama digidigi hakuna amani??

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Waliposhindwa kuwakemea MaRc na MaDc kucharaza watu wazima bakora tena hadharani ilikua ni mwanzo mwa vitendo viovu watu kujivika ufalme
 
For sure mwalimu johari hana kiburi chochote nimefanya nae kazi kama mkuu wangu namfahamu sana sasa haya ya kiburi labda wamekutuma. Malalamiko mwngi sana yako halmashauri nitayaweka hapa ili muone watu wanavyojifanya mungu watu katika halmashauri zetu
Wewe siyo moyo wake, unakomaa na hoja eti Johari hana kiburi. Alichokifanya kwako sicho atakachokifanya kwangu.
 
Mkuu Chato tena sikuelewi!! Mara Johari kapandishwa cheo yupo halmashauri, mara yupo shuleni chini ya Mwl Mkuu. Amepigwa akiwa wapi? Inaonekana Johari aliwahi kupata cheo zamani na kushushwa, kisa nini? Embu ongea vizuri tujue pa kuanzia.
 
Amenikela sana we acha tuu
Una uhakika na ushahidi Headmaster Kaliua High school na DEO Secondary wanashirikiana kuwala wanafunzi? Unajua umechoma Moto kichaka? Unaweza kutoa ushirikiano kwa tuhuma hizi za hovyo za watumishi wetu? Unafahamu majina na vidato vya wanafunzi? Mazingira ya kuvuana chupi je? Umeripoti Polisi, PCCB, Usalama wa Taifa, kwa Afisa utumishi au kwa DC nk?
 
Mwaliku wa kike akiolewa anakuwa mstaarabu ila akiwa singo maza na hajaolewa huo moto wake hakuna wa kusogea.
 
Sasa wizi unafanywa na kiongozi wa chama unaenda mlaumu mkurugenzi hawajabiki inawezekana kweli?
 
CWT wanafanya nini? Michango ya kujenga mavitambi tu. Na nyie waalimu mmezidi miss maboya this is slavery.
 
Hapa mwalimu mkuu anakosa na Ana kesi ya kujibu na napendekeza avuliwe madaraka Mara moja.

Kwa vyovyote vile na bila kujali Johari alijibu nini au alikosea nini mkuu Hana mamlaka kisheria Wala kijamii ya kumpiga MWALIMU.
 
Una uhakika na ushahidi Headmaster Kaliua High school na DEO Secondary wanashirikiana kuwala wanafunzi? Unajua umechoma Moto kichaka? Unaweza kutoa ushirikiano kwa tuhuma hizi za hovyo za watumishi wetu? Unafahamu majina na vidato vya wanafunzi? Mazingira ya kuvuana chupi je? Umeripoti Polisi, PCCB, Usalama wa Taifa, kwa Afisa utumishi au kwa DC nk?
Niko on field na niko kazini kama ukitaka maushahid kama yote yapo hakuna shida halafu siandikagi vitu vya kubumba kaka.
 
Kwa namna ulivyopangilia mada nyingi katika moja, na kutaja taja majina ya watu na vyeo vyao inaonekana mtoa post unajaribu kuwachafua watu ili waharibikiwe na nafasi zao!

Piga kazi hakuna mshahara ktk kufanya majungu sana sana utaumia roho na kupata vidonda vya tumbo hasa pale unapowaona uliowachafua wanadunda na kufanya kazi zao.
 
Back
Top Bottom