Tetesi: Wilson Nkambaku anafuata baada ya Nyalandu kuondoka CCM!

Tetesi: Wilson Nkambaku anafuata baada ya Nyalandu kuondoka CCM!

Correction...
Nimesoma darasa moja na Wilson Elisha Nkhambaku Ilboru na kumaliza wote 1996...Wilson hajawahi kuwa member wala kiongozi wa UKWATA, yeye alikuwa ni mwana-CASFETA(Umoja wa Wanafunzi wa Madhehebu ya Kipentekoste).

Pia Lazaro alikuwa ni Rais wa UKWATA Tanzania, siyo tawi la Ilboru tu.Lazaro ni Mlutheri, Wilson ni Mpentecostal

Mengine inaweza kuwa uko sahihi kiasi, not 100%.
Tupe nondo mkuu, wengine hatuyajui..
 
Anaitwa Wilson Nkambaku, Kwa sasa ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya aliyepangiwa kazi mwaka huu. Alikua mkuu wa wilaya awamu ya nne katika wilaya za Meatu na Arumeru kabla ya kurithiwa na Alexander Mnyeti.

Kwanini anaondoka?

1.Ikumbukwe huyu kijana wa Kinyaturu ndiye aliyerithi mikoba ya Nyalandu kwenye kiti Urais wa UKWATA pale Iiboru Sekondari miaka ya nyuma baada ya kumaliza muda wake.

2. Exposure zake zote nje ya nchi ni sawa na za Mh Nyalandu, alifanikiwa haya yote kupitia kwa kaka yake huyu ambaye ameondoka CCM na kwenda CHADEMA.

3.Alishinda nafasi ya Ubunge kwenye kura za maoni CCM 2010 jimbo la Singida Magharibi, lakini akadhulumiwa kwa fitna na hongo za CCM,alihamia CHADEMA ili kufanikisha mipango yake ambapo aliaminiwa na wananchi wakaahidi kumchagua kwa kura zote lakini baadae aliyekua Rais wakati huo alitumia nguvu nyingi kwa kumtumia Mh Nyalandu kumshawishi asihamie CHADEMA ili jimbo la Singida Magharibi lisiende na maji,ailirudi CCM kwa kushawishiwa na Nyalandu na baadae kupewa ukuu wa Wilaya.

4.Ndiye rafiki mkubwa sana pengine kuliko hata marafiki wengine wa Nyalandu hapa nchini.

5.Hawezi kuiona future yake ya kisiasa kwenye hii CCM iliyojaa visasi iliwa kaka yake ameondoka CCM.

5. Ni kijana mwaminifu na mlokole asiyekua na doa hata kidogo, features zake ni sawa na za Nyalandu.

6. 2020 kijana wa Kinyiramba Elibariki Kingu ajiandae mapema tu kuachia jimbo la watu.Itakua ni Combination ya Tundulu LISSU+Nyalandu kumnadi Nkambaku.


Je,mnafikiri Nyalandu yuko peke yake?
Kuna mengina ndani ya kapu, Lakini kuna tetesi kua Mh Nyalandu ana Marafiki zake Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa sasa wa wilaya na mikoa wasiopungua 100 ambao ndio walikua wapambe zake kwenye kusaka sahihi za kukamilisha mipango ya kugombea Urais 2015 ambao watamfuata muda si mrefu.

CCM nawaasa kaeni mtulie tuu, msianze kuchafua watu wanapoonfoka chamani. Watafteni na hawa 100 kabla hawajaondoka.
Sasa nimejua kwa nini Nyalandu aliongoza maombi ya kumwombea Lissu akiwa Mbeya.. Nafikiri huyo katibu aliratibu
 
singida imenjanjaruka..wanyaturu wameamua..wabaki wale wanafiki wanyiramba.
Sura ya Mwigulu Nchemba inaishara fulani, hata kama sii kwa viwango vya juu sana lakini haungi mkono matumizi ya smg area D.
N.B wanyiramba ni ndugu wa wanyaturu. (futa fikra za kikabila)

Magufuli anaharibu utaifa wetu kwa kuushangaa shangaa urais.
 
5. Ni kijana mwaminifu na mlokole asiyekua na doa hata kidogo, features zake ni sawa na za Nyalandu.

Haya mengine kuyaandika kama vile wewe ni Mola mmmmh

Naona mnaandika tu kutingisha watu wa chama chenu waanze kuwabembeleza.. kama mimi nipo huko nawafurumusha kabisa.
 
Kwa hiyo Wanyaturu wanafanya maamuzi yao kikabila?

For your information Wanyaturu wako wachache sana ni kabila dogo sana ambalo nafikiri hata wasomi wao ni wachache sana.Na kwa sababu ya uchache wao wanahulka ya kusaidiana.

Kumbuka aliyejeruhiwa ni Mnyaturu na amewatetea wanayturu wengi huko kwao.Siwezi kuita UKABILA ila wanajiona kwa uchache wao ni rahisi sana kumalizwa,Ndiyo sababu kuu wanapenda kuwa karibu na kusaidiana.

Sina uhakika kama Mwigulu hata JOIN fungu hili hata kama kwenda ACT Wazalendo
 
Mbona anachelewa?wakitaka na kujitenga Singida iwe nchi wajitenge tu hatuna shida na wanyatutu.
 
Back
Top Bottom