Wimbo huu............!!

Wimbo huu............!!

Chorus: Ya nini malumbano, ya nini maneno
najiweka pembeni naepusha msongamano
Bora nitulie ningoje changu na mie
Mola nijalie haya yasijirudie
X2


Washkaji walinambia kwamba demu ni kiruka njia
Nilidhani wamenikamia kunipania nikapuzia
Chezo lilipoanza, nilidanganya naenda Mwanza
Kurudi ndani nilipoanza , nakuta njemba imejilaza gheto

Nenda, nenda, nenda hata kama zamani nilipenda.

Chorus
: Ya nini malumbano, ya nini maneno
najiweka pembeni naepusha msongamano
Bora nitulie ningoje changu na mie
Mola nijalie haya yasijirudie
X2

By 20 Percent.

Ninapousikiliza huu wimbo najiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Lakini kubwa ni hili.
Haya yakiongewa/amuliwa na mwanaume INAELEWEKA katika jamii yetu ila si yakitoka mdomoni/moyoni mwa Mwanamke.... Si kwamba wanaume wao hawana tabia za ajabu kama zilizoelezwa kwa demu huyu wa 20 % lakini wanawake ni wazito kufikia maamuzi ya msimamo huu. Sijui kwa nini? Naombeni msaada.....
kuna mtu alinitumia msg maneno haya,sikujua kama ni nyimbo kumbe,big up 20%,najua mwanangu hamjui baba,toka niondoke uvinza ni miezi 7,mtunze wewe usije kuwa kahaba,ukimbemenda mimi utanibeba money money money imesababisha nikutoroke,na itanirudishe tuwe wote.
 
 
Last edited by a moderator:
Naomba nichangie Pamoja na kutaka usawa kina mama na kina baba naturally tuna tofauti za kimaumbile, kwa upande wa ngono kina baba ni dhaifu sana kwa sababu hisia zao zinavutwa na kuona wakati wakina mama hisia zao ziko mbali na zinasababishwa mpaka aimbishwe yaani apigwe sera ashikwe shikwe. Pia kina mama wana upendo wa kweli hawezi kukubali kukupa tunda mpaka awe amekukubali au awe mfanya biashara dada poa, lakini kwa akina baba anaweza kutembea na mtu for fun labda kavutiwa na miguu yake tu. Suala linalofanya kina mama wanynyasike ni mfumodume na unyonge wa kiuchumi wa mwanamke kwani mwanamke anapoolewa anakwenda kukaa kwa mume hivyo ni rahisi kuteswa kunyanyaswa akavumilia. Swala lingine ni watoto, mila na desturi ufahamu na kiwango cha elimu. Hata hivyo nawashauri wa kina mama mnapaswa kuwa ngangari mzee anapoleta za kuleta usimlegezee atakuletea magonjwa. Kwa ujumla vitendo vya kukosa uaminifu kwa mke au mume vinapswa kulaaniwa na si vya kuvumilika kwa pande zote hivyo havifai.
 
Back
Top Bottom