Naona NEC wamebanwa vilivyo na sasa wanajiandaa kuuweka mpira kwapani
Tuliwaambia tangu awali mwaka huu mtoto hatumwi dukani na hakuna njama mtakayopanga ambayo haitawekwa wazi.
Mmeengua wagombea wa upinzani, mkafanya kurudisha baadhi na bado hamkuwapa barua, mmefungia wagombea wa upinzani kufanya kampeni, mkakataa kuwaapisha mawakala wa upinzani na mbaya zaidi baada ya mbinu zenu za hovyo za kuongeza vituo vya kupiga kura na wapiga kura hewa kubumbuliwa mnajifanya mnajikosha kuwa ni njama za wapinzani kuwachafua.
Niwaambie tu NEC, hakuna rangi mtaacha ona mwaka huu, hakuna uovu mliopanga ambao haujulikani na hautajulikana. Pona yenu mwaka huu n kuruhusu uchaguzi huru na wa haki tu.
Mmeshikwa vibaya sana mwaka huu na kwamwe hamtoki.
Tanzania imeshaamua ni Tundu Antiphas Lissu na Maalim Seif tu!!