DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu, Wilson Mahera, ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Butiama, akimshinda mbunge aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini.
Katika mchuano huo uliohusisha watia nia watano waliopitishwa na chama hicho, Mahera ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ameongoza kwa kishindo kwa kupata kura 4,295, dhidi ya kura 2,341 alizopata Sagini. Jumla ya kura zilizopigwa katika jimbo hilo ni 8,844, ambapo kura 105 ziliharibika na kura halali zilikuwa 8,739.