Uchaguzi 2020 William Ngeleja: Hamis Tabasamu aligawa rushwa ya Tsh. 100,000 kwa wajumbe ili achaguliwe

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Kuna barua inazunguka inayoonesha kuwa ni ya William Ngeleja aliyekuwa mbunge wa Sengerema akilalamikia zoezi la kura za maoni jimbo la Sengerema.

Katika barua hiyo Ngeleja analalamika kuwa mgombea na mfanyabiashara Hamis Tabasamu aliyeshika namba moja kwenye mchakato huo wa kura za maoni aligawa rushwa ya laki moja moja kwa wajumbe ili achaguliwe kwenye mchakato huo.

Kama hiyo barua ni ya kweli basi CCM inanuka kwa rushwa.
 
Mh. Ngeleja anaanza kutapata kwani anajua kwa CCM hii hana chake. Hata angepata kura nyingi (kwani kwenye kura za maoni, kimsingi hakuna mshindi bali mwenye kura nyingi, huu ni mwanzo tu wa mchakato mrefu) kuliko watia nia wengine, jina lake halirudi this time, CCM imechoka kulea uozo, mafisadi na watoa/wala rushwa.
 
Mods wekeni hii barua
IMG_20200801_150756_669.JPG
IMG_20200801_150733_730.JPG
 
Kuna barua inazunguka inayoonesha kuwa ni ya William Ngeleja aliyekuwa mbunge wa Sengerema akilalamikia zoezi la kura za maoni jimbo la Sengerema.

Katika barua hiyo Ngeleja analalamika kuwa mgombea na mfanyabiashara Hamis Tabasamu aliyeshika namba moja kwenye mchakato huo wa kura za maoni aligawa rushwa ya laki moja moja kwa wajumbe ili achaguliwe kwenye mchakato huo.

Kama hiyo barua ni ya kweli basi CCM inanuka kwa rushwa.

Ngeleja aache Nongwa......Yeye badala ya kutoa 200,000 alikataa akatoa 50,000 na Maji sijui, Mwenzake Ka-Mtaimu akatoa 100,000.
 
Mmoja ametoa rushwa kubwa kuliko mwingine. Ila, wote walitoa rushwa.
Tabasamu alitoa laki kwa kila mjumbe, Ngeleja akatoa elfu 30 kwa kila mjumbe. Wajumbe wakaona hizi ni dharau yaani rushwa ya elfu 30 iliyokuwa inatumika 2015 bado unataka kuitumia 2020, wakapiga chini Ngeleja.

Ngeleja atafute kazi nyingine, uzuri bosi wake Rostam Aziz amerudi kwenye system.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]hakuzingatia mfumuko wa bei

Sent from my CAM-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom