wimbo bora wa injili kwa mwaka 2009

wimbo bora wa injili kwa mwaka 2009

Lazima mkubali kuwa rose muhando hana nyimbo yeyote mbaya.....angeamua kuingiza nyimbo yeyote ingeshinda alafu watu wangelalamika kuwa ameshinda nafasi mbili au tatu!

Lazima tukubali kuwa rose muhando is the best gospel artist of all the time....wanaosema kuwa nyimbo zake zinaimbwa na walevi wanasahAu kuwa hata yesu walimsema kuwa alikuwa anakula na watoza ushuru na malaya....anasema alikuja iili watu wote wapate wokovu ...wote wawe na uzima tena wawe nao tele.....sasa nilidhani wanaompinga rose wangemshukuru kwa kufuata maandiko amefanya hadi walevi ,wapagani na wasiokuwa wakristo walisifu jina kuu kuliko yote ...jina la yesu!....si kazi rahisi ...msimpinge ..mpeni sifa zake stahili na yeye anasema kuwa sifa na utukufu ziende kwa bwana! Mnataka nini zaidi!


Hongera rose muhando!!!!!!!


ANGALIA HAPA

http://www.globalpublisherstz.com/2009/05/07/shusho_mhando_nani_zaidi.html
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=89maW4DxP7k&feature=related[/ame]

Kuhusu kwaya ya AIC nafikiri kwa sababu hili kanisa liko zaidi Mwanza.

Ni sawa ukienda kwenye misa za kanisa la Moravian Church, misa ikiisha utashangaa ni Kinyamwezi na Kinyakyusa tu.

Rose Muhando nyimbo zake kweli zimekaa kimchiriku zaidi. Ni kama Kirk Franklin wa USA ambaye huwa anashusha RAP na heavy Funky kwenye stage/kanisa hadi unaweza ukashangaa. Waimbaji kama hawa huwa ni kivutio kikubwa sana kwa vijana na kuwashawishi waende kanisani.
 
yah yah!
Bukuku anaimba nyimbo kweli unazisikilizia moyoni live, nyimbo zinagusa, nyimbo zinaleta hisia.
rose muhando nyimbo zake ziko kibiashara zaidi, kidunia zaidi.

What do you mean kidunia zaidi? Unaweza kutenganisha roho na mwili wewe au unaongea tu? Huo wimbo unaouita wa kiroho usipokuwa una-sound vizuri nani atausikiliza? Unatakiwa kuimba nyimbo zinazo-sound vizuri na zenye jumbe nzuri na ndicho anachokifanya Rose Mhando and yes, lazima awe kibiashara otherwise mtafutie kazi nyingine ya kujipatia kipato halali. Yeye ni mwanamziki lazima apate kipato kutoka kwenye mziki kama ambavyo mfanya biashara anapata kipato chake kwenye biashara na mchungaji kutoka madhabahuni.
 
kama ilivyo miziki ya kidunia, kila style ya muziki ina wapenzi wake, vivyo hivyo na miziki ya injili kila style ina wapenzi wake na nilazima tukubaliane na ukweli kuwa wapenzi wa style ya ROSE MHANDO ni wengi compared to BAHATI BUKUKU na wenginge wote walishiriki
kipekee nawapa pongezi wote walioshiri kwani hata kuwa katika 30 bora za mwaka ni ushindi, maana nyimbo za injili ni nyingi sana zilizoheat 2009!!!
 
yah yah!
Bukuku anaimba nyimbo kweli unazisikilizia moyoni live, nyimbo zinagusa, nyimbo zinaleta hisia.
rose muhando nyimbo zake ziko kibiashara zaidi, kidunia zaidi.
Sawa, waimbaji wa nyimbo za dini wengi sana wanaimba kibiashara. Hata ukiwaalika kwenye shughuli za kiroho wanataka mapatano kwanza utalipa kiasi gani. Hawamtumikii Mungu ila wanachuma. Lakini Wanachuma kwa kutumia Jina la Mungu, ambaye akijitetea watu hawa wanaanguka vibaya maana viburi vimeshupaa. Watu wengi wanapenda kusikiliza maneno ya Mungu kupitia waimbaji na hivyo kulifanya soko la muziki wa dini kuwa njenje. Wanaofanikiwa kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu hadi rohoni wanamtanguliza Mungu katika uimbaji wao na hawana kiburi. Hata ukiwaita kwenye kazi ya Mungu wako radhi kuja bure au kupata chochote utakachokuwa nacho kwa vile wanajua wanamtumikia Mungu kwa vipaji vyao.

yah yah!
rose muhando nyimbo zake ziko kibiashara zaidi, kidunia zaidi.
Rose Muhando anaimba kwa melody na style ambazo vijana wengi wanapenda kusikia na kuona na kurukaruka. Yupo duniani na wale waliopo duniani ndio watakaokuwa wapenzi wake. Kwa hiyo lazima ziwe za kidunia zaidi. Hata hivyo ujumbe wa Mungu unaenda kuangukia pale penye udongo mzuri. Wapo watu wanapiga nyimbo hizo hata bar na kukatika viuno, wala hawasikilizi maneno ya wimbo na kutafakari, wanafurahia mdundo na melody kwa ujumla. Kama vile wnapiga nyimbo za kibolingo ambazo watu tunazipenda sana hata bila kujua zina maana gani.

Leka
 
Mahali pengine swali liliulizwa, kwa nini kaswida hazikushirikishwa endapo nyimbo za dini tu zilitakiwa? Swali hilo alilijibu vizuri sana Musa mwendeshaji kipindi cha Uswazi. Hawapeleki Kaswida zao TBC zikapambane na nyenzao. Mwakani wapeleke nao zipambane, si zinamtukuza Mungu pia? Kuchaguliwa inategemeana na wangapi wanakukubali kwa kazi yako.

Leka
 
Huo wimbo Nibebe unaimbwa sana kwenya harusi, na watu wanakata viuno utafikiri sio wa dini!! Hata The comed naona wameshaumeza!!
Hata mfalme DAUDI alikuwa akikata viuno wakati akimwimbia mungu. Hata hivyo swala la kukata viuno sio TATIZO la wimbo wa NIBEBE bali la huyo anayekata viuno. Wimbo hauwezi kuacha kuchanguliwa kuwa bora kwa sababu ati ukiimbwa watu wanakata viuno. Kwa ujumla nyimbo zote tatu zilikuwa bora lakini watu 7000 wamechangua wimbo wa NIBEBE wa Rose Muhando kuwa bora zaidi.
 
NAWAPONGEZA TBC kwa kuandaa mashindano ya nyimbo za injili ila siku nyingine wajitahidi sana kuwa na maandalizi mazuri ikiwa ni pamoja na kuwatatafuta watu wenye uelewa wa uchambuzi na ufundi,nilisikitishwa sana na kaka yule ambaye ni mchungaji na ambaye alikuwa mmoja wa wachambuzi alivyoshindwa kuimba vizuri alipopewa nafasi ya kuimba live,ushauri wangu kwamba siku nyingine watafutwe wataalamu wa muziki wenye kulenga kuzungumzia kuhusu fani na wala si maudhui
 
unfortunately sintaweza kuangalia link yako..kwani kwa standard zetu JF ...magazeti ya watu Low kama shigongo ya udaku na mengine ya aina hiyo ...are not prefered reference hapa....
sidhani pia mtu yeyote makini unaweza kumpa taarifa akauliza source ukamuambia ni shigongo style!
tatizo lenu ni kubwa sana watz!
yaani umeenda shule kidoogo unaanza matusi na kashfa!sasa usipoyasoma hayo magazeti utajuaje huo udhaifu wake?
 
sawa ni mzuri na tbc wamefanya kitu kizuri,ila wajithidi wakati mwingine kutafuta wachambuzi wenye ujuzi kuhusu nyimbo za injili.
 
Mimi nilipiga kura kwa wimbo wa MPINGA KRISTO. Nilikatwa Tsh 500/= walipotangaza zawadi nikawa hoi. Kwa kweli wasanii wetu wananyonywa na kila mtu tusiwalaumu waasia peke yao.
 
Tukubali kuwa Rose Mhando ni mwimbaji na mbunifu mzuri wa nyimbo za injili. Rose anajaribu sana kugusa hisia za kila mwanajamii, anajaribu hata kuwavuta wanajamii kupitia nyimbo hizo za hisia. Bahati Bukuku naye ni mtunzi na mwimbaji Bora. Juzi hata quality ya video yake ilikuwa nzuri sana. Wakati natizama niliwaambia niliokuwa nao kuwa kwa quality ya video, she was number one. Na wote walishinda Rose, Solomon na Bukuku were the best choices kwa upande wangu.

Kwa upande wa Global publishers, the Shigongo and its low stuff hawezi kabisa kuandika jambo nimpe credit. Kwanza magazeti yake yanatumiwa na watu kuchafua wengine, kama kuna story za kweli basi ni chache sana. Anapenda hongo na pesa, magazeti yake yanapigia watu simu kuwataka watoe pesa ili wasiandikwe. Anatumia vyombo vyake vya habari vibaya, huku anajifanya ni mlokole.
 
Back
Top Bottom