Uchaguzi 2020 Wilson Mahera: Kuna Viongozi wa Vyama vya siasa ambao wamejipanga kuharibu Taswira ya Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Wilson Mahera: Kuna Viongozi wa Vyama vya siasa ambao wamejipanga kuharibu Taswira ya Uchaguzi Mkuu 2020

Kila siku anajitokeza kuongea upuuzi tu, anaendelea kujidanganya na hayo matamko yake yasiyo na maana kila wakati, watanzania wa leo hawadanganyiki tena.

Anyway, naona Congress ya Marekani wameshamuandikia Magufuli barua nyingine kumkumbusha kulinda haki za raia, huyo Mahera muacheni aendelee kutapika tu.

Kamanda ni wapi kajibu upuuzi? Mbona kajibu uzushi wenu?
 
Huyu mpuuzi Sana, anajua Watanzania Ni wajinga Sana? Siku zake zinahesabika
 
Mpaka sasa Tume yetu ya uchaguzi iko vizuri sana! tangu nianze kupoga Kura sijawahi kuona tume imejiandaa vizuri kama mwaka huu 2020!
hongera kwa tume kuweni imara msitetereke, Tume ikikubali kutetereshwe mtasababisha matatizo makubwa,
 
JK alisema za kuambiwa changanya na za kwako. Mahera kuwa mwangalifu, baadaye utabaki peke yako. Mfano yanayoendela hivi sasa Nigeria ukiacha kauli ya icc, Mike Pompeo nae ametoa kauli anataka uchunguzi ufanyike, sasa mambo yakiharibika hapa Tanzania watendaji wa NEC lazima mtawajibika.
 
Waliongeliwa maana yake walikosa sifa za kisheria katika kuteuliwa up

Umeshambiwa wapinzani wa bongo ni magumashi bado wee inaendelea kuwamini itakula kwako amka nakuona uko usingizini. Kama viongozi wakubwa wachama wanashindwa kuelewana Sasa we unashanga hao wadogo kukosea taratibu za kisheria. CCM chama kubwa wanataratibu za kusimamiana na kuelekezana kwa kila hatua. Mfano tuliona kwenye ujazaji wa form Yani ulikuwa utopolo mtupu utafikiri chama hakina viongozi wa kuwasimamia viongozi wao.
Membe sio kiongozi wa juu wa ACT bali ni mgombea wa urais kupitia ACT.Kaenda juzi ACT. Na hana mvuto wowote. Watu wameamua kuungana na mgombea mwenye mvuto. Kwenye ujazaji wa fomu ni sababu za kipuuzi ndio zilitumika kuwaengua fullstop.
 
Mahera anaua soo baaada ya ushenzi wa tume kuwekwa hadharani. Hicho anachoagizwa kufanya kitampeleka pabaya. Aache mshindi halali apatikane, vinginevyo machafuko yako wazi peupe.

Membe sio kiongozi wa juu wa ACT bali ni mgombea wa urais kupitia ACT.Kaenda juzi ACT. Na hana mvuto wowote. Watu wameamua kuungana na mgombea mwenye mvuto. Kwenye ujazaji wa fomu ni sababu za kipuuzi ndio zilitumika kuwaengua fullstop.
Huo unao uita upuzi ndiyo takwa la kisheria. Kumbuka kila statement ya kisheria unaweza kuathili. Tatizo mnazani Ukiwa Upinzani basi utahurumiwa. Wakati wenzenu wa CCM wanajili makatibu kata wa chama ambao wanajielewa mnawafikiri ni wajinga. Kwa taarifa yenu vyama vyenu ambavyo havina uongozi ulioenea kila kona ya nchi vitaendelea kupigwa bao na CCM mpaka basi.
 
JK alisema za kuambiwa changanya na za kwako. Mahera kuwa mwangalifu, baadaye utabaki peke yako. Mfano yanayoendela hivi sasa Nigeria ukiacha kauli ya icc, Mike Pompeo nae ametoa kauli anataka uchunguzi ufanyike, sasa mambo yakiharibika hapa Tanzania watendaji wa NEC lazima mtawajibika.
Usidanganye watu kijana. Yanayoendelea Nigeria huwezi kuyaletea mfano hapa, vitu viko live kila mtu anaona.
 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles, leo Oktoba 23, 2020 amezungumza na Vyombo vya Habari kutoa rai kwa Watanzania, kuvipuuza vikundi au Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao wamejipanga kuharibu taswira ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.
View attachment 1609827View attachment 1609828View attachment 1609829View attachment 1609830
Hivi Mahera anatuchukuliaje Sisi??Kwani Kwa Uelewa wa Mahera Tume ina Taswira gani mbele ya jamii??

Yani anadhani watu wenye akili timamu wanaona Taswira nzuri Kwa Tume hii inayosimamia na kuhakikisha CCM inashinda Kwa hila?
 
Mkileta uzushi kwa tume Mahela anawabana Mbavu, mkileta uzushi kwa Magufuli Polepole anawana Mbavu mpaka mnashindwa kupumua. CDM mliambiwa mapema moto wa Magufuli unatisha. 2015 jina la Magufuli ndilo lilipatia ushindi mwembamba CCM. Baada ya miaka mitano baada ya kushima nchi amejipambanua zaidi kwa kutimiza zaidi ya asilimia80 ya ahadi za uchaguzi. Sasa usishangazwe na nyomi lake analopata na mahaba anayopewa na Watanzania. Ushindi wake mwaka 2020 utakuwa ni wakimbunga maana siyo kwa mahaba haya.
 
Machafuko yanini bwashee?
embu acheni kufikiria machafuko fikirieni amani kwanza.
twendeni taratibu kama mabadiliko yatakuja na yataletwa na CCM.taratibu tu tutafika bwashee mnapopataka.
Taratibu !? maujinga
 
Huo unao uita upuzi ndiyo takwa la kisheria. Kumbuka kila statement ya kisheria unaweza kuathili. Tatizo mnazani Ukiwa Upinzani basi utahurumiwa. Wakati wenzenu wa CCM wanajili makatibu kata wa chama ambao wanajielewa mnawafikiri ni wajinga. Kwa taarifa yenu vyama vyenu ambavyo havina uongozi ulioenea kila kona ya nchi vitaendelea kupigwa bao na CCM mpaka basi.

Ccm sio chama cha siasa bali ni kikundi cha dola kilichovaa koti la chama cha siasa. Hakuna taasisi yoyote inayoweza kuwachukulia ccm hatua yoyote. Mifano halisi ipo.
 
Najaribu kuwaza, Mahera anafahamu madhara binafsi anayo weza kukumbana nayo ikiwa uchaguzi huu utaharibika?

Anafahamu hatari ya kujikuta maisha yake yaliyobaki kuyamalizia gerezani na kuacha familia yake ikimlilia?

Je, anajua kuwa huyo anayetumia nguvu nyingi kumtengenezea mazingira haramu hatakuwa naye na atamkana kuwa hakumuagiza aliyofanya?

Kweli shetani akikuingia jambo la kwanza anakuvua akili na kukuachia fuvu tupu
Kwa candidates wa The Hague, Mahela yupo kati ya vinara
 
Huku wakiwa wamewaengua mamia ya wagombea wa upinzani na kuwapitisha mamia ya Ccm bila kupingwa!! Mbaya zaidi wakiwa wanafanya figisu za kutowaapisha mawakala wa Chadema.

Anatuona watanzania wajinga sana huyu mzee , sasa tutamuonesha wiki ijayo!!
Hivi Mahera anatuchukuliaje Sisi??Kwani Kwa Uelewa wa Mahera Tume ina Taswira gani mbele ya jamii??

Yani anadhani watu wenye akili timamu wanaona Taswira nzuri Kwa Tume hii inayosimamia na kuhakikisha CCM inashinda Kwa hila?
 
Ccm sio chama cha siasa bali ni kikundi cha dola kilichovaa koti la chama cha siasa. Hakuna taasisi yoyote inayoweza kuwachukulia ccm hatua yoyote. Mifano halisi ipo.
Mshauri Msajili akifute kama unadhani CCM siyo chama Cha siasa.
 
Viongozi wa vyama pinzani wenyenia ovu na uchaguzi huu washafahamika,wakijaribu wanapigwa spana.
Mkuu, we unaunga mkono wizi, ulaghai, utapeli na uharamia wote unaofanywa na ccm na vibaraka wake akina Mahela ?!
 
Mkuu, we unaunga mkono wizi, ulaghai, utapeli na uharamia wote unaofanywa na ccm na vibaraka wake akina Mahela ?!
Acha uzushi weka ushahidi wa uharamia wao ili tukujue kwamba wewe siyo mnafiki, mpayukaji, mchumia tumbo, hopeless. Let's ushahidi.
 
Back
Top Bottom