theory of population and ageing nazipenda sana namba huwa hazidanganyi ishi utakavyoishi weka matozo unavyoweza waambie watakula nyasi waambie watalima kwa meno waite farasi na wewe ndo chama umeshika hatamu unawanyoosha waite raia wana akili za kawaida waambie asietaka tozo ahamie Burundi waite kichwa cha mwendawazimu wewe ni waziri kwamisha bwawa lao la umeme waambie raia wanaolala njaa kuwa hivi ni vijisenti tu sijui pesa ya mboga watukane raia unavyoweza ila uzee upo unakuja mdogo mdogo na vigogo wote tutaenda nao tu na mashangingi yao yale ambayo ni kodi za wanyonge watayaacha yamepaki uani!!
wakiifisadi nchi waacheni tu kaburi ndo kiboko ya kila mmoja wetu!! yatapukutika yote in 20 years Allahu Aaalam maana mengi maviongozi ni mazee vijana hawana ajira wala ofisi
Umeandika Kwa hasira sana kiasi kwamba umeingiza feelings and emotions zaidi,but you touched the facts mkuu.
Kwa mtazamo wangu ni kuwa,hii dunia ya tatu au hizi nchi masikini Hawa wakubwa wanapata Mali Kwa ufisadi mwingi sana,sio Kwa ku crack mind zao na kuleta real solutions katika jamii zao.
Sasa kikawaida Kabisa Kama unakula bila jasho na jasho halitoki hiyo ni TOXIC.
Watu wengi hilo hawalijui,wewe angalia hata Dr,PhD holders wa nchi za kiafrika na hususani hapa nchini kwetu,wakipata nafasi tu ambazo ni nyeti ndani ya muda mfupi tu wanakuwa wa duara,wanakuwa shapeless wananenepa Ile mbaya bila Kujua hali hiyo ni magonjwa.
Kifupi lifestyle ya uchovu na uvivu ndio shida plus mindset ya ulafi ndio Kabisa.
Mtu anakuwa kiongozi lakini hata kuandika vitabu haandiki ili kuacha legacy utaachaje kukaribisha toxic kwenye mwili wako na mindset yako?
Mtu umepata Mali za kifisadi utaachaje kuwa mvivu Kwa sababu most of the things you do are shortcuts sio real solutions to the community.
Na wengi Kwa kuwa wanatoka familia fukara zaidi basi matokeo yake ndio hayo.
Nasema hivi sio kuwa hatufi,hapana wote tutakufa lakini Kuna tofauti kati ya mwenye nafasi kimaisha na asiye na nafasi kimaisha.
Kwa wenzetu specifically Japan,78 years ni umri wa kati tu.
Yule Shizo Abe waziri mkuu wa zamani aliyepigwa risasi just imagine mama yake mzazi yupo hai na yuko fresh tu.
Hiyo yote ni lifestyle Yao na mindset Yao Iko vizuri sana sio kama sisi kwenye jamiii yetu.
Sisi huku mtu anaweza akakaa na malaria bila kutibiwa hata mwezi na anaona ufahari tu kuwa yuko ngangari lakini Kwa undani Kabisa ni anajiua taratibu.
Mtu anakaa na njaa kutwa nzima na anaona sawa tu kama kaujanja Fulani hivi kumbe ndio unajiondoa taratibu.
Mtu ana sex mara nyingi zaidi ya anavyokula au zaidi ya protein input yake na anaona sawa tu.
Mtu anakunywa pombe na kula hovyo tena bila mazoezi anaona sawa tu.
Sasa hayo yote ujanani yanawezekana lakini huko uzeeni kuanzia miaka 45 na kuendelea shida zinaanza.
Ndio maana hizi nchi zetu ni kawaida sana watu kulamba Lolo kati ya miaka 50 na 70 hapa.
Kwa wenzetu sio rahisi Sana,hata Kwa baadhi ya jamii hapa hapa kwetu sio rahisi Sana kutokana na lifestyle na mindset zao.
Mfano jamii za wamasai Wanatoboa 95 plus hata jamii za watu wa kanda ya ziwa.