Pre GE2025 Wilbroad Slaa: Hata CCM wanasema kuhusu No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona kilichofanyika Dodoma, wamevunja sheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Kumbe kuna watu uko CCM na wenyewe wanapendezwa na hii agenda ya CHADEMA ya No Reforms No Elections?

Akiwa anazungumza leo kwenye ukumbi wa Mlimani City wakati yuko kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Dkt Slaa amesema kuwa kuna baadhi ya watu CCM wanaunga agenda ya CHADEMA ya No Reforms No Elections akidokeza kuwa hata namna CCM walivyopitisha mgombea wao kwenye Uchaguzi hii haijakaa sawa kisheria

"Hata CCM wanasema No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona ngoma iliyofanyika Dodoma, waliofanya wakati wanatetea wanaogombea. Kwanza wamevunja sheria. Wameanza Uchaguzi wa mapema kinyume na sheria alafu sisi wanatuambia tuko nje ya sheria"

Your browser is not able to display this video.
 
"No Reform, No Election" ilipaswa kuwa ajenda ya kitaifa; na kiukweli ina manufaa zaidi kwa CCM kuliko hata CHADEMA. Ni vile tu hawataki kufungua jicho la tatu..!
 
Huyu mzee anaendeshwa zaidi na hisia,aidha ni mwota njozi, ccm haikuvunja sheria kwa sababu, halmashauri kuu ilikuwa pale na kamati kuu,ingelikuwa mh. Samia angejifanyia yeye binafsi bila ya uwepo wa muhimili hiyo ingelalamikiwa!
 
Kwamba hatujui ukweli wa kilichofanyika huko Dodoma? Au kwakuwa huko ccm ni jinai kwenda kinyume na matakwa ya mwenyekiti?
 
Kweli lakini aiseeπŸ˜…πŸ˜…
 
Huyu mzee anaendeshwa zaidi na hisia,aidha ni mwota njozi, ccm haikuvunja sheria kwa sababu, halmashauri kuu ilikuwa pale na kamati kuu,ingelikuwa mh. Samia angejifanyia yeye binafsi bila ya uwepo wa muhimili hiyo ingelalamikiwa!
Unajua maana ya katiba
 
Watakuwa ni CCM Ufipa wale dizaini ya Mpina πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/reel/DG8En0BMuj0/?igsh=aHF0eGoyMDdxcHp6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…