Kuna nyimbo za aina nyingi
1.Biashara mara nyingi hizihazina ujumbe wa maana ni zinauzika sababu ya vibes zilizomo, hizi hupendwa zaidi clubs.
2.Burudani, hizi huburudisha, kuliwaza, kufariji, hizi huleta utulivu tu ndani ya mtu.
3. Ujumbe maalum mfano kampeni ya kitu fulani kubring awareness, matangazo ya bidhaa nk
Hapa pia zipo za ujumbe maalum kwa watu maalum zamani watu walikuwa wakitungiwa nyimbo ngomani kama akifanya tukio lililotrend hutungiwa kupewa makavu yake.
Wimbo huu wa mediocre umeangukia kundi la tatu, ni ujumbe maalum, hauna haja ya kutrend wala kuuzwa au kuvunja record zozote, lengo ni moja tu ujumbe uliokuwa ukimkaba mtunzi kwa miaka ufike kwa mlengwa, na kwa masaa haya sita natumaini mlengwa kapata ujumbe wake.
Hatuhitaji kuucheza clubs wala kuupakua utuburudishe maana hauburudishi wala.
King pole kwa kuumia miaka yote umetoa la rohoni.Haki yako ya msingi tunaiheshimu.