Adili Utotole
Member
- Jul 20, 2022
- 14
- 14
Wilaya ya Kiteto ipo Kusini mwa mkoa wa Manyara. Kiteto ina kilomita za mraba 16,685 na jumla ya wakazi 244,669 kwa mujibu wa Senasa ya mwaka 2012.
Upande wa Mashariki Kiteto imepakana na mkoa wa Tanga , Kusini mkoa wa Dodoma, Kusini Mashariki Mkoa wa Morogoro upande wa Kaskazini imepakana na Wilaya ya Simanjiro na Magharibi imepakana na Wilaya ya Babati ambayo ndiyo makao makuu ya mkoa wa Manyara.
Ni kilomita takribani 77 kutoka njia panda ya NACCO , barabara kuu ya lami kuelekea Dodoma mjini mpaka kufika makao makuu ya Wilaya ya Kiteto (Kibaya mjini).
Kiasili wenyeji wa Wilaya hii ni Wamasi, lakini kutokana na kuendelea na kupanuka kwa mji ,Sasa hivi Kiteto kuna makabila kutoka mikoa mbalimbali. Kwa Sasa kilimo ndicho uti wa mgongo maeneo mengi ya Kiteto tofauti na ufugaji, ni kwa sababu ya uwepo wa hali nzuri ya hewa na udongo wenye rutuba.
Maeneo ya kilimo Kiteto yanapatikana katika kata za Dosidosi, Engusero, Njoro, Mbigiri, Kijungu, Lengati, Sunya ,Lengatei ,Lupopong, Laitimi, Pori namba moja na Pori namba mbili, Kisima ,Grosari ,Mirerani ,Mbeli, maeneo ya Ndedo na eneo maarufu la mashamba ya kukodi Kwa Mkorea.
Wakulima wengi Sasa wamegeukia zao la Alizeti kutokana na kuongezeka kwa soko la zao hilo kwa sababu ya uhaba wa mafuta ya kupikia maeneo mengi ya Dunia hali inayosababishwa na kuendelea kwa vita vya Urusi na Ukreine. Kiteto ndiko ambapo wafanyabiashara na Taasisi Kama JATU wamewekeza mashamba ya mahindi na Alizeti.
Leo hii ukienda Kiteto mjini utashangaa kuona kila mtaa zikiwa zimesimikwa mashine nyingi za kukamua na kuchuja mafuta ya Alizeti. Mtaa wa sokoni pekee una takribani mashine Saba ,Uwanja wa michezo wa halmashauri kuna mashine tatu ambazo zimesimikwa kwa kufuatana ,yani ni umbali wa mita kumi au 15 ilipo mashine nyingine.
Ekari moja ya Alizeti hutoa wastani wa gunia nane hadi tisa Kama msimu ukiwa mzuri, msimu wa mavuno huanzia shilingi 60,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 120,000 au shilingi 130,000 kwa gunia la debe Saba, huku gunia moja likitoa wastani wa Lita 17 Hadi 22 za mafuta . Alizeti Wilayani Kiteto huchukua miezi mitatu Hadi minne tangu ipandwe mpaka mavuno kwa mbegu ya kisasa. Wakati mahindi hutoa wastani wa gunia tano au Saba kwa ekari moja ,Bei huanzia shilingi 30,000 kipindi Cha mavuno hadi kufikia ukomo wa shilingi 70,000 kwa gunia la debe sita na huchukua Hadi miezi sita mpaka kuvunwa.
Mfano ,Mimi kwa msimu wa kilimo 2021 - 2022 nilikodi na kulima ekari nane na nusu Lengati ,ambapo mahindi nililima ekari moja tu. Lakini Alizeti nimevuna gunia 43 huku mahindi nikiambulia debe nne ,ukizingatia kulikuwa na Mvua chache msimu uliopita ,mzee mmoja jirani yangu alilima ekari 40 za mahindi amevuna gunia 16 tu ,pia ninaye ndugu yangu yeye alikodi shamba ekari tano Dodoma,sehemu kubwa alipanda Alizeti, lakini amevuna gunia sita za Alizeti na kupata mbili za mahindi. Unaweza kuona maajabu ya Alizeti kwa mashamba ya Kiteto.
UTAPATAJE SHAMBA KITETO
Mashamba Wilayani Kiteto yanapatikana kwa kukodi au kununua. Kukodi ekari moja hugharimu shilingi 35,000 Hadi shilingi 50,000 kwa mashamba yenye rutuba nzuri, Japo yapo mpaka mashamba ya 25,000 Ila ukikutana na Mmasai kavurugwa anaweza kukodisha hata eneo lenye mawe, [emoji3]. Kulima kwa trekta ni shilingi 35,000 Hadi 40,000 ekari moja kwa Sasa ,kupalilia huanzia shilingi 20,000 Hadi 60,000 kwa majani marefu.
Kwa mashamba ya kununua huanzia shilingi 500,000 Hadi 1,000,000 kwa ekari moja, pia ni nadra Sana kupatikana kwa Sasa hivi. Unapo maliza tu kuvuna ndipo unafanyika utaratibu wa kutafuta shamba kwa msimu ujao. Kuanzia mwezi wa tisa sio rahisi kupata shamba Kiteto sababu ya uhitaji mkubwa wa watu.
FAIDA ZA KUWA NA SHAMBA LA ALIZETI KITETO
(i) Kuongeza kipato katika familia hata mtu binafsi ,kwa sababu maeneo tajwa juu yana kawaida ya kutoa mavuno mengi ya Alizeti tofauti na mazao mengine
(i) Kuondokana na uhaba wa mafuta ya kupikia, ukienda maeneo ya Kiteto ,kumuona mtu anaenda kununua mafuta ya kupikia ni aghalabu ,Sana Sana ni wageni au wanaokwenda kuweka kambi mashambani,kila mtu hujitahidi kuwa na mafuta yake ndani.
Hakuna gharama ya kukamua na kuchuja mafuta ya Alizeti Kiteto,hata uwe na gunia 200 Unaenda kukamua ,unachujiwa na kuondoka ,sijajua kwa maeneo mengine ya nchi.
(iii) Kuongeza ajira
Ukilima Kiteto utakuwa umeongeza ajira kwa vijana, madereva wa trekta, wasaidizi wao ,na wale wanaofanya kazi za shamba ,kulima, kupalilia na kuvuna.
MASOKO
Soko la Alizeti Sasa hivi ni la uhakika kila sehemu, hata pale unapoamaliza kuvuna wafanyabiashara wanakufuata shambani uwauzie Alizeti ,ukikamua pia utauza mafuta.
Kama wewe ni mgeni Kiteto yapo maghala ya kukodi ili kuweka mazao ,yapo mpaka karibu na mashambani.
CHANGAMOTO ZA KILIMO CHA ALIZETI KITETO
(i) MUDA
Wageni wengi hushindwa kulima kutokana na kukosa muda wa kusimamia mashamba ,kilimo chochote huhitaji uangalizi. Unapopanda mbegu ya Alizeti lazima uhakikishe imeota ,Kama haijaota vizuri lazima utafute watu upandie tena, la sivyo utacheza mchezo wa pata potea.
(ii) MTAJI
Unapo hitaji au kupata shamba la kulima lazima uwe na pesa, hakuna shamba la kukopeshwa ,mmiliki anataka hela mkononi .
(iii) Changamoto ya Vibarua
Ukianza harakati za kulima ukiwa Kiteto usithubutu kusema "natafuta Vibarua", hautapata ndugu, watu hawapendi kabisa kuitwa Vibarua kule na wengi wao sio wenyeji ,huchukuliwa sehemu tofauti tofauti . Ukipata wenyeji watafanya kazi lakini watakuchelewesha,watakuja saa nne asubuhi ,watalima au kuvuna saa Saba mchana wanarudi kwao. Pia hupenda Bei ya juu ,huduma nzuri Kama kunywa chai asubuhi na kula ubwabwa wa Nyama kila siku [emoji3]
Msimu wa mavuno ukiwa mzuri ,msimu unaofuata Vibarua huwa wachache ,msimu ukiwa mbaya unaofuata Vibarua huwa wengi.
Ni hayo machache kuhusu fursa za mashamba Wilayani Kiteto,naomba maoni na kura yako pia , mawasiliano yangu kwa email ,utotolemoja@gmail.com

Upvote
13