A
Mkurugenzi yuko sahihi kabisa,natamani hili liwe agizo kwa nchi nzima,mtoto wa miaka 12/13 Hana uwezo wa kuchagua masomo,asome yote akifika kidato cha tatu atakuwa ameshapambanua sayansi ni ipi na art ni ipi.Wilaya ya Mbinga Mkurugenzi amelazimisha shule zote za Sekondari kuanzia Mwaka 2025 kuwa Kidato cha kwanza wanatakiwa kusoma masomo yote bila kujali wameyachagua au la, kitu ambacho ni kinyume na Mtaala wa Elimu wa 2014 ulioboreshwa wa 2023.
Mtaala huo wa sasa unawataka wanafunzi kusoma masomo 6 ya lazima na kuongeza masomo chaguzi mawili ama matatu ila yasizidi 10.
Yeye anadai kuwa Kidato cha Kwanza na Kidato cha Pili hawana uwezo wa kuchagua masomo, hivyo wasome yote watachagua wakifika kidato cha tatu sasa hili linafanyika naona hakutakuwa na utofauti na utaratibu uliopita unaomlazimisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha pili kusoma masomo yote.
Mimi kama Mwalimu sio haja ya kuwa na Mtaala ulioboreshwa ikiwa Serikali na Wizara ya elimu na taasisi zilizo chini yake wanapambana kuboresha Elimu harafu watu wa ngazi ya chini kwenye utekelezaji nao wanakuja na mipango yao. Wanajua hairuhisiwi kabisa ndyo maana hawajatoa barua rasmi.
Tangazo halijatolewa kwa maandishi, linatolewa kwa mdomo na kwa ukali kila tukikutana nao.
Aliagiza Mkurugenzi baada ya hapo Maafisa elimu Taaluma nao wakawa wanatilia mkazo kila tukikutana nao. Hata juzi wamesistiza tena kuwa hakuna kuwatenga wanafunzi.
Naona wanakwepa kutoa agizo la maandishi kwa maana wanajua athari zake. Ila wanasisitiza kwa nguvu kuwa "Mbinga DC utaratibu wetu sio kuwatenga wanafunzi watachagua masomo wakiwa kidato cha tatu" jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Wizara na Taasisi ya Elimu.
Mkuu unagangaika na mwalimu mzembe asiye na chembe ya huruma na utu kwa watoto wetu.Tafuta email ya mkenda weka msisitizo
Mkuu uishi maisha marefu,umeandika nilichokuwa nafikiria,huyo Mkurugenzi Yuko sahihi mtoto wa miaka 12 ana uelewa Gani??Mkurugenzi yuko sahihi kabisa,natamani hili liwe agizo kwa nchi nzima,mtoto wa miaka 12/13 Hana uwezo wa kuchagua masomo,asome yote akifika kidato cha tatu atakuwa ameshapambanua sayansi ni ipi na art ni ipi.
Huu ulalamishi ni wa walimu wa sayansi ambao ni wazembe,wamepata kichaka cha kujifichia , hawataki kuwa na kundi kubwa la watoto kwa mgogo wa sayansi.
Walimu tuwe na huruma na utu,wewe mwalimu kwa akili ya kawaida mtoto wa wa kidato cha kwanza anauelewa wa kubainisha habari za sayansi, biashara au uchumi!? Chukulia ni mtoto wako anakuletea taarifa kuwa walimu wamemkataza asisome sayansi,ili Hali mtoto yuko kidato cha kwanza.
Hapa shuleni kwangu Kuna bomu ambalo litalipuka 2028, watoto walikimbilia sayansi bila kuwa na uelewa dheni sasa wanaona sayansi ni ngumu,wakitaka kurudi art hawawezi kwani Kuna masomo hawajasoma Toka form one
Binafsi nampongeza mkurugenzi kwa kuwa na utu na moyo wa kujari mstakabari wa watoto wetu,natamani hata huku kwangu mkurugenzi atoe tamko la kulazimisha mtoto wa fomu one asome masomo yote hadi afike kidato cha tatu ndo aamue aelekee wapi.
Wewe mwalimu mzembe huna utu Wala moyo wa huruma ndo maana unamlalamikia mkurugenzi, binafsi kama mdau na mwalimu nampongeza sana DED kwa uamuzi mzuri, mungu ambariki kwa kujari masrahi ya watoto wetu.