SI KWELI William Rutto, ahudhuria mazishi ya kifo cha Rigath Gachagua

SI KWELI William Rutto, ahudhuria mazishi ya kifo cha Rigath Gachagua

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
SAMIA PICHA.jpg
 
Tunachokijua
Samia Suluhu Hassan ni mwanasiasa wa Tanzania ambaye kwa sasa anahudumu kama Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. William Samoei Ruto Ni rais wa tano na wa sasa wa Jamhuri ya Kenya, akiwa ameingia madarakani tarehe 13 Septemba 2022 kwa upande mwingine Donald trump yeye ni rais wa 45 na 47 wa marekani

Madai

Kumekuwepo na picha inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, ikidaiwa kuwaonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Marekani, Donald Trump, na Rais wa Kenya, William Ruto, wakiwa katika hafla inayodaiwa kuwa ya kuomboleza mwili wa aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

Picha hiyo imesambazwa ikihusishwa na hali ya kisiasa nchini Kenya.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kidijitali umebaini kuwa picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde hivyo inathibitisha kuwa picha hiyo sio halisi na haijatokana tukio linalodaiwa kutokea nchini kenya

Aidha, hakuna ushahidi wa kuaminika uliowasilishwa kuthibitisha madai kwamba Rigathi Gachagua amefariki dunia au kwamba hafla hiyo ya kuomboleza mwili wake imefanyika.
Back
Top Bottom