Willy Gamba, Hofu, Njama, na E MUSIBA, Mnakumbuka Enzi Hizo?

Hivi Mbuzi Mzee ni kiherehere gani kilikupata ukaanza kutuwekea hii riwaya ilihali hukuwa na uwezo wa kuiweka mpaka mwisho wake?
 
haiendelei?

Nadhani kwa wanaosoma huu uzi kwa mara ya kwanza.., wangewekea Note hapo juu "Pitio la Nusu Kitabu cha Kufa na Kupona...," ili wajue wanachopata ni nusu kitabu na sio kitabu chote
 
Mungu mkubwa JF ni zaidi ya yote machozi yananitoka kila ninapomkukumbuka mzee Musiba sijui kwa nini alikufa mapema !!!!! ah jamani kweli kazi ya Mungu haina makosa nikupitia vitabu vyake pamoja na kile cha 90 minutes at Entebe nilijikuta nakuwa mcheza karate mzuri sana kiasi mpaka leo naweza kumkabili mtu yeyote anayetishia usalama wangu R.I.P. Mzee MUSIBA WASOMAJI WAKO TUTAKUKUMBUKA DAIMA. Mleta mada chapisha vitabu vingine viingie sokoni na kama utataka nitafute tutengeneze sinema ya hivi vitabu japo nimezeeka mkono bado natembeza.
 

Mkuu haya uliyoyaweka kwenye hii paragraph yako ni kweli ?, ulijua karate kwa kusoma hivi vitabu ?

By the way kabla hujatoa asante nyingi za kutosha, ni kwamba hii ni "Pitio la Nusu Kitabu cha Kufa na Kupona" Kwahio ujue kabisa unapata nusu hadithi na sio kitu kamili
 

Kaka naona sijaeleweka vizuri vitabu hivi vilinihamasisha sana kupenda mchezo huo kwani kila nikenda mazoezini sikuwa nachoka haraka kwakuwa nilitamani kuwa kama Willy Gamba na ilifika nikawa najiita mimi ni Willy Gamba wa Kikosi cha Kisasi na siyo kwenye vitabu hivyo kuna mafunzo ya karate
 
Mbuzi Mzee ungefanya ustaarabu sana kama ungekuja hapa na kutuambia...mwisho wako wewe ni hapa ulipoishia!haipendezi mkuu,kwa wewe na heshima uliyojijengea humu jukwaan plus ukongwe ufanye mambo nusu nusu na usiwataarifu raia wanaokuita kila saa!
Just this time b gentlemen na kutuambia hatima ya hichi ulichokianzisha!
Thank you kaka!
 
Last edited by a moderator:
Nahisi wanafamilia wa mwandishi wamemjia juu wakitaka haki miliki izingatiwe,ama ni POLICCM wamekudaka kwa kuandaa DVD ya uchochezi?
 
Ebana wakuu hivi vitabu bado vinapatikana huko bongo? swali la pili, kwa miaka ya sasa kuna waandishi(watunzi) wa riwaya kama waliokuwepo miaka ya zamani 70,80, na 90? Primary na sekondari nilikuwa mpenzi mkubwa wa riwaya za kipelelezi, kipolis hasa za Willy Gamba na Joramu Kiango. Sidhani miaka ya sasa kama kuna watunzi wanaowafikia hawa. Watanzania wa sasa sidhani kama tuna appreciate fani ya kujisomea kama miaka ya zamani.
 
Jamani wapi vile
Salam toka kuzimu
Malaika wa Shetani
Tumerudi na roho zetu
Roho Mkononi
NK NK
 

Mkuu ni PM hii chakula na ingine kama iko. Mungu akuzidishie.
 
Your literature's inspired me to what i am , thank you Sir,
 
Hofu, Njama, niliwahi visoma hivyo vitabu. Nikivipata tena sitaacha kuvisoma kwa kweli.
 
Kikosi cha kisasi pia . Unaweza ku feel kuwa Willy Gamba ni mwanadamu halisi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…