Pre GE2025 Wilbroad Slaa: Hata CCM wanasema kuhusu No Reforms No Election kazaneni hapo hapo. Mliona kilichofanyika Dodoma, wamevunja sheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Slaa hana jipya .CHADEMA Haina mvuto
 
Dingi anapuuzwa sijaona akipewa attention kubwa licha ya kuwekwa sero n.k.
He is trying to be relevance but mhh. Haaminiki.
 
Huyu mzee anaendeshwa zaidi na hisia,aidha ni mwota njozi, ccm haikuvunja sheria kwa sababu, halmashauri kuu ilikuwa pale na kamati kuu,ingelikuwa mh. Samia angejifanyia yeye binafsi bila ya uwepo wa muhimili hiyo ingelalamikiwa!
Halmashauri kuu ndio nn ww popoma chama kilivunja kanuni full stop
 
Tindo
Mambo ndo kama hayo .....watajitokeza wengi tu acha watu wachekeche
 
Samia anazidi kulipigilia misumari jeneza la CCM mazishi yanakuja.
 
"No Reform, No Election" ilipaswa kuwa ajenda ya kitaifa; na kiukweli ina manufaa zaidi kwa CCM kuliko hata CHADEMA. Ni vile tu hawataki kufungua jicho la tatu..!
Mkuu, nadhani wanawake wange ipigia sana hii NO R, NO E, ukizingatia kwamba kwenye Rasimu ya Mapendekezo ya Katiba ya Mzee Warioba, ilipendekeza kwamba katika kila jimbo kuwe na wabunge 2, kwa maana ya KE na ME. KE washindane kivyao na ME nao kivyao na hatimaye kupata hao Wabunge 2 ndani ya Jimbo na hatimaye Bunge kuwa na uwiano wa kijinsia
 
Rasimu ya Mapendekezo ya Katiba ya Mzee Warioba, ilipendekeza kwamba katika kila jimbo kuwe na wabunge 2, kwa maana ya KE na ME.
Kifungu cha ovyo sana kwenye ile rasimu.
 
Je Ndio mkakati wa Chadema kuhakikisha CCM inabaki madalakani!?

Nchi itahitaji Rais atapigwa miaka 5 mingine bila uchaguzii🐔🐔🐔
 
Ndugu najua umeandika kwa kuchanganyikiwa iko hivi.
Ccm inamsimamisha uraisi bara dr. samia suluhu hassan.
Na kule zanzibar ni mh. Mwinyi.

Na si hivyo tu. Uchaguzi upo, ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi aliye juu ya miaka kumi na nane.
Na atayeshinda ni CCM chini ya samia na mwinyi ,bara na zanzibar respectively, Washiriki uchaguzi, na hata wasiposhirika hao wapinzani. Ccm itashinda tu. Tena mapema.
 
Hatukatai CCM kushinda

Hata akichukua urais na majimbo yote ya ubunge ni sawa ila tunachohitaji nikuwepo kwa uchaguzi wa haki na uhuru unaosimamiwa na tume huru na sio bao la mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…