Wimbo gani ukiusikia unakukumbusha magumu uliyoyapitia?

Wimbo gani ukiusikia unakukumbusha magumu uliyoyapitia?

Acha tu ndugu yangu. Ni nyimbo mchanganyiko ambazo zilikuwa zinanikumbusha jambo flani hivi, .zipo kwenye playlist yangu.
Sasa hivi siwezi tena kusikiliza mziki wowote.
Kiufupi naumwa mwili na roho na sioni matarajio ya kupona.
Update playlist,usiwe mnyonge boss,
 
Nakumbuka nipo Form One wimbo maarufu wa "Fanta Wangu Uliamua" kama sikosei uliimbwa na Orchestra Bima Lee, ukiwa bado ni maarufu, Mzee wangu alipata uhamisho wa kikazi.

Uhamisho huu ulinipelekea kuhamishiwa "boarding" kwani hapo awali nilikuwa bado nasoma "day school" nyakati hizo vijana wa Kidato cha Kwanza tulipitia changamoto nyingi sana hasa kwa wale ambao walioishi bweni.

Tuliitwa kila jina baya, njuka, bazoka, salamander, goromondo, n.k. Nakumbuka nilihamia bweni mwezi Julai, lakini nakumbuka kupitia mimi upuuzi huu wote ulikomeshwa na kufikia ukomo wake. Nilifanikiwa kuwatambua baadhi ya watesi wangu hali iliyopelekea wao kufukuzwa shule moja kwa moja, na hii ikawa ni mwanzo na mwisho kabisa wa kuendekeza ujinga wa kuwahangaisha vijana wadogo wa Kidato cha Kwanza

Kila nikiusia wimbo huu huu ukipigwa, unanilumbusha maisha ya wakati huo nilipo kuwa bado kijana mdogo wa kidato cha kwanza.
 
Aina ya nyimbo gani unapenda ??genre.. unampenda demi Lovato??
 
See, I'm ahead of them, Asiwaju I'm a fucking baller, Ighalo ni mi No man fit talk shit to me Ni ilu mi, you go collect o See, omo na me dey lead, Asiwaju I'm a fucking baller, Ighalo ni mi No man fit talk shit to me Ni ilu mi, you go collect o, ah I'm on a different steeze Singlet, belt and ripped-out jeans Man too wise, I no fit lose that cheese Oluwa thunder my body with blessings Ogbeni! Ogbeni! Leave that thing When I say kuku-ruku, cook that thing Who dey che-, who dey check am, oya look that thing Face white, yansh black, I rebuke that thing Make nobody try stress me, I no be JJC I don't know if you get it, on a top rating, affiliate with the best team You wan race me? We no dey do the same thing, hmm-mm Canoe no be jet ski, omo you say wetin? No go reason me less, omo you go chop craping I do it diligently Won le mi, won le ba mi Man getting high 'til I fade out If the vibe no pure, on my way out Hullabaloo, anytime we step out The men dem
 
Back
Top Bottom