A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Mbinga Mkurugenzi amelazimisha shule zote za Sekondari kuanzia Mwaka 2025 kuwa Kidato cha kwanza wanatakiwa kusoma masomo yote bila kujali wameyachagua au la, kitu ambacho ni kinyume na Mtaala wa Elimu wa 2014 ulioboreshwa wa 2023.
Mtaala huo wa sasa unawataka wanafunzi kusoma masomo 6 ya lazima na kuongeza masomo chaguzi mawili ama matatu ila yasizidi 10.
Yeye anadai kuwa Kidato cha Kwanza na Kidato cha Pili hawana uwezo wa kuchagua masomo, hivyo wasome yote watachagua wakifika kidato cha tatu sasa hili linafanyika naona hakutakuwa na utofauti na utaratibu uliopita unaomlazimisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha pili kusoma masomo yote.
Mimi kama Mwalimu sio haja ya kuwa na Mtaala ulioboreshwa ikiwa Serikali na Wizara ya elimu na taasisi zilizo chini yake wanapambana kuboresha Elimu harafu watu wa ngazi ya chini kwenye utekelezaji nao wanakuja na mipango yao. Wanajua hairuhisiwi kabisa ndyo maana hawajatoa barua rasmi.
Tangazo halijatolewa kwa maandishi, linatolewa kwa mdomo na kwa ukali kila tukikutana nao.
Aliagiza Mkurugenzi baada ya hapo Maafisa elimu Taaluma nao wakawa wanatilia mkazo kila tukikutana nao. Hata juzi wamesistiza tena kuwa hakuna kuwatenga wanafunzi.
Naona wanakwepa kutoa agizo la maandishi kwa maana wanajua athari zake. Ila wanasisitiza kwa nguvu kuwa "Mbinga DC utaratibu wetu sio kuwatenga wanafunzi watachagua masomo wakiwa kidato cha tatu" jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Wizara na Taasisi ya Elimu.