Wimbo wa Diamond Platnumz - WAAH ndio nyimbo namba moja duniani kwa sasa!

Namba moja kwenye nini? Halafu siyo "nyimbo ya" ni "wimbo wa". Siku nyingine ukiandika usome kwanza ulichoandika kabla ya kupost.
 
Mwisha wasiu views za kibongoni utopolo tu.

Kwanza wa promo alilofanya hata kufikisha hizo views bado probably ni failure.

Umetumia masaa kibao kwenye TV uko LIVE kuanzia mapokezi ya Koffi Airport, kurekodi wimbo, kushuti video ( both traditional and social media ).

Gharama ya hiyo promo probably ni zaid ya 10M kama ukiweka gharama.
shida ya mtanzania anaweza asijue mchana atakula nini ila budget za wenzie anazijua a to z
 
Mkuu na wewe umeamini hili? Ngoja nikupe mfano, video ya dynamite ilipata 101 milion views ndani ya saa 24 toka iwe uploaded, How you like that ilipata views 86.4 in milion ndani ya 24 hours ndani ya saaa 24, Icecream views 79 milion

Na ndani ya saa ishirini na nne hizi, video iliyotazamwa sana inaitwa Titlian imetazamwa mara 8.1 milion ndani ya saa 24 hizi, kifuatiwa na bichota mara 6.4 milion.

Hivyo wah ambayo imechukua wiki kufikisha views milion 10 haiwezi kuwa ya kwanza worldwide, labda kama ni Afrika au East Afrika
Boss, kwanini umedeal sana kwenye Youtube wakati kuna platform nyingi sana ambazo zinatumika kujua wimbo namba moja kidunia?
kwa uelewa wangu huwa hawaangalii tu youtube wameifuatilia watazamaji wangapi? ila huwa wanaangalia kwa ujumla platform zote
 
Yes, lazima sasa wewe kama unatangaza target yako ni nini kama siyo kuwajulisha watu.
 
Tanzania hata ufanikiwe vp watu watakuvuta chini walazimishe ufanane wa failure zao, na kuwalazimisha waamini mafanikio yako ni kujiumiza tuu maana hawatakaa wakubali, watakuja na sababu za kwa nini wewe ulichofanya sio lolote wakati wao hata 1% ya hicho hawawezi.
 
When zarithebosslady is Tanzania this diamond shines and his music performances is well.

Nyota ya dai ni zari, she shines him.

Sema tu jamaa haelewi hilo.
 
Boss, kwanini umedeal sana kwenye Youtube wakati kuna platform nyingi sana ambazo zinatumika kujua wimbo namba moja kidunia?
kwa uelewa wangu huwa hawaangalii tu youtube wameifuatilia watazamaji wangapi? ila huwa wanaangalia kwa ujumla platform zote
hata ikiwa hivyo bado hauwezi kuwa number 1 duniani, mitandao mokubwa ya kustream miziki ni spotify, tidal, itunes, google play, amazon.
kumbuka huko kwingine unalipia youtube ni bure. Mziki wetu na afrika in general haujaweza kufika level hizo bado. Wasanii wa afrika wanavunjiana rekod za kiafrika afrika tu si worldwide

Na wao wanalijua hili ndiyo maana mara zote mapambano yao uwa ni youtube, uwa hawaongelei platforms nyingine maana huko downloads na streams uwa si nyingi kama views za youtube
 
Tanzania hata ufanikiwe vp watu watakuvuta chini walazimishe ufanane wa failure zao, na kuwalazimisha waamini mafanikio yako ni kujiumiza tuu maana hawatakaa wakubali, watakuja na sababu za kwa nini wewe ulichofanya sio lolote wakati wao hata 1% ya hicho hawawezi.
Mambo mengine si kushushana chini ni kuset facts straight tu maana otherwise itakuwa kichekesho mbele ya watu kuwa watu wanadanganywa. Haiwezekani wimbo huko kwa wenzetu juzi mpaka jana uwe na views milion 8 ndani ya saa 24, halafu Waah imepata views milion 10 ndani ya wiki iwe ya kwanza.

Ni kuset facts straight. Diamond strategically ni mjanja yani ni kama kampuni ya Apple, Apple walikuwa na tabia ya kusema wao ndiyo bidhaa zao za kwanza kufanya hiki za kwanza kuwa na kile hata kama si kweli. Utaskia the first smart phone, the slimmest phone ever built, the fastest chip. Ni njia ya kujibrand na kibiashara zaidi na kama ina work ni nzuri. Lakini sasa ikifika kwa watu wanaotaka kuset facts straight lazima wajadili siyo kukubali tu.
 
Yaani katika dunia hii ya watu karibu takriban bilioni 8, nyimbo ya kijana wetu, mTanzania mwenzetu, Diamond Platnumz - WAAH ndio nyimbo namba moja duniani kwa sasa. Wizara ya maliasili na utalii itumie fursa hii adhimu kuiambia dunia kwamba Tanzania ina nini cha kuwapa watalii, maana kila mtu anaiulizia Tanzania sasa hivi, hata search rating za Tanzania zimepanda sana kwa sasa.
Video clips zina maelezo zaidi:

Tuwekee lyrics hapa.
Kaimba nini??
 
Mkuu na wewe umeamini hili? Ngoja nikupe mfano, video ya dynamite ilipata 101 milion views ndani ya saa 24 toka iwe uploaded, How you like that ilipata views 86.4 in milion ndani ya 24 hours ndani ya saaa 24, Icecream views 79 milion

Na ndani ya saa ishirini na nne hizi, video iliyotazamwa sana inaitwa Titlian imetazamwa mara 8.1 milion ndani ya saa 24 hizi, kifuatiwa na bichota mara 6.4 milion.

Hivyo wah ambayo imechukua wiki kufikisha views milion 10 haiwezi kuwa ya kwanza worldwide, labda kama ni Afrika au East Afrika
Kuna watu huko viwers milioni 100 in one day
 
Hiyo SIRI haiangalii tu views za youtube kujua nyumbo namba moja, bali inaangalia cummulative engagement ya watu katika platforms zote kama na hasahasa instagram jinsi watu wanavyo repost, kucomment na kufanya challenges mbalimbali za huo wimbo (engagement ndio hasa huketa pesa kwenye marketing); jinsi jina linavyokuwa searched kwenye search engines hasa google, jinsi inavyonunuliwa /kusikilizwa kwenye platforms kama audio mack, amazon, boomplay na nyinginenezo..., statistical dimensions zipo nyingi sana, hata hapa tunapojadili ni kwamba tumekiwa engaged na huo wimbo, Siri inaangali hivi vyote na kujua ipo ndio namba moja kwa wakati husika. Ondoa chuki na legeza ubongo.
 
Boss, kwanini umedeal sana kwenye Youtube wakati kuna platform nyingi sana ambazo zinatumika kujua wimbo namba moja kidunia?
kwa uelewa wangu huwa hawaangalii tu youtube wameifuatilia watazamaji wangapi? ila huwa wanaangalia kwa ujumla platform zote
Platform ya billboard inashika namba ngapi?
 
hata ikiwa hivyo bado hauwezi kuwa number 1 duniani, mitandao mokubwa ya kustream miziki ni spotify, tidal, itunes, google play, amazon.
kumbuka huko kwingine unalipia youtube ni bure. Mziki wetu na afrika in general haujaweza kufika level hizo bado. Wasanii wa afrika wanavunjiana rekod za kiafrika afrika tu si worldwide

Na wao wanalijua hili ndiyo maana mara zote mapambano yao uwa ni youtube, uwa hawaongelei platforms nyingine maana huko downloads na streams uwa si nyingi kama views za youtube
Kweli kabisa
 
Platform ya billboard inashika namba ngapi?
😅😅😅, hii ni sawa na kuuliza nyimbo iliyoshika namba moja billboard imeshika namba ngapi kwenye Clouds top 20 ambapo wasikilizaji ndio hupiga simu na kupiga kura ipi ishike namba moja, nani ataipigia kura Waah? Angalia jibu langu la post namba 36 kwa ufafanuzi zaidi
 
Twende tu haraka haraka!! Kwa hiyo diamond platnumz ndiye msanii namba moja duniani!!! Wimbo wake unaoitwa sijui nini nini ndiyo wimbo namba moja duniani!!! Na wasafi classic ndiyo bendi bora duniani, dah,basi mangufuli babalao
 
Back
Top Bottom