Mwanajamii pole sana lakini wimbo huo upo sawa kabisa, kwanza zinaa haitokei mpaka mwanamke akubali!!!! Ina maana kama wanawake wakitokea kuwa ngangari na NO zao basi wanaume wangepata taabu sana isipokuwa kwa wale waliopewa YES. Uthibitisho wa hili Quran inataja aya yoyote inayoanza na uzinifu inaanza kwa kusema na MWANAMKE MZINIFU kisha inamalizia MWANAUME MZINIFU na inapotaja kuhusu wizi inaanza na MWANAUME MWIZI kisha inamalizia na MWANAMKE MWIZI. Maana yake haipatikaniki zinaa kwa ridhaa bila mwanamke kukubali na ndiyo maana 20% akasema anajiweka pembeni aepushe malumbano akijua wazi kabisa kuwa jambo hilo la njemba kuwa pembeni mwa kitanda chake hakijatokea kwa bahati mbaya bali kwa makusudi mazima kabisa.
Nikukumbushe mbali kidogo mwanajamii enzi za nabii Yusuph na mke wa Farao pindi mke wa Farao alipomtaka Yusuph, nabii Yusuph alikataa na akaomba ni kheri afungwe kuliko vitimbi vile na Mungu akamjalia akafungwa kweli. Hoja ya msingi hii, kwa kuwa wanawake hawana tamaduni ya kutongoza hivyo basi akitingozwa na kukubali hapo ndipo tendo la ndoa/zinaa linaweza kupatikana.
Hivyo mwanajamii hii ni kama asili tuliyoirithi maana hata ukiangalia kiukweli kati ya mijizi ya kiume na kike ni wazi ya kiume ndiyo imejaa ndiyo maana MUNGU akaonyesha kila kitu kwa asili yake.
Hukusu maamuzi ni sawa kabisa hicho ni kitu ambacho kipo kiasili zaidi kama maumbile yetu jinsi yalivyo, wanawake wanaweza kukosa ustahimilivu katika baadhi ya mambo lakini wanaume wakawa tofauti kabisa mfano kwenye misiba utakuta wanawake wengi ndiyo wanaolia sana kuliko wanaume n.k Hivyo hivyo utakuta wanaume hawana uvumilivu kabisa katika masuala ya mapenzi linapotokea suala kama hilo ulilosema/jengea hoja. Wanaume wamekuwa na jazba na maamuzi magumu/mazito katika masuala mazima ya mapenzi.