Wimbo mpya wa Ruby kijembe kwa Mawingu na Ruge

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Habari wakuu,

Nimeusikia kwa mara ya kwanza wimbo wa mwanadada Ruby baada ya kujitoa katika matamasha ya Fiesta. Wimbo unaitwa Wale Wale, mwadada kama kawa kaimba poa sana wimbo unamelody kali sana yaani zile zinaitwaga "Catch Melodies".

Lakini maudhui ya wimbo naona kama katupa jiwe kwa Clouds na Bwana Mutahaba.

 
If u pray for rain you gt to deal with mud... Hii vita ukianza hakuna kurudi nyuma na unapokwenda hupajui. Wish u all the best mdada.
 
Ujue kila mtu ana mazuri yake na mabaya yake. Ila muda mwingine tusahau tusonge mbele? Yeye kabaniwa pesa sawa, mbona yeye alimbania kiumbe, tena juu kwa juu? Hakuwa na haki ya kuishi?Watu wamefanya kazi kubwa wewe kufika hapo, je hiyo ndio shukrani? Katika maisha bila uvumilivu utaangaika sana mpaka kifo chako. Kutoka kulala chumba kimoja na mjomba wako hadi kuwa na sehemu yako sio swala dogo! Mdogo wangu Rubby ukupaswa kuongea wala kuonyesha dalili zozote za kihisia.. Walio kutoa ni kama baba zako hapa mjini, wanajua madhaifu yako mengi sana. Nakusuhii usirudie tena, watu watafurah kwa kile unachoonyesha lakini je watakusaidia nini? Jitazame upya dada yangu. Bongo hii story kila sehemu, kula na maladhi juu yako
 
well said,,,,,
 
Umeongea point mkuu
 
Umeongea point mkuu

Unajua mkuu nimepitia maisha ya shida sana, moja vitu nilivyo pitia ni pamoja na kunyonywa sana au kupunjwa. Pamoja na yote nilikuwa mvumilivu sana, machozi yangu yalikuwa moyoni sio kwa uwazi kama dada Rubby anavyo fanya. Lakini leo nimejua faida ya kupitia yote hayo, leo nikisimama ni mwanaume hasa yote kwa sababu nilikuwa mvumilivu na bado ni mvumilivu. Darasa la saba nimekuja kwa Treni ya ng'ombe hapa mjini. Leo nakula ubaridi kwangu mpaka kwenye usafiri nakula hewa ya Japan sio mchezo. Yote kwa sababu ya uvumilivu. Uvumilivu ni silaha mpaka kwenye mapenzi.
 
Kwa upande wangu naona Ruby kafanya maamuzi mazuri tu,bora mwanaume unanyonywa upande mmoja tu wa kipesa. Dada zetu wananyanyasika sana, kwahiyo wanatakiwa watokee kina Ruby kama kumi hivi hii tabia itaisha. Riziki anatoa Mungu haya mambo ya kuvumilia kila kitu kwa karne hii hayana mashiko. Kama unajiamni na unakipaji kwann uishi kama mkimbizi. Ruby kaza but Mungu atakusimamia tu. Acha na miungu watu
 
Watu kama nyinyi ndo mnawafanya hawa wanakufa masikini kama kweli clouds hawanyonyi wasanii
mafanikio aliyonayo barnaba na kipaji hayaendani
unamjua recho unajua yuko wapi
clouds sio wakuwatetea sema wasanii wanakuwa waoga tu
 
Watu kama nyinyi ndo mnawafanya hawa wanakufa masikini kama kweli clouds hawanyonyi wasanii
mafanikio aliyonayo barnaba na kipaji hayaendani
unamjua recho unajua yuko wapi
clouds sio wakuwatetea sema wasanii wanakuwa waoga tu
Ni kweli
 

Watu wataogopa kuwekeza kwa vijana, kwa sababu, haiwezekani Mtu awekeze kwako harafu ule umzidi. Kuna mifano mingi, kwa mfano, Tanzania mwekezaji anachukua asilimia ngapi? Na Tanzania inachukua asilimia ngapi? Yeye alikuwa afanye miradi mingine njee ya Music. Jina lake katika music ndio libebe biashara zake.. Hakuna pesa inayotosha kama huna miradi au vyanzo mbali mbali vya kuingiza pesa.

Naomba awapigie magoti kisha anipe umeneja wa kumsimamia aone atakavyo nukia pesa, atakuwa hana haja hata ya kulipwa hata sent moja. Kama yule mama alie tumbuliwa kisa hajapokea msharaha miezi kibao uku kazi anafanya. Mama nani vile yule?
 
Watu kama nyinyi ndo mnawafanya hawa wanakufa masikini kama kweli clouds hawanyonyi wasanii
mafanikio aliyonayo barnaba na kipaji hayaendani
unamjua recho unajua yuko wapi
clouds sio wakuwatetea sema wasanii wanakuwa waoga tu

Kuna pesa inayotosha? Nijibu ilo swali.

Wewe tayari unajina kubwa east afrika kwanini jina lako lisiwe biashara? Mtu kama Rubby anaweza hata kutafuta connection akatengenezewa bikini za aina yake.. Kila akiimba bikini inaonekana kiaina aina, mara yupo beach bikini hiyo.. Na uwakika atapata pesa zaidi ya hiyo anayoitaka.. Rubby naomba urudi uombe msamaha, kisha niwe meneja wako hakika utakuwa wa mfano Tanzania, ntakutumia vile inavyotakiwa tupige pesa. Soon tutatoa bikini zinaitwa Rubby hiyo ni moja tu.. 2 nitafute.
 
Acha kumtisha wewe yani kwa vile wamemsaidia ndo akubali kuendelea kuburuzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…