Eti Hawa wahuni ndio mpinzani anategemea wakutangaze mshindi!Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu, Wilson Mahera, ameibuka mshindi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Butiama, akimshinda mbunge aliyekuwa akitetea nafasi hiyo, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini.
Katika mchuano huo uliohusisha watia nia watano waliopitishwa na chama hicho, Mahera ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ameongoza kwa kishindo kwa kupata kura 4,295, dhidi ya kura 2,341 alizopata Sagini. Jumla ya kura zilizopigwa katika jimbo hilo ni 8,844, ambapo kura 105 ziliharibika na kura halali zilikuwa 8,739.
Umesema ukweli sana! Ana roho mbaya sana! Alipokuwa tamisemi ameharibu na Kila hela nyingi sana za shule inayoitwa Arusha Primary School (Arusha School). Aliihamishia tamisemi kinyume Cha Sheria wakati ilikuwa wizara ya elimu kwa Sheria ya bunge! Hakuipeleka bungeni ijadiliwe akafanya kihuni ili aitafune viziri!Ilikua ni rahisi Ngamia kupenya TUNDU la Sindano Lakini sio Kwa SAGINI, MTU MWENYE ROHO MBAYA, MBINAFSI .
Kwanini mkuu?ni swala la aibu kwa chama changu na serikali yangu na yeye mwenyewe Mahera
Kama umekua mkurugenzi wa TUME ya UCHAGUZI ambayo tunawaambia watanzania kuwa TUME HURU YA UCHAGUZI,kumbe ni mwana CCM haiKwanini mkuu?