Wimbo gani ukiusikia unakukumbusha magumu uliyoyapitia?

Wimbo gani ukiusikia unakukumbusha magumu uliyoyapitia?

Screenshot_20240608-174530.png

utakumbukwa daima hayati mzee mwinamila wa tabora

Napendaga Sana nyimbo za asili za mzee mwinamila..
 
Acha tu ndugu yangu. Ni nyimbo mchanganyiko ambazo zilikuwa zinanikumbusha jambo flani hivi, .zipo kwenye playlist yangu.
Sasa hivi siwezi tena kusikiliza mziki wowote.
Kiufupi naumwa mwili na roho na sioni matarajio ya kupona.
Muache aende...!😂
 
Fireboy jealous huu wimbo unatoka nilikua juu ya mawe sio poa
 
Mimi kwakweli ile album ya wenge musica bcbg yenye nyimbo kama masuwa, bana lunda, ndombolo n.k ilinikuta katika mapito magumu.

Leo hii nikisikia nyimbo yoyote ya kwenye ile album nakumbuka mbaaali sana napata hisia sana ya hata kutoa machozi.

Mungu wetu ni mwema sana.
Nyimbo za Jud Bucher kama sijakosea jina lake, rege flani hivi, miaka ya 2002, dah acha kabisa
 
Screenshot_20240608-180116_Samsung Music.jpg

Popote ninaposikia wimbo wowote kutoka kwenye hii album. Huwa nakumbuka mbali sanaaa, kikubwa huwa nasemaga Mungu amlaze mahali pema bibi yangu. She's was fighting hard 😪, hii ndo cassette pendwa kwenye radio yetu ya Panasonic, ilikuwa inatumia battery 6. Mama akija kutoka mjini alikuwa anatuletea boxes za kutosha za battery za National. Ila kijijini kwetu zilikuwa zinapatikana sana Tiger head na Bell
 
Nakumbuka nipo Form One wimbo maarufu wa "Fanta Wangu Uliamua" kama sikosei uliimbwa na Orchestra Bima Lee, ukiwa bado ni maarufu, Mzee wangu alipata uhamisho wa kikazi.

Uhamisho huu ulinipelekea kuhamishiwa "boarding" kwani hapo awali nilikuwa bado nasoma "day school" nyakati hizo vijana wa Kidato cha Kwanza tulipitia changamoto nyingi sana hasa kwa vijana wa bweni.

Tuliitwa kila jina baya, njuka, salamander, goromondo, n.k. Nakumbuka nilihamia bweni mwezi Julai, lakini nakumbuka kupitia mimi upuuzi huu wote ulikomeshwa na kufikia ukomo wake. Nilifanikiwa kuwatambua baadhi ya watesi wangu hali iliyopelekea wao kufukuzwa shule moja kwa moja, na hii ikawa ni mwanzo na mwisho kabisa wa kuendekeda ujinga wa kuwahangaisha kijinga vijana wadogo wa Kidato cha Kwanza
Safi sana
 
P funk ft Madee HAYA YOTE NI MAISHA
 
Mimi kwakweli ile album ya wenge musica bcbg yenye nyimbo kama masuwa, bana lunda, ndombolo n.k ilinikuta katika mapito magumu.

Leo hii nikisikia nyimbo yoyote ya kwenye ile album nakumbuka mbaaali sana napata hisia sana ya hata kutoa machozi.

Mungu wetu ni mwema sana.
Nipe - goodluck gosbert
 
Asha wa TID, namkumbuka mtoto mmoja wa kimakonde kutokea Tandahimba huko
 
elimu ya mjinga nimajungu Banza stone.. kile kipindi nilisimamishwa kazi ukitizama ndio nilikua nahitaji pesa haswa kuliko kawaida
 
Acha tu ndugu yangu. Ni nyimbo mchanganyiko ambazo zilikuwa zinanikumbusha jambo flani hivi, .zipo kwenye playlist yangu.
Sasa hivi siwezi tena kusikiliza mziki wowote.
Kiufupi naumwa mwili na roho na sioni matarajio ya kupona.
Unahitaji uponyaji Demi? I am here for you
 
Back
Top Bottom