Uchaguzi 2020 William Ngeleja: Hamis Tabasamu aligawa rushwa ya Tsh. 100,000 kwa wajumbe ili achaguliwe

Uchaguzi 2020 William Ngeleja: Hamis Tabasamu aligawa rushwa ya Tsh. 100,000 kwa wajumbe ili achaguliwe

Ngeleja atulie.....hata kama kazidiwa kete......pia itategemea baba kaamkaje.....yeye na Tabasamu wanaweza pia wasipite.....
Kwanza hachoki......?.....apishe na wengine waongoze bana......
Ningekuwa Magu natupilia mbali hizo kura za maoni bali naangalia CV ya mtu.
 
Mh. Ngeleja anaanza kutapata kwani anajua kwa CCM hii hana chake. Hata angepata kura nyingi (kwani kwenye kura za maoni, kimsingi hakuna mshindi bali mwenye kura nyingi, huu ni mwanzo tu wa mchakato mrefu) kuliko watia nia wengine, jina lake halirudi this time, CCM imechoka kulea uozo, mafisadi na watoa/wala rushwa.
Nitajie asiye fisadi ccm.
 
Hata hivyo Ngeleja hawaelewani na mkubwa wa kaya maana mbili 15 alikuwa team Ma'nvi sasa mkulu hapendi dharau na pale
Sengerema si ana watu wake...
 
Kwelj shetanj akizeeka anakuwa malaika. Leo Ngeleja nae analalamikia rushwa😀😀
 
Si angepeleka tuhuma takukuru mapema? Anasubiri abwagwe ndio apeleke?
 
Ngeleja na ww bana hebu acha kulialia...zile za mgawo wa mboga ww ushaziswallow zote?? Sasa si unatoa na ww kidogo kwa wajumbe!!
 
Huyu anajisahau wakati ule alipokea pesa ya Rugemalila kiliposanuka akakimbiliaa kuirudisha leo anajifanya anachukia rushwa
 
Kuna barua inazunguka inayoonesha kuwa ni ya William Ngeleja aliyekuwa mbunge wa Sengerema akilalamikia zoezi la kura za maoni jimbo la Sengerema.

Katika barua hiyo Ngeleja analalamika kuwa mgombea na mfanyabiashara Hamis Tabasamu aliyeshika namba moja kwenye mchakato huo wa kura za maoni aligawa rushwa ya laki moja moja kwa wajumbe ili achaguliwe kwenye mchakato huo.

Kama hiyo barua ni ya kweli basi CCM inanuka kwa rushwa.
Hata ngeleja huenda alitoa rushwa , sema yeye hakuweka package nzuri
 
Kuna barua inazunguka inayoonesha kuwa ni ya William Ngeleja aliyekuwa mbunge wa Sengerema akilalamikia zoezi la kura za maoni jimbo la Sengerema.

Katika barua hiyo Ngeleja analalamika kuwa mgombea na mfanyabiashara Hamis Tabasamu aliyeshika namba moja kwenye mchakato huo wa kura za maoni aligawa rushwa ya laki moja moja kwa wajumbe ili achaguliwe kwenye mchakato huo.

Kama hiyo barua ni ya kweli basi CCM inanuka kwa rushwa.
ulitakiwa ujihakikishie kama ni kweli ama lah ndo uje kupost
 
Back
Top Bottom