Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Peter Slaa akizungumza hivi karibuni kupitia jukwaa la Kumekucha la mtandao wa Clubhouse.
"Mimi kwa maoni yangu Tundu Lissu (Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA bara) anachopigania ni kukisaficha chama (CHADEMA) na kukipeleka kwenye hatua ya mbele na ndiyo maana ametoa sera yake na ilani yake ya uchaguzi, kwasababu alichotangaza ni kwanini ametaka kuingia kwenye uongozi (Kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa) na akipata uongozi anaogombea atafanya nini.
Ninadhani aliorodhesha dosari kadhaa ndani ya chama ikiwa ni pamoja na uwezekano wa rushwa ndani ya chama, rushwa ndani ya chaguzi za chama, yeye akaeleza kwamba akichaguliwa atafanyia kazi hayo mambo.
Ikumbukwe kwenye katiba ya CHADEMA ya sasa, haizungumzii majukumu ya Makamu Mwenyekiti, haimpi nafasi ukiachana na wajibu wa Makamu Mwenyekiti kama Mwenyekiti wa maadili pale ambapo jambo linapelekwa kwake, haimpi hiyo nafasi yoyote ya kurekebisha jambo lolote isipokuwa lile lililokabdhiwa kwake na Mwenyekiti au lalamiko lililopelekwa kwake na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama.
Kwahiyo yeye Lissu anatumia mambo hayo kama nyenzo ya kampeni yake kwamba nikiingia kwenye uongozi haya ndiyo nitakayoyafanya kuimarisha chama chetu.
Sasa masuala ya kama yameshatokea mazingira ya rushwa ndani ya CHADEMA, ninadhani Lissu ameyaweka wazi"