Wilaya Kaliua na sakata la Mwalimu Johari kupigwa ofisini

Acha kumtetea mkuu wa wilaya , kifupi mkuu wa wilaya naye hafai kuwepo hapo kwa sababu naye ni sehemu ya tatizo

Haiwezekani wilaya iwe na tuhuma nyingi kiasi hicho nayeye yupo na hayo yote yapo ndani ya mamlaka yake halafu uniambie eti mkuu wa wilaya anachapa kazi !?

Hapana mkuu wa wilaya naye ni tatizo hapo kaliua.
 
Adui ya mwalimu ni mwalimu.

Poleni jamani, maisha gani hayo kama digidigi hakuna amani??

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Waliposhindwa kuwakemea MaRc na MaDc kucharaza watu wazima bakora tena hadharani ilikua ni mwanzo mwa vitendo viovu watu kujivika ufalme
 
Wewe siyo moyo wake, unakomaa na hoja eti Johari hana kiburi. Alichokifanya kwako sicho atakachokifanya kwangu.
 
Mkuu Chato tena sikuelewi!! Mara Johari kapandishwa cheo yupo halmashauri, mara yupo shuleni chini ya Mwl Mkuu. Amepigwa akiwa wapi? Inaonekana Johari aliwahi kupata cheo zamani na kushushwa, kisa nini? Embu ongea vizuri tujue pa kuanzia.
 
Amenikela sana we acha tuu
Una uhakika na ushahidi Headmaster Kaliua High school na DEO Secondary wanashirikiana kuwala wanafunzi? Unajua umechoma Moto kichaka? Unaweza kutoa ushirikiano kwa tuhuma hizi za hovyo za watumishi wetu? Unafahamu majina na vidato vya wanafunzi? Mazingira ya kuvuana chupi je? Umeripoti Polisi, PCCB, Usalama wa Taifa, kwa Afisa utumishi au kwa DC nk?
 
Mwaliku wa kike akiolewa anakuwa mstaarabu ila akiwa singo maza na hajaolewa huo moto wake hakuna wa kusogea.
 
Sasa wizi unafanywa na kiongozi wa chama unaenda mlaumu mkurugenzi hawajabiki inawezekana kweli?
 
CWT wanafanya nini? Michango ya kujenga mavitambi tu. Na nyie waalimu mmezidi miss maboya this is slavery.
 
Hapa mwalimu mkuu anakosa na Ana kesi ya kujibu na napendekeza avuliwe madaraka Mara moja.

Kwa vyovyote vile na bila kujali Johari alijibu nini au alikosea nini mkuu Hana mamlaka kisheria Wala kijamii ya kumpiga MWALIMU.
 
Niko on field na niko kazini kama ukitaka maushahid kama yote yapo hakuna shida halafu siandikagi vitu vya kubumba kaka.
 
Kwa namna ulivyopangilia mada nyingi katika moja, na kutaja taja majina ya watu na vyeo vyao inaonekana mtoa post unajaribu kuwachafua watu ili waharibikiwe na nafasi zao!

Piga kazi hakuna mshahara ktk kufanya majungu sana sana utaumia roho na kupata vidonda vya tumbo hasa pale unapowaona uliowachafua wanadunda na kufanya kazi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…