Wilaya ya Tarime ilikuwa mji wa roho mkononi

Wilaya ya Tarime ilikuwa mji wa roho mkononi

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
2010 kurudi nyuma tarime ilikuwa uwanja wa vita.

Sio majambazi,
Sio vita vya koo,
Sio vikundi vya magenge,
Sio vikundi vya wizi wa ng'ombe,
Sio matukio ya kuachiana hospitali au mochwari.

Kuna serial killers walioibuka wakati tofauti, wakawa wanakawa wanatembea na bunduki na wanakuuliza hiki ni nini? Ukisema bunduki, basi akafyatua risasi. Walifanikiwa kuuliwa baada ya kuuwa watu wengi

Kuna wakati ule mji kila aliekuwa anaibuka na vipesa kidogo lazima waje wamteke nyumbani, ilikuwa haipiti miezi kadhaa kusikika sauti za risasi na vilio vya "UWIIIIIIIIII" vya wakina mama kuwa wamevamiwa.

Hii ilijenga watu kuwa na roho kuntu, sio wakina baba au wakina mama, vijana walikuwa tayari kupigwa risasi waingie mgodoni wafukue mabaki ya dhahabu kwenye udongo na kama ulipata chochote kitu na hawakujui katika circle yao lazima waibuke na wewe.

Vijana walikuwa tayari kufa kuvuka boda kwenda kupiga matukio kenya au ku-deal na mazaga zaga.

Koo zilipigana sana, watu walikatana mapanga utafikiri nyama za buchani, kuna wakati ITV walirusha habari jamaaa alikuwa amepigwa mshale wa tako na anapelekwa hospitali.

wanawake walipigwa na wanaume zao na kubaki na makovu, watu kadhaa walioonekana kama ni ma-spy waliuliwa katika mji ule.

Tarime was tarime, then. Nina uhakika wakazi wa tarime walio in 30s+ watakubaliana na maandishi haya.
 
Wanyanchariiii na wanyanchokaaa 😊😊😊

Aliishia wapi mwamba. Na alikuwa akifanya nini
Inasemekana walimuua watu wa mifumo.alikamatwa mkoani tanga akijaribu kutoroka then wakamleta had tarime wakamdunga "mambo fulani" akakata moto
 
Kuna serial killers walioibuka wakati tofauti, wakawa wanakawa wanatembea na bunduki na wanakuuliza hiki ni nini? Ukisema bunduki, basi akafyatua risasi. Walifanikiwa kuuliwa baada ya kuuwa watu wengi
Huyu jamaa alikuwa analipiza Kisasi. Baada ya kukamatwa alisema yote. Enzi hizo alikuwa anawauliza watu kwa kilugha (Keno nki) "Hiki nini"?

Baada ya kanda maalumu kuhamia nadhani ni Rebu pale na kuongezwa kwa jeshi kule Nyandoto ilipunguza Sana haya matukio
 
Kuna miji ya ajabu sana, badala ya kupambania maendeleo wanapambana wao kwa wao, ndio sababu mkoa wa Mara umechoka sana, mkoa una mbuga, madini, ziwa, mpaka wa Kenya, lakini maendeleo ni zero, huo muda waliokuwa wanatumia kuumizanza wangetumia kujielimisha kusimaia rasilimali za mkoa wangekuwa mbali.
 
Aisee! Mnatuchafulia tarime yetu! Hivi nyuma ya mwaka 2010 ni wapi palikuwa hakuna matukio mabayamabaya?
 
Sijui huyu mwamba alikuwa anataka nini
Stori za kwa nini alikuwa akifanya hivyo ni nyingi sana ila ambayo inasemwa semwa na wengi ni kwamba alicheza dili fulan na ma babylon wa tarime ambalo hilo dili lilipelekea yeye akamatwe na kufungwa ila hao mababilon wakamuahidi,kuwa asiwe na wasi wasi aende jela atumikie kifungo then watapigana wamtoe but pia watajenga nyumba ya mama yake ambayo ilikiwa ni mbavu za mbwa tu.mwamba akakubali kufungwa ila alipoingia hawakutimiza ahadi,hawakumtoa jela lakin cha zaidi hawakumsaidia mzazi wake kuweka maisha yake sawa ikiwemo hilo la kumjengea,kifungo kilipoisha mwamba alitoka akakuta jamaa ni mabilionea na wanakula maisha na hawana habari na makubaliano waliyoingia,akawafata na kuwataka wampe mzigo kidogo wakiokubaliana na kuhakikisha wanamfanyia bi mkubwa wake yale waliyopatana,mababilon wakaona kama mwamba hana mwelekeo na hana raman wakawa wanamzungusha zungusha bas akaweka kinyongo akaua wote ambao kwa namna moja au nyingine walikuwepo kwenye ile chain ya lile dili.inasemakana mmoja wao ni yule mfanyabiashara mwenye hotel iliyo mbele ya blue sky(nimeisahau jina) ,hotel hii kwa sasa inamilikiwa na mke wa marehemu na wameifanyia marekebisho makubwa tu.in short jamaa aliuwa kat ya watu 8 jad 13 ambao alikuwa na visasi nao aidha katika hyi dili niliyosema au visasi vingine amavyojua yeye
 
Kuna miji ya ajabu sana, badala ya kupambania maendeleo wanapambana wao kwa wao, ndio sababu mkoa wa Mara umechoka sana, mkoa una mbuga, ziwa, mpaka wa Kenya, lakini hovyo kabisa.
we jamaa una chuki zako binafsi. Hivi hapa tanzania kuna sehemu haina raslimali? Mbona bado maisha ya wananchi ni hoi? We jamaa wewe! Haya bhana!
 
A
Aisee! Mnatuchafulia tarime yetu! Hivi nyuma ya mwaka 2010 ni wapi palikuwa hakuna matukio mabayamabaya? acheni us***e!
Arusha na dar es salaaam kuna matukio ya ajabu sana na ya kikatili mno ila sijui kwa nin tarime ndo inaonewa zaidi🤔🤔🤣
 
Kule Ronsoti makaburini niliona fuvu la mtu, sijui hakuzikwa vizuri yule!!!

Ule mji ilikuwa ikifika tu saa moja jioni watu wote mjini wanarudi makwao, tulikuwa tunakunywa bia pale J.J na Criss Pub, ndiyo ilikuwa maeneo ya kujidai. Around 2012

Kama we ni mgeni ukichukua demu pale jamaa wanakuangalia kwa roho mbaya sana.
 
Ndio maana kukawa na kanda maalum.Ujinga wa watu wa kule mtu anakuwa mwizi lakini maendeleo hakuna sababu na shule nayo hakuna.
Mtu anakuwa mwizi wa ng'ombe akiwa mzee nguvu zikiisha anakuwa korokoroni
Wezi wa mikoa ya kaskazini akitajirika anafungua duka kubwa au hotel au biashara kubwa kisha anakuwa mzee wa Kanisa.
Mji wa Tarime huwezi kuta duka la Mhindi na mgeni na ndio maana hakuna maendeleo
 
we jamaa una chuki zako binafsi. Hivi hapa tanzania kuna sehemu haina raslimali? Mbona bado maisha ya wananchi ni hoi? We jamaa wewe! Haya bhana!
Mkuu nimewahi kwenda Mara ni mkoa uliochoka sana, ni mkoa wenye stendi mbovu zaidi nchi nzima, hivi ile stendi ya Bweri ni maegesho ya magari au ? mkoa una mbuga ya Serengeti lakini wazawa wamelala sana hawataki kujielimisha mambo ya tourism mbuga iwanufaishe, wanaonufaika ni watu wa nje, pale Musoma Mjini pamepoa sana, Mkoa mzima hauna hata chuo chochote wala campus ya maana zaidi ya hicho chuo kipya kinachojengwa tangu enzi za Kikwete. Wabunge mnaoweka hawana elimu mpaka serikali imeamua kuingilia kidogo kuwaondoa wabunge wa darasa la saba kuweka wenye degree na masters angalau mkoa uongeze wabunge wenye sifa za kuwa mawaziri.
 
Kule Ronsoti makaburini niliona fuvu la mtu, sijui hakuzikwa vizuri yule!!!

Ule mji ilikuwa ikifika tu saa moja jioni watu wote mjini wanarudi makwao, tulikuwa tunakunywa bia pale J.J na Criss Pub, ndiyo ilikuwa maeneo ya kujidai. Around 2012

Kama we ni mgeni ukichukua demu pale jamaa wanakuangalia kwa roho mbaya sana.
sasa huyu pimbi mlevi nae anajaribu kusema nini?
 
Back
Top Bottom