Wimbi la viongozi kwenda Wasafi FM badala ya TBC

Wimbi la viongozi kwenda Wasafi FM badala ya TBC

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
638
Reaction score
1,150
Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la viongozi wa kiserikali kushiriki mahojiano mbalimbali pale Wasafi FM. Yaani ni kama wanapishana vile, ukiangalia namba ya viongozi hawa hawa kwenda TBC FM ni kama haiko kabisa.

Je, huku si kukosa uzalendo?
 
Siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa Sana la viongozi WA kiserikali kushiriki mahojiano mbalimbali pale Wasafi FM. Yaani ni kama wanapishana vile, ukiangalia namba ya viongozi hawa hawa kwenda TBC FM ni kama haiko kabisa. Je huku si kukosa uzalendo?
Apana c kukosa uzalendo ila ni majibu tosha kuwa TBC hakuna mtu anehangaika kuiangalia. yani hawatakiwi
 
Audience, yaani Hadhira inayokusudiwa ukitaka kufikia watu wengi zaidi ni busara kuwaza utawapata wapi.
 
Viongozi wa CCM wameipoteza mvuto TBC, baada ya kuona imedoda sasa wanalazimisha kwenda kwenye nyingine zenye mvuto.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Siku zote vyombo vya habari vya serikali (afrika) huwa havina mvuto kwa wasikilizaji sababu mojawapo ikiwa ni chombo husika kuegemea zaidi kwa anayekipa ruzuku kuliko wanaosababisha kipate ruzuku.

Pili havina uhuru wa kuhabarisha, wanategemea taarifa za mheshimiwa kasema, hii inaleta tofauti kuubwa sana na vyombo vya mabeberu.

Tatu staff wake hawana ubunifu wowote hiyo inachangiwa na kuwa na uhakika wa mshahara na mikopo tofauti na private media.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukienda studio huwa Kuna kifaa kinaonesha namba of viewers/listners kwa wakati ule.

Mfano TBC ukiwakurupusha kabla hawajachakachua utakuta viewers/listners ni elfu tano Tanzania nzima, wakati wasafi unakuta milioni Saba.

Viongozi wanaokwenda kuhojiwa Mara nyingi wanakwenda kuuza sura tu. Hua hawaongei yaliyo mioyoni mwao. Kama yule aliyesema wananchi wameichoka CHADEMA wakati yeye mwenye ubunge kaupata kwa kubebwa na tunakoelekea wizara imeanza kua ngumu kwake.

So wanakwenda kuuza sura kwenye audience kubwa.
 
Hivi inakuaje TV ya mtu binafsi inakua "classic" kuliko TV ya nchi?
Huo ndo msingi wa hoja yangu, TBC inajiendesha Kwa Kodi zetu nini kinasababisha ikose mvuto na kupoteza namba ya wasikilizaji? Tunaanza kufundisha watoto historia ya Tanzania ili wawe wazalendo, Kwa nini hawa viongozi wasiwe wazalendo Kwa kuhakikisha TBC FM inasikilizwa na watanzania walio wengi!
 
Audience, yaani Hadhira inayokusudiwa ukitaka kufikia watu wengi zaidi ni busara kuwaza utawapata wapi .
Unaweza kutupatia Jibu ni kwanini Jibu liwe kwamba Audience inapatikana Wasafi na siyo TBC FM, Kwa nini Wasafi aweze kuvutia hadhira na TBC ashindwe ili hali TBC anajiendesha Kwa Kodi zetu? Wakati Wasafi ni mojawapo ya Wale wanaolipia huduma za TBC
 
Back
Top Bottom