Wimbo wa Hainaga ushemeji umenishangaza

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Hainaga ushemeji ya ManFongo ni wimbo uliobamba sana kwenye hizi nyakati za Tanzania ya wazinzi. Cha ajabu nilikuwa nasikilizaga chorus tu sijawahi kuconcentrate kusikiliza verse zake, jana wakati nimetulia napata moja moto moja baridi nikawa nasikiliza mstari mmoja baada ya mwingine, nikashangaa sana kumbe verse na chorus havina mahusiano kabisa.

Kwenye chorus anazungumzia kitu kingine, verse vitu vingine sasa nikajiuliza huu wimbo umetambaje na kwanini watu wengi wamekomalia kwenye chorus tu au ndo mwisho wetu wa kufikiri ulipoishia? Maana nilichogundua tukiuliza watu 10 waliousikiliza wimbo huo uenda ni mtu mmoja tu anaweza akawa ameelewa verse zinazungumzia nini.

Alichokifanya ManFongo ni kama kwenye kichwa cha habari cha gazeti kiandikwe kuhusu Tetemeko la Kagera halafu kwenye content waelezee kuhusu msambwanda wa Wema Sepetu.
 
Personally napenda mdungo tu! Nna uhakika kuna wengine wanapenda kwa sababu hii
 
Singeri generaly ni mzk wa wauni ndyo maana ata majina yao yana sadifu kma "man fongo.Sholimwamba.Nijaboy" sasa unazan ww apo utaerew Nn
 
Hainaga ushemeji na salome ni nyimbo za kufungiwa
 
Umesikiliza Salome (Diamond ft. Rayvanny) lakini? Huo wa Man Fongo una afadhali kidogo..
 
Upo wap unapata moja Barid moja moto

Waiter zungusha tena..!!![emoji481] [emoji481] [emoji481]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…