Tetesi: Wilson Nkambaku anafuata baada ya Nyalandu kuondoka CCM!

Ikumbukwe huyu kijana wa Kinyaturu ndiye aliyerithi mikoba ya Nyalandu kwenye kiti Urais wa UKWATA pale Ilboru Sekondari miaka ya nyuma baada ya kumaliza muda wake.
Correction...
Nimesoma darasa moja na Wilson Elisha Nkhambaku Ilboru na kumaliza wote 1996...Wilson hajawahi kuwa member wala kiongozi wa UKWATA, yeye alikuwa ni mwana-CASFETA(Umoja wa Wanafunzi wa Madhehebu ya Kipentekoste).

Pia Lazaro alikuwa ni Rais wa UKWATA Tanzania, siyo tawi la Ilboru tu.Lazaro ni Mlutheri, Wilson ni Mpentecostal

Mengine inaweza kuwa uko sahihi kiasi, not 100%.
 
Hivi Lowasa alikuja na mafuriko ya watu wangapi?
Kama siyo maigizo!
 
Haya!! yetu macho na masikio. ILA muangalie msije mkafuatwa na ma Nissan Patrol.

Hawapendagi ujinga wakiishiwa cha kukufanya.
 
Hata waleeeee walipoondoka hadithi ni hizo hizo ana watu 100 sijui 200 watamfuata mpaka sasa bado tuko ufukweni mwa bahari tunasubiri jahazi lililobeba hao watu, sasa mmeanza tena haya tunasubiri basi hao wenyeviti na makatibu 100
 
Lowasa alikuja cdm na gad leo iko hivi ilivyo, no new vibration may bring unique impact.
Tusake maisha tutupe siasa pembeni
 
Huyo Kijana kaamua kuukomoa Mkuki kwa kuukalia!
 
singida imenjanjaruka..wanyaturu wameamua..wabaki wale wanafiki wanyiramba.
 
Huyu jamaa alimaliza shule ya msingi mtamaa " ni moja kati ya watu wenye akili sana niliyepata kuwaona lakini baada ya kwenda ilboru sijui kama aliweza kutendea haki ubongo wake maana sikujua alielekea wapi hadi niliposikia yupo kwenye masiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…